Ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika wastawi

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
__172.100.100.3_temp_9500049_1_9500049_1_1_93bd7ff0-597c-4eec-96c1-b1090e0054d7.jpg

Maonesho ya pili ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yamefanyika huko Changsha mkoani Hunan, China, na kushirikisha zaidi ya nchi 40 za Afrika na karibu kampuni 900 kutoka China na nchi za Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya uhusiano wa kirafiki kati ya China na Afrika, ushirikiano wao wa uchumi na biashara umepata mafanikio mazuri.

Maonyesho ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika ni hatua halisi ya kwanza ya utekelezaji wa “Hatua Nane” za kuhimiza ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika zilizotangazwa na Rais Xi Jinping wa China katika Mkutano wa FOCAC uliofanyika Beijing mwaka 2018, ili kujenga jukwaa jipya la ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya pande hizo mbili.

Ingawa China na Afrika zina umbali wa zaidi ya kilomita elfu 10, ushirikiano wao wa uchumi na biashara una historia ndefu. Tangu miaka elfu moja iliyopita, hariri na kauri za China zilianza kusafirishwa kwenda Afrika kupitia meli za wafanyabiashara. Majumba ya Makumbusho yaliyoko pwani ya Kenya bado yanahifadhi vipande vingi vya kauri ya China. Baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, China imedumisha ushirikiano mzuri wa uchumi na biashara na nchi za Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, majukwaa ya FOCAC na pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” yameendelea kuchangia maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika, na ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya pande hizo mbili pia umeongezeka na kukua siku hadi siku.

Kulingana na takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Mamlaka kuu ya Forodha ya China, tangu kuanzishwa kwa FOCAC, thamani ya biashara kati ya China na Afrika imeongezeka kutoka dola bilioni 13.5 za Kimarekani mwaka 2000 hadi dola bilioni 201.5 za Kimarekani mwaka 2020, na wastani wa ongezeko la kila mwaka umekuwa asilimia 14.5. China imekuwa mwezi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 12 mfululizo.

Ushirikiano wa uchumi na biashara ni moja ya sehemu muhimu zaidi ya uhusiano kati ya China na Afrika. Ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea, China ina mfumo kamili zaidi wa uzalishaji wa viwanda na soko kubwa zaidi la bidhaa na huduma duniani. Kwa upande mwingine, likiwa bara lenye nchi zinazoendelea nyingi zaidi, Afrika ina maliasili nyingi na soko linaloendelea kukua kwa haraka. Ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya pande hizo mbili una nafasi pana ya ukuaji.

Katika miaka ya hivi karibuni, China na nchi za Afrika zimenufaishana katika ushirikiano wao wa uchumi na biashara. Bidhaa za China zenye bei rahisi na ubora wa juu zimeingia kila mahali barani Afrika. Wakati huohuo, kampuni za China pia zimeanza kuzalisha bidhaa katika nchi za Afrika, na licha ya kukidhi mahitaji ya wenyeji, bidhaa hizo pia zinauzwa kwa nchi za nje, jambo lililoongeza pato la kitaifa la nchi hizo za Afrika. Kwa upande mwingine, licha ya kutoa bidhaa kubwa zikiwemo mafuta na madini kwa China, katika miaka ya hivi karibuni, bidhaa nyingine bora za Afrika pia zimeingia kwenye soko la China. Kwa mfano maua ya Kenya, kahawa ya Rwanda, na matunda ya Afrika Kusini vinapendwa sana na wateja wa China. Takwimu zinaonesha kuwa maagizo ya China ya mpira, pamba, kahawa na bidhaa zingine za kilimo kutoka Afrika yameongezeka mara mbili katika mwaka uliopita.

China na Afrika ni marafiki, wenzi na ndugu wakubwa. Kutokana na juhudi za pamoja za pande hizo mbili, ushirikiano wao wa uchumi na biashara utakuwa na mustakabali mzuri zaidi, na kuendelea kuchangia juhudi za kutimiza ndoto ya Wachina ya ustawishaji wa taifa la China na ndoto ya Waafrika ya mshikamano na maendeleo.
 
Back
Top Bottom