Ushiriki wa JWTZ katika 'Operesheni Tokomeza'

Hayo matukio machache ambayo nakiri yametokea,yasilipake tope jeshi letu!!kwa mtu ambaye amewahi kuishi nchi zenye political instability kama Rwanda,sudan,Iraq,Afgh huwezi kubeza displine ya jeshi letu hata siku moja,mambo ya kijeshi usije uka relate na siasa hata siku moja-kumbuka jeshi ni muhimili mkuu wa serikali na sio chama ,chuki za kuichukia ccm zisikufanye uichukie TPDF ,Congo wenzio wanasali wangekua na jeshi lenye nidhamu kama JWTZ wangekua mbali kimaendeleo.
Zisikie mbali kabisa habari za uasi wa jeshi(highest level of indispline)
ndugu sisi hatuna political instability!na waasisi wa taifa hili waliwekeza kwa hali na mali katika kujenga Jeshi la Wananchi wa Tanzania sio jeshi uchwara la kutumiwa na wanasiasa wachovu.hivi mtaji wote huo tuliowekeza ktk kulifanya jeshi letu liwe la ulinzi wa watanzania miaka nenda rudi ndio zimeishia hapa kwenye jeshi uchwara linalojisifu kutumia mbinu za kivita dhidi ya watu walewale walioapa kuwalinda?hakuna excuse hapa!hili jeshi limetumika kama toilet paper na limejichafua lenyewe!na kama limebakiwa na chembe yeyote ya sifa za jeshi profesional basi wahusika wavuliwe nyadhifa zao na kuwa court marshalled.full stop!vinginevyo aibu ya uozo wa utawala wa nchi hii umeshaingia huko jeshini pia....kale kajeshi kenye nidhamu alikojitahidi kukajenga Nyerere sasa Kananuka!
 
Halafi wavimbiwa wa masisiem wanasema ombeeni taifa liwe na amani huku wanafanya unyama huu kwa raia wasiokuwa na hatia....inauma sana
 
ndugu sisi hatuna political instability!na waasisi wa taifa hili waliwekeza kwa hali na mali katika kujenga Jeshi la Wananchi wa Tanzania sio jeshi uchwara la kutumiwa na wanasiasa wachovu.hivi mtaji wote huo tuliowekeza ktk kulifanya jeshi letu liwe la ulinzi wa watanzania miaka nenda rudi ndio zimeishia hapa kwenye jeshi uchwara linalojisifu kutumia mbinu za kivita dhidi ya watu walewale walioapa kuwalinda?hakuna excuse hapa!hili jeshi limetumika kama toilet paper na limejichafua lenyewe!na kama limebakiwa na chembe yeyote ya sifa za jeshi profesional basi wahusika wavuliwe nyadhifa zao na kuwa court marshalled.full stop!vinginevyo aibu ya uozo wa utawala wa nchi hii umeshaingia huko jeshini pia....kale kajeshi kenye nidhamu alikojitahidi kukajenga Nyerere sasa Kananuka!

tatizo hujalewa nini ni nini!!,rais kama amiri jeshi mkuu anapotoa amri kwamba kitu flan kifanyike huwa kinachofuata ni utekerezaji na sio hapana kama wewe unacolazimisha iwe.we unaenda moja kwa moja kulilaumu jeshi wakati amri inapokelewa kutoka juu na kufanyiwa kaz.

tatizo hapa ni je kulikuwa n umuhim wa kulishirikisha JWTZ???,we ulitaka CDF,akatae amri ya Amir jeshi mkuu??,ama hujaelewa hata unachoandika?Maandaliz duni ya opareshen na kuchukulia mambo juu juu ndo tatizo kubwa sana katika mfumo hapa kwetu
 
Back
Top Bottom