Ushiriki wa JWTZ katika 'Operesheni Tokomeza'

Siku zote nimekuwa nikisema, nalichukia JESHI letu, hasa roho mbaya za wanajeshi! Mimi sielewi hao wabunge wanaopigia debe muda wa wanafunzi kwenda Jeshini uongezwe kutoka miez 3 hadi 6 kama wanjua madhila wanayokutana vijana wetu, cjui wanataka wafundishwe roho mbaya...
 
Kama hawa ndio wanaowafunda vijana wetu, sioni ni kwa nini huo mpango usisitishwe...
 
Mkuu nakubaliana na wewe. Nchi hii kazi kubwa ni kupiga siasa wala sio kufanikisha chochote. Taratibu za kawaida za kiraia zilishagonga ukuta ndio maana ikaonekana itumike operation. Sasa hapo si lazima kuwe na tofauti?
 
Tanzania hatuna Aman! Bali ni waoga na tuko washamba! Kila siku tunaambiwa ni Nchi ya Amani tunashangilia.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
!
!
ipo siku tutawazoea hawa wanajeshi just like tumewazoea askari polisi.

ipo siku tutasema na retreat no surender.........f.u.k the army
 
Tanzania hatuna Aman! Bali ni waoga na tuko washamba! Kila siku tunaambiwa ni Nchi ya Amani tunashangilia.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Kinachosikitisha zaidi ni kuwa hili lilikuwa tatizo la mkuu wa majeshi na amiri jeshi mkuu, lakini wala hawatajwi kuwajibika...
 
waziri mmoja amejiuzulu hao wengine wametimliwa na mh hao wengine wanangoja nn?ikiwa mabosi wametimliwa unakuta mtu anapewa nafasi ya uwaziri anashindwa kabisa kuona matatizo ya watanzania matokeo yake ndio hivi tunapigwa na tunapata ulemavu harafu haohao wengine wako bussy kuusaka uraisi sasa umuongeze nani ikiwa haya matatizo umeshindwa kuyaona roho mbaya tu hutufai jk piga chini watu hawa na wasipewe nafasi
 
Hayo matukio machache ambayo nakiri yametokea,yasilipake tope jeshi letu!!kwa mtu ambaye amewahi kuishi nchi zenye political instability kama Rwanda,sudan,Iraq,Afgh huwezi kubeza displine ya jeshi letu hata siku moja,mambo ya kijeshi usije uka relate na siasa hata siku moja-kumbuka jeshi ni muhimili mkuu wa serikali na sio chama ,chuki za kuichukia ccm zisikufanye uichukie TPDF ,Congo wenzio wanasali wangekua na jeshi lenye nidhamu kama JWTZ wangekua mbali kimaendeleo.
Zisikie mbali kabisa habari za uasi wa jeshi(highest level of indispline)
 
Katiba Mpya itamke waziwazi kwamba ni marufuku kwa JWTZ kujihusisha katika masuala au operesheni yoyote ya kiraia au kisiasa isipokuwa katika mazingira ya hali ya hatari, ugaidi, au uokozi katika majanga. Haki za binadamu na kiraia lazima ziheshimiwe mahali popote na katika mazingira yoyote ambapo operesheni za kipolisi zitakuwa zinafanyika.

Ni kosa kwa kiongozi yeyote wa kiserikali kutoa matamko au vitisho vyenye mwelekeo wa kuwatisha au kuwaogofya wananchi katika masuala ya kisiasa. Adhabu itakuwa kifungo cha miaka mi5 jela. Ni kosa kwa kiongozi wa kidini kutoa matamko au vitisho vyenye mwelekeo wa kuwatisha au kuwaogofya wananchi katika masuala ya kisiasa. Adhabu itakuwa kifungo cha miaka 8 jela.

Ni kosa kwa kiongozi wa kijeshi kuzungumzia au kujihusisha na suala lolote la kisiasa kwa namna yoyote ile. Adhabu itakuwa kifungo cha miaka 30 jela. Natumaini Shimbo muda huu angekuwa ananyea ndoo.
 
Ni kweli yote uliyoyasema. Kama mambo siyo critical kwa kiwango ambacho kinaweza kutatuliwa na jeshi letu la polisi, JWTZ lisitumike. Jeshini hamna kubembeleza raia, na kwa hakika jeshi ndivyo linavyopaswa kuwa, sasa kabla ya kutuma vikosi vya JWTZ tathmini ya kina ifanyike ili kujua kama kuna ulazima wa kuwahusisha walinzi wetu hawa wa mipaka na ofcourse na amani pia, bila kusahau uokozi wakati wa matukio ya dharura.
 
Kwahiyo hata huko wanakoenda kutunza/kurudisha /kulinda amani huwa hakuna discussion? Tatizo la Jeshi letu bado limerithi mambo ya kikoloni, hata hapa Ikola Mpanda huwa wanakuja wanafanya fujo wanachukua wasichana na wake za watu semehu za starehe kwa lazima muda wa Usiku na gari lao la Landlover ukitaka kujitetea wanakuchukua wanakupeleka kambini gwao unaenda kupata kipigo huwa najiuliza hivi huyo Co wao haoni kuwa nitabia za kinyama. Sasa hebu fikiria kambi kama hii ukawapeleka kwenye hizo operation si ndo watafanya mambo kama yalivyofanyika, tusishangae Wanajeshi wa nchi hii ndo wanavyofundishwa ingawa utawasikia wakuu wa majeshi wakikanusha kwenye vyombo vya habari, nawashauri wakuu wa vyombo vya ulinzi wawabadilishe fikra askari wao ili wajue wajibu wao ni upi ktk jamii.

Mkuu Free ideas,

Una haki ya kusema hivyo. Lakini umeeleza jeshini hakuna cha dscussion kama ilivyoagizwa ni hivyo, sasa SWALA ni kwamba hawakuelzwa majukumu yao ktk hiyo operation. Kama wanajeshi wanafanya walichoelezwa na makamanda wao na hawawezi fanya vingine basi wangepewa very clear mission basi haya mambo yasingetokea. Nina wasiwasi na hao viongozi wao hasa mkuu wa operation. Hawakuelezwa what should be achieved and under which conditions!

Kwa kifupi ni kwamba hata iwe jeshi kama kuna clear mission haya makosa hayawezi kutokea. Pili lazima tujue na viguma kwa watanzania kufanya vitu vya kutumia akiri na kuwaza zaidi. Watanzania hasa wale ambao wako ktk nagazi za uongozi iwe siasa au hata nje ya hapo SWALA LA KUTUMIA AKIRI NYINGI NA KUWAZA HALIPO what counts first ni je kuna CHOCHOTE HAPA!!!!!!!!

IT IS A SHAME KUWA NA WASOMI AMBAO HAWAWEZI KUTUMIA AKILI KIDOGO KUFIKIRI KABLA YA KUTENDA KITU. WASOMI WETU THEY CANNOT DELIVER ANYTHING AT ALL. HII NDIYO TANZANIA YA SASA. MWALIMU NYERERE MASIKINI AMEONDOKA NA TANZANIA TUNAYOYIJUA!!!!!
 
Mkuu nakubaliana na wewe. Nchi hii kazi kubwa ni kupiga siasa wala sio kufanikisha chochote. Taratibu za kawaida za kiraia zilishagonga ukuta ndio maana ikaonekana itumike operation. Sasa hapo si lazima kuwe na tofauti?

asante mkuu,ndo mana nikasema,unapoamua kulitumia jeshi,tegemea lolote na kwa maana rahisi ni kwamba ni jambo serious.pia inamaana kwamba idara zingine zimeshindwa.

kwa maana hiyo jeshi litatumia nguvu hata extra maana haliwezi kubali kushindwa,na itakuwa aibu kushindwa maana jeshi ngazi ya mwisho kwa swala la ulinzi.

Muhimu hapa ni serikali kuwa makini na ushiriki wa JWTZ katika mambo ya ndani ya nchi ambayo yangeweza hata kumalizwa na idara nyingine.Isije fika siku JWTZ wakaitwa eti kuna majambazi yamevamia benki
 
Hayo matukio machache ambayo nakiri yametokea,yasilipake tope jeshi letu!!kwa mtu ambaye amewahi kuishi nchi zenye political instability kama Rwanda,sudan,Iraq,Afgh huwezi kubeza displine ya jeshi letu hata siku moja,mambo ya kijeshi usije uka relate na siasa hata siku moja-kumbuka jeshi ni muhimili mkuu wa serikali na sio chama ,chuki za kuichukia ccm zisikufanye uichukie TPDF ,Congo wenzio wanasali wangekua na jeshi lenye nidhamu kama JWTZ wangekua mbali kimaendeleo.
Zisikie mbali kabisa habari za uasi wa jeshi(highest level of indispline)

uko sahihi,na ndo mana hata katika uzi wangu sijaonesha kulibeza jeshi ila wachangiaji kila mmoja na mawazo yake.Naliheshim sana JWTZ na nina imani kubwa sana na lo.Tatizo langu ni wanaorishirikisha jeshi katika inshu ambazo hazina ulazima wa kulishirikisha.
 
Naliheshimu sana jwtz...
ila naichukia serikali ya ccm kwa kuingiza siasa kwenye jeshi la police ndio maana operation nyingi zinakwama..
 
uko sahihi,na ndo mana hata katika uzi wangu sijaonesha kulibeza jeshi ila wachangiaji kila mmoja na mawazo yake.Naliheshim sana JWTZ na nina imani kubwa sana na lo.Tatizo langu ni wanaorishirikisha jeshi katika inshu ambazo hazina ulazima wa kulishirikisha.

Umeisoma repoti ya kamati vizuri? Mbona naona tuhuma nyingi zimepelekwa kwa polisi na KDU?
 
Umeisoma repoti ya kamati vizuri? Mbona naona tuhuma nyingi zimepelekwa kwa polisi na KDU?

nimeisoma vizur sana mkuu,lakini mbali na tuhuma nyingi kupelekwa huko polisi na KDU inafahamika kabisa nani alifanya nn na wapi,kwenye Report kuna mahalai anataja tu vitendo bila kutaja nani alihusika,.nimefuatilia na kujua nani alihusika kwa kipi ndo maana nikaandika mkuu.

Na kinachozungumzwa hapa kwa uzi wangu ni ulazima wa JWTZ kushiriki opareshen TOKOMEZA na sio nani katajwa sana kwenye Report ..thax
 
Upo sahihi kabisa na hili tangu mwanzo watu wengi walionya sana kuihusisha JWTZ kwenye shughuli ile lakini serikali haikusikia na matokeo yake ndiyo haya. Tunao polisi wengi sana yanini kuwatumia wanajeshi? huwa sionagi mantiki ya kukimbilia kuwatumia wanajeshi angalia hata kule mtwara walipeleka wanajeshi wakati polisi wapo?!
si useme tu rais KIKWETE hakusikia au aliamua hivyo!!
 
Serikali yoyote ile inayoamua kulitumia jeshi kupambana na wananchi wake ni ya kidhalimu na ya kifashisti. Jemadari anayeliruhusu jeshi kutumika dhidi ya wananchi wake ni wa kuchukuliwa hatua ikiwemo kuvuliwa cheo na kufikishwa mahakamani...huyo ni adui wa taifa na hana tofauti na kamanda wa jeshi la uvamizi. Kiongozi yeyote wa nchi anayeamuru jesho kufanya uovu kama huu ni wa kukamatwa na kufikishwa kwenye mahakama za kimataifa.

Mag3: Your signature speaks for itself. I will say no more.
 
Back
Top Bottom