Wakina Lissu na Mbowe wapige operesheni angalau kwa wiki moja chama changu kiamke usingizini. Viongozi wa CCM wamelala sana

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
878
4,108
Operesheni 255 iliyopigwa kanda ya ziwa na Kusini iliwaibua akina kinana na Chongoro kuingia mtaani. Waliposhindwa kushawishi watu ikalazimu ateuliwe Naibu WAZIRI Mkuu ambaye naye pia amepita mtaani watu wamemkataa kimtindo.

Lakini pia operesheni ile iliondoka na katibu Mwenezi na baadaye umeondoa Katibu Mkuu wa Chama changu. Kupitia operesheni ile tumeona mabadiliko ya baraza la mawaziri na wajibu hoja wameongezeka wizarani.

Niwaombe akina Mbowe na kikosi chake kiingie tena mtaani yapo mambo mengi yamekwama. Mkisimama majukwaani watu wanakosa usingizi. Anzeni mwaka mpya kwa non stop wananchi tukumbukwe na wakubwa watumbuane.
 
Labda operation za ngiri maji na matende lakini kwenye siasa jamaa zako wameshajifia!
 
Kwenye siasa lazima ujibalansi usichokwe, ukianza mapema unatoa muda mwingi wa counter attack, ukipiga shambulizi la karibu na uchaguzi, mfano miezi mitatu minne kabla, adui atabaki anaweweseka.

Huu ni muda wa kujisuka kwenye matawi ili ukifanya shambulio unakuwa na infantria ya kutosha, ndicho inafanya CCM.
 
Back
Top Bottom