Mnawaonea sana Clouds Duh! Hivi nani aikuambieni kuwa taaluma ya utangazaji ni kuwa na IQ kubwa, kujua kila kitu? Sio kweli, jaribuni kufanya assessment ya watangazaji wazuri kwenye vituo vyote mtagundua kwamba sio kusoma sana bali ni ujanja ujanja ndio unaomsaidia mtangazaji kuwa vizuri (kipaji).
BTW umewahi kujiuliza kama Div 1 nzuri za form six haziendi kusomea utangazaji wa habari? Hii ni kazi ya kijanja janja, unasomea kazini na uzoefu ndio unaokujenga. Watangazi wa Clouds hawana tofauti na watangazi wa radio zingine hapa TZ, hii clouds tunayoilalamikia ndio kila siku tunaisikiliza kwenye magari yetu ndio maana tunapata muda wa kuwaponda.
Huwezi kusema yule baba/mama anakoroma usiku akilala kama hulali naye, haya maswala yanatakiwa yawe kama maoni tu. Mnadhani ni asilimia ngapi wanavijua vipindi vya Kiss FM, Times FM, EA Radio, TBC FM, RFA, Magic FM, Radio Tumaini, Praise Power Radio, Radio Iman na Radio One zaidi ya wanavyovijua vya Clouds FM?