fyddell
JF-Expert Member
- Dec 19, 2011
- 11,210
- 20,246
Haha nimecheka sana baada ya kusoma Visa vya wadau, ngoja nishee nami hiki kimoja. Niko na best friend wangu/ classmate wangu (may his soul rest in peace) mapumziko, kumbe alikuwa na ugomvi na vijana wa form two, sisi form one. Gafra jamaa wakaibuka tulipokuwa tunakula mihogo wakaanza kumzingua, kuona vile nikashindwa kumuacha mshkaji wangu akionewa wakati mi nipo. Nikachomoa kuni kwenye jiko la mihogo na kuanza kuwatembezea wale jamaa. Wakati napambana nao, kumbe mshkaji wangu alikuwa amekimbia pembeni na kuokota mawe na kuanza kuyarusha kwa wale washkaji nami nipo katikati yao. Ile nageuka tu, jiwe likatua juu ya jicho, damu zilizoruka pale sijawahi ona. Jamaa wote na mshkaji wangu wakakimbia, mimi kilio juu huku nimeshikilia pale nilipopigwa na jiwe, uniforms zote zimelowa damu.
Baada ya hapo sikuingilia tena ugomvi usionihusu
Baada ya hapo sikuingilia tena ugomvi usionihusu