Ushawahi kumuuguza mtu mwenye matatizo ya akili?

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
14,840
31,583
Habari JF,

Ningependa kujua subjective experiences zenu kuhusu kichaa.

Ushawahi kuumwa kichaa? Ushawahi kukumbana na kichaa? Ulijuaje huyu ni kichaa? Wewe au familia yenu mshawahi kuwa na kichaa? Mlienda wapi kutafuta msaada? Hospitalini? Kanisani? Kwa Mganga?

Alipona? Alipona kabisa, au alirudia kuumwa?

Nini mtazamo wako kifanyike kusaidia vichaa na familia zao, at Individual level, family support and at national level?

I know its a taboo subject, ila ningependa kuona uzoefu wenu. LETS TALK ABOUT IT hapa, tuko anonymous usiogope, kama vipi njoo na ID yako afu utiririke. 😂 😂
 
Nilikutana mwaka juzi na mama mmoja, mwanaye amejifungua akapatwa kifafa cha mimba kikapelekea ukichaa kamili, hawakujua wakawa wamemleta kwa mchungaji mmoja maarufu ati aombewe ana mapepo!

Dada ana nguvu huyo, nikasaidia kuwapeleka kitengo cha wagonjwa wa akili, mle nikaingia!
Inatia huruma, vichaa kumbe vinatibika tu bwana; yule dada ametumia dawa kwa muda mrefu now ni mzima, ila hana kumbukumb kam ana mtoto😭😭😭😢😢!aliniuma balaa mikono!

Mungu awasadie wagonjwa wa akili jamani..ingawa na humu wamo!👯
 
Haya maswali mkuu mtu akiyajibu kwa ufasaha kwa kirefu atakuwa ameandika paper kabisa. Ungeuliza moja kama lililopo kwenye title then mengine ungechomeka kulingana na response za wadau. Ila uko vizuri, it seems you are conducting a research YES?
 
No i'm not doing any research..not at the moment Mkuu,..hayo maswali nimeweka tu,kama unaweza kujibu maswali mawili au yote,yote ni sawa tu...na kama unaona the thread is lacking something unaweza uka add Mkuu.
 
Daahh kuna sehemu huwa naenda na kuna mama mmoja ni kama amerukwa na akili kutokana na kichaa cha mimba wakati wa kujifungua. Huwa namuhurumia sana na mbaya zaidi wameshafanya kila njia lakini ndio hivyo

inasikitisha kiukweli
 
Kwanza naomba nikurekebishe kwamba kiswahili fasaha ni wagonjwa wa akili/magonjwa ya akili. Kwenye kamusi ya kiswahili hatuna msamiati wa kichaa. Kwa kimombo tunaita mental disorders/illnesses..

Haya magonjwa yamegawanyika katika makundi yafuatayo, soma kwa makini huenda na wewe msomaji umo kwenye kundi mojawapo:

1. Magonjwa ya Mhemuko (Mood disorders) kama vile unyogovu(depression) na mfadhaiko wa akili (bipolar disorder).

2. Magonjwa ya Wasiwasi (Anxiety disorders).

3. Magonjwa ya Kuvurugika Haiba ya Mtu (Personality disorders).

4. Magonjwa ya Kisaikolojia (Psychotic disorders) kama vile Schizophrenia.

5. Magonjwa ya Kula (Eating disorders).

6. Magonjwa ya Kiwewe (Trauma-related disorders) kama vile msongo wa mawazo baada tukio baya ama kusikitisha mfano ajali au kufiwa (Post-taumatic stress disorder).

7. Magonjwa yatokanayo na Kubwia Madawa ya Kulevya (Substance abuse disorders).

Kwa hiyo ukiangalia hizo categories kila mmoja wetu lazima ataangukia kundi fulani Japo unaweza usiwe na sifa zote za kuitwa mgonjwa wa akili.

Cc Unforgetable
 
Wagonjwa wa akili huwa watata sana pale wanapokuwa kwenye acute state (muda ambao kichaa kinapanda juu zaidi). Aisee, huu ndio ule muda ambao unatakiwa muwe makini mnoo maana kuua kwake ni kitu cha kawaida sana.

Muda huu wanakuwaga na nguvu zisizomithilika, na bahati mbaya hata wakiua kisheria hawana kosa.

Unforgetable
 
Nina dada angu ni kichaa anachukua dozi muhimbili, Kuna mtukio mengi mabaya yanatokea kwenye jamii watu huwa wanamlaumu muhusika lakini kwa experience ninayoipata kwa dada angu ugonjwa wa kichaa ni ugonjwa hatari na serikali ipo kimya.

Huyu sister akiwa njian ukiambiwa mgonjwa unakataa kabisa na ana biashara zake kabisa. Shida akiacha dawa wanaojua ndio wanaelewa mtu baki unaweza sema anajifanyisha
 
I feel you man, usiombe aache dawa halafu kipande, mtajutaa

Cc Unforgetable
 
Asante kwa kunisahihisha Mkuu, niikua nataka nije na topic ukisikia kichaa unafikiria na nini ili watiririke..LOL...kuna lugha unayobidi uitumie mtaani sio kama ofisini. Inaweza umemaanisha kitu kimoja, ila uwasilishaji ikawa kawa tofauti mental illnesses/ Magonjwa ya akili. ni clusters of many mental conditions. Ila nimegundua kwa kikwetu kichaa wengi wana refer to patients with Schizophrenia...na ndio ilikua target yangu… Asante.
 
Nina dada angu ni kichaa anachukua dozi muhimbili, Kuna mtukio mengi mabaya yanatokea kwenye jamii watu huwa wanamlaumu muhusika lakini kwa experience ninayoipata kwa dada angu ugonjwa wa kichaa ni ugonjwa hatari na serikali ipo kimya.

Huyu sister akiwa njian ukiambiwa mgonjwa unakataa kabisa na ana biashara zake kabisa. Shida akiacha dawa wanaojua ndio wanaelewa mtu baki unaweza sema anajifanyisha

Kwa wale mnaotibiwa sasa hivi ..msiache dawa ni muhimu,Asante Mkuu Beef Lasagna
 
Back
Top Bottom