Kuna jamaa alikua anasoma Udom, alikua anakuja kwa kaka yake ambae amepanga nyumbani kwetu. Tunacheki movies, mpira na kutembea mtaani pamoja. Udom tulikuwa tunakula nae kwa wajasi ng'ox 2010's.
Ila siku moja nikamkuta katika shule flani hivi anafundisha, nilikua nimeenda kufanya usahili maana waliniita. Mkurugenzi alivyoona Udom, akasema tena mwenzio yuko hapa na akamwita, kisha akamuuliza;unamfahamu huyu? Niwenzio wa Udom. Jamaa bila hiana kasema hanijui.
Lakini jioni tunakutana kitaa ananiita jina langu na kuanza kumung'unya maneno yasiyoeleweka. Kiukweli huwa inaniuma hadi leo, usiombe kukanwa hadharani tena mbele ya macho yako mchana kweupe, utatamani kulia hutaweza, roho itakuuma sana sana sanaaa.