Leo nimeamini si kila anayeitwa mchawi au mshirikina kisa mali ni kweli

ryan riz

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
422
675
Ndugu hii dunia ina mambo ya ajabu unaweza yakakukuta usijue yalianza vipi mpaka yakafika hapo yalipo. Mimi ni mtumishi wa serikali yaani kifupi ni Mwalimu Idara ya Sekondari, sasa kulingana na kamshahara ketu huwa kidogo huwa hakatoshelezi mahitaji nilijiongezaga kwenye vibiashara vya kuunga unga.

Baada ya mtaji kukua nikaingia kwenye biashara ya mkaa bila hata kuwa na kibali, nilifikia kuwa na mtaji wa gunia 300 japo nlipitia changamoto nyingi kwenye biashara hiyo kutokana na kutokuwa na kibali pia kugombana sana na mkuu wa kituo(MKUU WA SHULE) pindi kwenye harakati hizo ila sikukata tamaa. Nashukuru Mungu nliweza pata faida ya kama 15+milion, nikajiingiza kwenye biashara ya Nguo za kina dada nikawa na duka kubwa tu na kwa vile nashukuru Mungu kwa kunipa lugha nzuri na ya ushawishi nilijengenezea wateja wengi tu.

Nilimweka dogo kwenye duka langu nikitoka kazini tunaenda kusaidiana na dogo. Hapo kulingana na faida nayoipata nilikuwa nanunua viwanja najiwekea wala sikuwa na mpango nao kuvijenga ila lengo lilikuwa nikikwama kwenye biashara nitumie kuvikopea mkopo.

Baada ya miaka kama miwili nilifikisha viwanja kumi, watu walijua mimi kama dalali wa viwanja hivyo marafiki na marafiki wa marafiki wakawa wananitumia kutafuta viwanja, hii ikanishawishi nikaiingia rasmi kwenye kazi ya udalali wa viwanja na kwa kuwa na mtaji wa vile viwanja kumi ikawa nauza na kununua viwanja, huku nakomaa na biashara ya nguo na UALIMU wangu. Nilijikuta nyumba yangu ya kwanza nimeijenga kwa uharaka ila haikuwa nzuri sana japo kiwanja kilikuwa na sqm 1300. Baada ya mwaka eneo lilobakia nikajenga mavyumba kama shule yaani yamezunguka kiwanja chote kama fensi, humo ndani kukawa na nyomi la wapangaji.

KISA CHA MADA HII KILIPOANZIA
Mimi ni mtu wa kuficha mambo yangu nayoyafanya huwa sipendi sana kumwambia mtu kama nafanya maendeleo flani sababu najua nafanya kwa ajili ya maisha yangu na si kwa ajili ya mtu. Kutokana na mishe ya udalali ya viwanja nilipata viwanja vinne maeneo ya watu wazito na mimi nilipanga kuja kuvifanyia vitu vizito. Sasa bahati iliyotokea pale kwenye ile nyumba yangu kama Treni kuna jirani yangu alikuwa ananyumba kali alipata matatizo flani kazini kwao baada huyu bwana mkubwa kuingia madarakani ya ubadhilifu wa fedha ya umma, akawa anaipiga bei nyumba yake na mimi alinifuata akananiambia bei yake, kiukweli ilikuwa chini kulinganisha na nyumba ilivyo. Hapa ndio ukawa wa mwanzo wa neema kwangu nyingine zaidi ya Mungu alizonijaalia awali.

Ile nyumba niliinunua nilichanganya akiba yangu na nashukuru Mungu nilikuwa sijawahi kukopea mshahara wangu hivyo nilikopa kahela kidogo karefu maana mwaka jana ndio nilipanda daraja na nikachukua huo mkopo na kuchanganya na akiba nikawa na kama 40+milion, na nyumba ile bei yake ilikuwa inauzwa kwa bei hiyo.

Sasa baada tu ya kununua miezi miwili tukaambiwa eneo lile tunapitiwa na SGR, Hapo mzee wangu akaanza kuumwa huko Mwanza alilazwa Bugando, nikaomba ruhusa kazini kwenda kumuuguza, pindi nipo nauguza dogo akawa ananipa taarifa kwamba watu wa SGR wameshatathmini, ikafika muda wa kupeleka acc. kwa ajili ya malipo nikachomoka hospitali nikaja kusign fomu zao, nikarudi Mwanza kuendelea kumuuguza mzee.

Sasa kama mnavyojua watumishi wa serikali kuna muda ruhusa ufikia ukomo baada ya kubebana sana ikabidi nirudi job. Sasa nilivyorudi dogo alienda kule Mwanza alipolazwa mzee. Mimi nikaanza kununua tofali ili nianze ujenzi mpya kwenye kiwanja moja wapo kati ya vile vinne kwa sababu nilijua pale tunapokaa hatuna chetu tena miezi kadhaa huko mbeleni.

SASA NDUGU MALIPO YALITOKA YA SGR NA HAPA MKASA NDIO ULIPOANZIA.Nashukuru Mungu lile Treni langu(nyumba kama shule) lilitoa hela ya maana sana na ile niliyonunua ilizaa faida mara mbili. Hivyo vile viwanja niliachia mikwaju ya maana kule ushuani kwa pamoja na ile ambayo nilianza peleka tofali kwa ajili ya kukaa mimi nikaicha kwanza.

Mwenyezi Mungu aliongeza neema zake maana kwa kuwa serikali ndio imehamia mkoa naokaa mimi na nilikuwa na kiwanja kikubwa karibu na maofisi yao wanayojenga njia ya kwenda UDOM basi alitokea mdosi kwenye maofisi yao alikipenda kile kiwanja kwa ajili ya biashara zake, alikinunua kwa hela nzuri sana maana bei niliropoka ili asinunue sababu hata mimi nikuwa na mpango nacho kwa baadae.

Hivyo ile hela ukijumuisha chenji SGR iliyobaki baada ya kujenga nyumba tatu bora kabisaa za kupangisha.Nilijenga kiukweli nyumba ya ndoto ya vijana wengi sana. Balaa lilianza baada ya mwezi kuhamia mtaa ule wa kishua kumbe majirani zangu walijuaga mimi ni msimamizi tu wa zile nyumba japo hazikuwa zinafuatana karibu karibu, sasa mwezi huo huo mzee alifariki hivyo kibinadamu tu niliwapa taarifa msiba wa Mzee na kwa mtaa ule wanakaa maafisa wengi walianzishaga chama cha wababa kwa lengo la kutambuana na kusaidiana kwenye maswala kama hayo.

Tatizo lilianza mimi kutoa taarifa ya msiba wa mzee, kumbe kuna watu wanavijihela na wasomi tu ofisi kubwa kubwa ila nimafa....la sana, yaani msiba ndio ulifungulia MANENO MANENO yote kwamba mimi nimemuua mzee ili nitajirike haiwezekani kwa Mwalimu kujenga nyumba nne kwa mpigo tena eneo lenye viwanja bei ya juu. Kumbe mimi nimeanza kununua viwanja kabla wale kenge majirani zangu wengi wao ambao wameletwa na Magufuli kuwatimua huko walipokuwepo na kuwahamishia hapa.

Nilikuwa najua haya mambo yako uswahili tu, kumbe kila sehemu daah, yaani nashukuru ndugu mmoja mstaarabu alikuja kuniambia dogo kwenye hichi chama chetu wengi wanajua umeua mzazi wako kutokana mambo ya ujenzi ulivyoyafanya kwa uharaka na pia wanavyokuona unatembelea pikipiki badala uwe umenunua hata gari?

Daah iliniuma sana na inaendelea kuniuma, tena hata juzi wife kwenye msiba flani mtaani kwetu kuna mdada mmoja alimwambia wife hivyo hivyo. YAANI SASA HIVI HATUNA AMANI NA SEHEMU TUNAYOISHI KWA NAMNA WAPUMBAVU WACHACHE WANAVYOCHUKULIA. Yaani sijui ni dhambi mwalimu kuwa na vijimali au kijana mdogo kuwa na vijimali au akawa na pikipiki badala ya gari kali.

Watu hawajui kuwa nafanya udalali wa viwanja, watu hawajui kama nina duka la nguo mjini, watu hawajui kama ujenzi wa SGR kupitia fidia umeyanyanyua maisha yangu ILA WANACHOJUA JAMAA NI MWALIMU KAUA MZAZI WAKE NDIO KAPATA VIJIMALI HIVI DAAH....,?
 
Pole sana Mkuu, maisha yanachangamoto nyingi sana. Kikubwa hukufanya kama wanavyokusingizia, mshukuru Mungu na songesha maisha yako zaidi.
 
Hongera Mwalimu, kwa nature ya kazi yako na Maendeleo yako kuamini bado Ni vigumu.
 
it will rain, but it can't rain forever.. Changamoto tu hizo za maisha mkuu ... Hawawezi kukusema milele vumilia watanyamaza tu.
 
Polite language ipe thamini ktk maisha yako, usimdharau mtu kama ambavyo wewe hupendi kudharauliwa, uandishi wako unaonesha wewe ni mjivuni kidogo huko mtaani. Huenda hiyo ikawa ndio chanzo cha hayo yote. Kwanini uwaite kenge hao jirani zako??

Kuhusu hayo wanayokuzushia yasikuumize kichwa. Yapuuzie na usimuoneshe mtu kuwa yanakuumiza.
 
Pole Sana na changamoto hiyo lkn.katk haya maisha vitu hivyo vipo pia usipende sikiliza ya walimwengu ..utayasikia mengi Sana hata zaidi ya hayo ...fanya yako Kaka
 
huo ndo uhalisia wa maisha ya dunia, kikubwa nikuangalia maisha yako maana maneno ya wasemaji ukiyapa nafasi utajiumiza bure.

zamani mimi sikua napenda kusikia nasemwa vibaya, na nikisemwa niliumia sana bt kuna rafiki yangu nilimweleza masaibu yangu ndo alinifungua macho, alinambia ishi usemwe kufa usifiwe, akanambia kama hutaki semwa basi kufa bt kama unapenda kuishi kubali kusemwa sana mpaka basi alafu we hujali wala nini....

tangu wakati huo sijawahi shughulishwa na maneno ya wasemaji maana hata ufanyeje huezi epuka labda ufe.
 
Mimi sitaki kabisa tena biashara ya haisii dalala. Kuna trafiki flan alikuwa na dalala nyingi lakini kuna wakati zilifululiza kupata ajali na kuua abiria na kusababisha ulemavu. Watu wakazusha eti kafara na wakati kwenye hizo ajali ni uzembe wa dereva kabisa ulevi na madereva wengine.
 
Pole Sana. Mwaka Jana nilipitia changamoto kubwa ya kumuuguza mtoto wangu nilitumia fedha nyingi Sana ili kulinda afya yake.Mungu ni mwema alipona nikaona ni fursa nzuri ya kuendeleza ujenzi wa nyumba yangu. Bahati haikuwa upande wangu mwezi January tarehe 9 ilinyesha mvua kubwa Sana na kubomoa nyumba za wananchi wengi. Mojawapo ilikuwa nyumba yangu Tena wiki iliyokuwa inafuata nilikuwa naezeka bati. Niliumia Sana baadaye kidogo Kuna mtu tuliwatia fanya biashara fulani akanidhulumu miaka mingi iliyopita ghafla baada ya nyumba kuanguka wiki iliyofuata alinitafuta na kunilipa fedha yangu Kama sehemu ya mtaji na faida ya biashara yetu. Kwa uchungu nilianza kujenga Tena Kwa hasira lakini watu wabaya wakanitengenezea zengwe kuwa huyu kwa kazi yake pesa katoa wapi za nyumba kuanguka na leo ameanza kujenga upya? Nilitengenezewa kesi mbaya ya kupoka fedha za wateje mkononi nashukuru Mungu baada ya ukaguzi wa kina nilishafishwa na maisha yameendelea.Inshallah next week nahamia mjengoni. Ndugu yangu nikutie moyo songa mbele usisikilize maneno ya watu. Jambo la msingi andaa kisu na kuni Mungu atakupa mwanakondoo. ( Kwa kile kidogo ulicho nacho anza na mwombe Mungu atakuonyesha njia Hadi wanadamu washangae,si unaona wewe ulianzia biashara ya mkaa,duka then udalali na leo umebarikiwa . Endelea
 
Back
Top Bottom