Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?
Wakuu natumaini wote mpo salama na mnaendelea vyema kusherekea sikukuu hizi Dah, kwa upande wangu mimi sipo sawa kabisa hapa najiona mkosefu sana na sijui hata jamii itanielewa vipi, nimekuja huku naamini kuna wakubwa na watu wenye busara naweza pata ushauri.. Nayopitia kwa sasa na jinsi...
Kwema wanafamilia....
Maisha haya hayana mapumziko, hasa hasa sisi wanaume, wanakuambia utapumzika ukifa.... Misukosuko nayo ni sehemu ya maisha hata ujitahidi vipi lazima tu Kuna namna flani ivi maisha yatakupa mawazo ya hapa na pale, ila ndo hivo ukiwa hai kupambana ni lazima Wala si hiari.....
Hiki kisa Cha pili hakina hata muda mrefu kilianza tu mwaka huu huu, hii part itakua exclusive Kwa ajili ya Samira tu, kama ulipitia kisa Cha kwanza ni rahisi kuendelea, huyu Binti mawasiliano yake nilikua nayo tulikutana mtandaoni huko.... Kama mjuavyo siku hizi Dunia ni kama Kijiji, ukitulia ukisema umtafute mtu kama mmepotezana hapawi na ugumu Sana kama zamani.... Tuliwasiliana tu Kwa Muda bila kuongea mambo mengi Sana, Sana Sana kujuliana Hali na mambo ya career.... Hakuna vitu personal Sana kama mambo ya familia Wala nini kila mtu alikausha kuhusu hio mada, baadae pakawa hakuna Cha maana Cha kuongelea basi mawasiliano ni kama yakafa japo Kila mtu ana namba za mwenzake, ni mwendo wa kuchunguliana status basi na kukausha, japo mi sio mtu wa status kabisa ndo ivo labda Kwa mwezi mara moja au hivo
Sasa huu mwaka ilikua February sijui, akaanza kunidadisi mambo ya mahusiano yangu, nikamwambia mi nishaoa huku Nina watoto wanne japokua sikumpa Mikasa niliyopitia, basi nikapewa hongera za kinafki na nini maisha yakaendelea, baada ya yapo mawasiliano kama tena yakafa, ikafika mahali ntamtumia sms Whatsapp ata ni blue tick tu Wala hajibu, nikajua tena hapa nilivyomwambia Nina familia na watoto tena wote hao kaona akimbie kabisa, hapo mi Sina hata feelings Wala nini ni kama naona mawasiliano ya kawaida, Wala hatukuwahi kukumbishiana mambo ya mahusiano Wala nini.....
Hali hio imeenda mpaka mwezi wa nne, hapo mimi kazini huku nikapata changamoto flani, kuna project ikawa inafanyika dar nikapangwa hl.... Na ilikua inachukua muda kidogo... Nilitakiwa niwepo huko kama miezi miwili alafu Kuna training ya nje ikawa kama imeungana na ratiba, Kwa hiyo nikimaliza dar natakiwa kwenda training tena, Sasa kukaa mbali na familia nayo ni changamoto kidogo, nikajaribu kuikwepa ila ndo hivo tena nikawa Sina namna
Nyumbani huku Wala Sina changamoto na familia naona Kila kitu kipo sawa tu, mwezi wa nne nikatia Kambi dar tukawa tunakaa hotelini huku mwanza tulitoka wawili tu, uzuri napo huku tunakua busy kiasi Kwa hio at least unaona hata muda unaenda Kwa Kasi, nikawa kama napata shauku nimtafute samira tuonane hata tujuliane Hali na nini ila basi tu nikawa nasita sioni Cha maana Sana baada ya sisi kukutana, siku tu nikamtafuta Whatsapp Wala hakujibu, jioni nikampigia Simu hakupokea Wala hakunitafuta tena...... nikawa nawaza hapa nakosea ukute mtu kashaolewa afu nashindwa kuweka mipaka (kumbuka hapo sijawahi kumuuliza kuhusu mambo yake ya mahusiano)... mpaka siku naona status ilikua birthday yake amepost alikua ameenda vacation nje, akawa amepost yupo na mtu wake japokua alipost sijui tu picha za wakiwa wameshikana mikono, hotel views huko aliko, hakumpost sura kabisa, si unajua tabia za dada zetu sijui kwanini wanakuaga wagumu kupost wenza wao, unaweza ukampeleka mtu vacation ukaambulia kupostiwa mikono Yako tu na caption za mahaba, anyway ndo kama ikawa ivo, na mimi Sasa ile Hali hata ya kumtafuta nikaachana nayo naona maisha yashaendelea Kila mtu anaendelea na maisha yake, waswahili wanakuambia maji yakishakaa chini ya daraja ni kuachana nayo tu
Sasa Kuna siku kama wiki tu imepita akawa kanitafuta Whatsapp, basi kusalimiana na nini, from nowhere, tukajikuta tumechat Sana usiku ule almost usiku kucha, hapo ndo akaanza kunipa lawama nilichomfanyia huko nyuma, akinieleza kuhusu mahusiano yake yaliopita na nini, yaani karibu mambo yote tangu tupotezana na nini, hapo mimi nikampa some details kuhusu maisha yangu ila sio Kila kitu.....
Kwanza akashangaa namwambia nipo dar, hapo tena namwambia Nina muda kidogo..... Okay hio siku ya kwanza mambo niliyonotice kutokana na maongezi yetu
I) hajaolewa Bado, according to her, yupo kwenye relationship ila sio serious Sana ndo sijui wamekubaliana ivo.... Japo nikawa namskiliza tu Wala sikumhoji kuhusu zile status naona ingekua sio sawa Wala nini
ii) she has a very successful carrier, ana biashara zake alinitumia social media platform nizione, na kwa kuangalia tu naona kama maisha ameyapatia Sana, sema pia nikahisi inatokana na backup maana katoka kwenye familia sio Haba Kwa jinsi nilivyonotice kwenye maongezi yetu
iii) hakua na shida ya sisi kuonana ila sio mambo ya mapenzi tena Wala nini, japo hapa nilikua nahisi tukionana kuna feelings tu za kijinga zitakuja ila sikuchukulia maanani Sana
Siku inayofata tukaanza kuongea Sana , nimetoka kazini kapiga tumeongea muda mrefu Sana masaa na masaa.... Baada ya hapo sms utani utani na nini, hapo naanza kuona kama naanza kucatch feelings ila najiambia hakuna bana hayo yashapita.... Siku ya tatu akaniambia kuna mahali anataka weekend anipeleke...... Nikamwambia sawa hakuna shaka.... Dah kumbe kiutani utani balaa ndo linaanzia hapo..... Mpaka Leo hua nawaza labda tu alipanga kulipa kisasi mi sikushtuka mapema Wala nini, maana wanasema mwanamke hua hakubali matokeo Ivi ivi akipata nafasi ya kisasi anaitumia ipasavyo.... Ngoja niandike ya pili, ntaiunganisha hapa hapa ili huu Uzi usiwe mrefu kama ule wa mwanzo.....
NB: ukikutana na makosa ya uandishi potezea, Leo weekend kumbukeni watu tushagawana akili na kampuni za pombe