Za leo ndu wapendwa, mimi nimeolewa na mda wa mwaka na nusu sasa. Hapo nyuma niliwahi kuwa na boyfriend tuliye kaa naye kwa mda wa miaka mitatu hivi. Huyu X-bf alikujakufahamu kuwa niliolewa na akafanya juhudi sana kutafuta no. yangu ya simu mpya. Ss huwa ananipigiaaga na kutunimia messages za mapenzi. Nimemkataza lakini haonyeshi kunielewa kabisa, mpaka sasa nimeamua kukaa kimya ila ndo kama vile amezidisha kutuma sasa. Kwa ajili ya kujiweka in a safe position, nilimwambia hata mume wangu lakini hakusema kitu alibakia kunyamaza tuu. Sasa naombeni msaada katika hili swala maana linanikera sana sana. Nifanye nini?
asante sana kwa ushauri wako, hayo mambo ya design za simu sina uzoefu nao ila kwa sasa natumia sony ericson t280i. May be unipe darasa zaidi.
new samsung models zina uwezo wa ku-delete sms koka kwa yeyote usiyetaka kusoma sms zake na pia ku-end call. Huitaji ku-download software yeyote bali kuweka hiyo namba ya huyo x-bf kwenye reject list za call na sms. Try e200
Lorain kama unamaka ex wako,,,,,,nimeamini wanawake ni weak....yaani mie ndio kama mumeo sijui ningekufanyaje maana uwezo uko juu yako wewe unaonekana unapenda msg za ex wako kuna kitu unaficha hapa.........
kuna kijamaa kimoja kilikuwa kinamsalandia gal wangu knamsumbua sana nikajua gals are weak nikizubaa jamaa gal wangu atamegwa....nilichofanya nilimualika jamaa dinner na gal wangu wakiwa hawajui kinachoendelea kaama nimewalika wote kanza nilikuwa na hasira kali nikamuuliza jamaa kama anampenda gal akasema anampenda nikamuuliza gal je aanmpenda jamaa akakataa....
Nilichofanya nikaona usanii nachezea nikamtwanga talaka pale pale.....
Ndio lilalokuja kwako lorain iweje mko bara tofauti apate namba yako na wewe unamlea lea tu fisadi huyo? nikifikiria haya nataka kubadiili signature yangu niwe nipo nipo milele
Nauthika zaidi na Ex, lakini pia sikufurahia response ya Mr. nilipomshirikisha. Maana nilimwambia aniambie yeye kama mwanaume nifanye nini? akabakia kupandisha mabega tuu. It is true what you have said, may be he did that so that he can have kisingizio of the same.
kITU KAMA NINI NAOMBA UWE HURU KUULIZA, INSTEAD OF ?????
Nilivosema hivo na maana kuwa wewe uko Sweden na huyu jamaa yuko bongo,mimi nimewahi kuishi ulaya na marekani najua upweke ulivyo,nahisi ulianza kuwasiliana na ex wako out of boredom lakini mambo yakaja kuharibika baadae.Inabidi pia ujue kuwa wanawake likitokea jambo wanapenda kuliongelea saa hiyo hiyo lakini sisi wanaume tunapenda kulichekecha akilini kwanza kabla ya kuliongelea na usitegemee jibu kutoka kwa mumeo hapo hapo.Kama mumeo umeshamtaarifu acha kujibu sms's za huyo ex-bf na atachoka na kuacha kutuma.Lorain nimesoma posts zako nyingi unakua muwazi na passionate katika kujadili lakini katika hii naona kuna upungufu.
Thanks for your post, but am in Denmark. When I had asked for the language which i would prefer to know and i mentioned Sweden, it was for my sisters purposes. Just wanted to supprise her if i could get it. Narudia kusema hivi wandugu, nilishakaa kimya sanaaaaa ila the guy is not stopping that is why I came to ask for the advices here.
Mdogo wangu Lorain nitumie jina na namba yake kwenye pm mi niko bongo ntaongea nae kiutu uzima atanielewa.
Siwezi kukupa, ingekuwa vizuri unipe hayo maongezi ya kiutu uzima niongee naye mimi mwenye. U can pm me the message. Thanks for your help Lagatege.
We si umeshaongea nae na imeshindikana? Inabidi apatikane mtu mwingine[sio lazima mimi]aweze kuongea nae 'basically tell him to move on and get a life'
Tak en meget min bror, kama huaelewa nimesema asante sana kakangu. Ujumbe umefika ingawa pia hayo nilishasema sana.
hivi hii issue yako imefikia wapi Mkuu Loraine,
Nilifikiri ulishapata jibu ya huo ex- je bado anasumbua?
Dada Lorain, pole sana. Hilo ni tatizo dogo sana maana anajojaribu kukifanya ni kuingilia nyumba yako na kukudharirisha. Pamoja na kuwa ni sehemu ya gharama unazolipa kwa uhusianao ambao haukuwa sawasawa huko nyuma, ushauri wangu ni kuwa nenda kam-ripoti polisi na kumfungulia kesi ya kukutumia msgs za kukudhalilisha wewe na mumeo.
Chukua hatua haraka
Hii haitakaa sawa ndugu yangu, huwezi kumshitaki mtu aliye ulaya, wala sidhani kama huyu binti kasema kama kazalilishwa yeye na mume wake, na wala hakusema kama huu uhusiano haukuwa sawasawa huko nyuma, ulitakiwa umpe ushauri sio madharau.
Rolain chuja ushauri unaopewa na machache yabebe na yaliyobaki yaache humu humu. Tafuta njia bora ya kudumisha ndoa yako. Huyu x-bf wako asije kukuharibia ndoa yako baadae na yeye akaja na toto la kizungu..... mwambie kama kweli anakupenda akae bali na wewe pamoja na ndoa yako kwa ujumla, badilisha number yako then hide it kwa kuweka private number, wape watu wachache tu ambao unawaamini na sio kila mtu ili uweze kuja kumjua mtu anayegawa number yako ya cm.
pole sana nenda kamshtakiZa leo ndu wapendwa, mimi nimeolewa na mda wa mwaka na nusu sasa. Hapo nyuma niliwahi kuwa na boyfriend tuliye kaa naye kwa mda wa miaka mitatu hivi. Huyu X-bf alikujakufahamu kuwa niliolewa na akafanya juhudi sana kutafuta no. yangu ya simu mpya. Ss huwa ananipigiaaga na kutunimia messages za mapenzi. Nimemkataza lakini haonyeshi kunielewa kabisa, mpaka sasa nimeamua kukaa kimya ila ndo kama vile amezidisha kutuma sasa. Kwa ajili ya kujiweka in a safe position, nilimwambia hata mume wangu lakini hakusema kitu alibakia kunyamaza tuu. Sasa naombeni msaada katika hili swala maana linanikera sana sana. Nifanye nini?