Ushauri wenu wanaJF, mke wangu ana tabia za umbea

Mkuu nimesoma mwanzo mpaka mwisho ingawa kwa tabu sana.

1. Hama kwenu kakae hata chumba kimoja na mkeo.
2. Mpe mimba mpate mtoto.
3. Mkanye mkeo mkiwa wawili usiache wazazi wawasaidie hata ishu ndogo.
4. Mpende mkeo na waheshmu wazazi wako.
5. Narudia hama kwenu na nenda mbali kaanze maisha....
Mkuu kuhama tunahama namke analijua hilo tunanyumba iko mwishoni kuisha vimebaki vitu vidogo vidogo kuikamilisha kama miezi miwili haifiki tutakua tumehamia na wife analifahamu hilo...binafsi mke anabaki na nafasi kama wazazi wanabaki nanafasi yao siegemei kokotote kule zaid nfariji sana mke wangu kipi kinamshindwa kustahamili miezi miwili mapaka kufia kutoa kashfa nzito nzito..na baba yake mzazi mke wangu kuna sku nilimtembelea ktkt kupiga piga story anakanambia jambo ambalo nami nilishalibaini kwa mke wangu kua ana hiyo tabia baba mkwe alinambia hivi naumwa hali yangu nzuri tu nina nafuu ashangaa kawapigia baba zake wadogo wahuko mikoa mingne kuwaambia naumwa sana sitaki kwenda hospitali hili jambo lilinifanya nithibitishe kwa baadhi ya mambo niliokua nayaona kwa mke wangu nahata kumkaya ..ndio maana nkaja huku ktk jukwaa kupata uzoefu zaid kwa walikua ktk ndoa mda mrefu walio ktk mahusiano nahata kwa asie kua na ndoa wote hao busara zao ni muhimu sana
 
Nimeshindwa kusoma uzi wako, ukikua utajifunza uandishi
Sawa mkuu..uandishi sio fani yangu fani yangu ni biashara ndio iko ktk damu uandishi ntaajiri mtu wakuniandikia sio kila kitu lazima nikije watanisaidia wangne wanaojua kwa ujira
 
Sijamaliza kusoma yote lakini jee anayoyasema kwa watu ni yakweli au ni ya uongo? Umbea wake ni wakweli au wakutunga?
Ukishaoa hama na mke wako mkajenge familia yenu ninyi wawili achana na mambo ya ndugu wazazi nk.
Anayoyasema niyaukweli nimeshayafanyia uchunguzi sana tena sana maana hayo mambo tulikua tunajadili watu wandani tu
 
Hapana mkuu kila kitu kiko poa mjengo uko mwishoni kukamilika kama miezi miwili imebaki kuisha kabisa nakuhamia na nawife anajua hilo nashangaa kwanini kawa gafla hivi

Basi hamia kwanza kwako
Then urudi tena
 
Anayoyasema niyaukweli nimeshayafanyia uchunguzi sana tena sana maana hayo mambo tulikua tunajadili watu wandani tu
Kama yana ukweli pengine alikuwa akikushirikisha wewe unaona anaisema vibaya familia yako.
Na si kila mtu ana uwezo wa kukaa na kitu moyoni.
 
Hata Malkia yamemshinda kukaa na watoto wake pamoja na wajukuu
Yaani kuwaweka wanawake nyumba moja ni time bomb
Maneno na kusutana baina ya wakwe na wake zenu hayataisha kama hutaanza kutafuta maskani yako wewe na mke wako
Ila kama ndio mila zenu kukaa na mama itabidi uvumilie tu
Wewe ni mwanaume inabidi upuuzie kabisa mambo haya ya kike kwani sisi tupo tofauti
Kwa ushauri wangu ungetafuta hata kibanda mkajistiri na mke wako na mama mumuache kwake
Kibanda mkuu ninacho kimebaki kama miezi miwili tu kukikamilisha na kuhamia kabisa..ila nlitaka kwa faida tu kupata busara za kuishi na mtu wanamna hii
 
Mbona mmejazana hapo nyumbani kwa wazazi wako?
Acha ujinga kwanza, toka hapo nyumbani, nenda kapange kwako haraka sana...
Hata sijamaliza kusoma habari yako, tatizo hapo ni huo mlundikano.... Baba mkwe, mama mkwe, mdogo mtu na mkewe, wewe na mkeo, sijui nani na nani tena....
Toka hapo upesi sana na mkeo nenda ukapange hata kama itakua ni chumba kimoja na choo cha nje, ndoa yako itakua na amani zaidi, niamini mimi brother!! Fanya hivyo kwanza haraka sana, kabla ya chochote.
malembeka18
Nimeshafanya yote hayo nina nyumba nyangu mkuu iko mwishoni kuisha nahamia kama miezi miwili haifiki kuisha nakuhamia so nyumbani nlikua nakaa kuimarisha ziadi uchumi huku nkijenga
 
Kibanda mkuu ninacho kimebaki kama miezi miwili tu kukikamilisha na kuhamia kabisa..ila nlitaka kwa faida tu kupata busara za kuishi na mtu wanamna hii

Ni wewe ndio uliosababisha yote hayo na umbea na visa havitaisha hapo mpaka uhame tu
Huyo ni mke wako na njia za kumrekebisha zipo nyingi ila la kwanza ondoka hapo
 
Kama yana ukweli pengine alikuwa akikushirikisha wewe unaona anaisema vibaya familia yako.
Na si kila mtu ana uwezo wa kukaa na kitu moyoni.
Hapana wala sikuwahi kumuwazia kuhusu kuwa naona anaisemea vibaya familia yangu ila nlikua naona anakosa hekma..

nakweli kama unavosema sikila mtu mtu anauwezo wakukaa nakitu moyoni nami hilo nimelitambua kwa mke wangu hawezi kukaa na kitu moyoni..ndio maana nimekuja huku kupata busara zakuishi na mtu wa namna hii
 
Huyo anaathiriwa na mazingira

Nenda kaishi mazingira ya peke yenu uone atakavyokuwa mpole
 
Hapana wala sikuwahi kumuwazia kuhusu kuwa naona anaisemea vibaya familia yangu ila nlikua naona anakosa hekma..

nakweli kama unavosema sikila mtu mtu anauwezo wakukaa nakitu moyoni nami hilo nimelitambua kwa mke wangu hawezi kukaa na kitu moyoni..ndio maana nimekuja huku kupata busara zakuishi na mtu wa namna hii
Ushauri ni kwamba.
Mruhusu awe anakwambia wewe kila kitu kibaya kuhusu familia yako. Hivo atayamwaga kwako na hatoyapeleka nje.
 
Siku nyingine jaribu kuweka japo Paragraph ili uweze kusomeka kwa urahisi,nasubiri urekebishe ili nisome mada yako,nimesoma nusu tu nikawa napotea potea!
 
Back
Top Bottom