Ushauri wenu: Ninahitaji Toyota "saloon car" bajeti yangu haizidi Tsh 12m

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Jan 2, 2011
303
154
Wandugu, kama uzi wangu unavyojieleza..Nina kiasi cha Tsh 12 milioni (Bei ya kununulia, kodi ya serikali na gharama zote ziwe ndani ya hiyo Tsh 12m), na ninataka kuagiza gari la kutembelea kutoka Japan.

Je, gari gani ninaweza kulipata kwa bei hiyo hadi ninalishika mkononi. Naomba ushauri wenu pia uzingatie gari ambalo unywaji wake wa mafuta ni nafuu sana

Ushauri wenu ni muhimu sana tafadhali ndugu zangu.

Ninawasilisha kwenu
 
Carina TI ni nzuri hata unywaji wake wa mafuta si mbaya,ukitaka namna ya kuagiza ni PM nikupe maelekezo mkuu ya ushuru na bei ya kununulia kule na usafiri na sbt wako vizuri nimeshawahi kufanya nao biashara
 
Sawa kiongozi. Nitakucheki
 
Habari,

Jana usiku niliona thread yako , lakini nikawa nimetoka online, kurejea sijuiona tena.

Nimeitafuta mno, but sikuiona, nafurahi saa hii nimeiona !!

Mimi ni muingizaji na muuzaji wa magari kutokea japan, U.k na south africa. Hua ninachukulia sokoni moja kwa moja, gari ambazo ni first grade!

Ndio, kwa offer hio ninaweza kukupatia gari, kama upo serious, tuwasiliane pm
 
Kuna kitu sijaielewa kwenye TRA calculator. Sehemu ya customs value CIF. Ni garama ya nini?
 
nenda beforward wapo karibu na ocean road hospital, watakusaidia kila kitu
 
Watake radhi watu,

Sio wote waendao 'pm' ni matapeli.
Sio wote mkuu Nakubali kuwa kuna watu hawapend kutoa michango yao hadharani. Sio vema kwani mchango wao waeza kuwa suluhisho kwa wengine wengi pia.

Sio wote waendao pm ni matapeli ila kwenye mambo ya biashara mara nyingi watu wengi wanatapeliwa PM.

Pm conversions are one against one however when done in the forum become many to many business, discussion, advice, opinions, assistance ....which reduce the chance to client from becoming the victim.

Sent from my L3 using JamiiForums mobile app
 
Habari,

Jana usiku niliona thread yako , lakini nikawa nimetoka online, kurejea sijuiona tena.

Nimeitafuta mno, but sikuiona, nafurahi saa hii nimeiona !!

Mimi ni muingizaji na muuzaji wa magari kutokea japan, U.k na south africa. Hua ninachukulia sokoni moja kwa moja, gari ambazo ni first grade!

Ndio, kwa offer hio ninaweza kukupatia gari, kama upo serious, tuwasiliane pm
Kama kweli unafanya biashara hiyo weka peupe mawasiliano yako ili nasi wengine tukutafute!
 
Sio wote mkuu Nakubali kuwa kuna watu hawapend kutoa michango yao hadharani. Sio vema kwani mchango wao waeza kuwa suluhisho kwa wengine wengi pia.

Sio wote waendao pm ni matapeli ila kwenye mambo ya biashara mara nyingi watu wengi wanatapeliwa PM.

Pm conversions are one against one however when done in the forum become many to many business, discussion, advice, opinions, assistance ....which reduce the chance to client from becoming the victim.

Sent from my L3 using JamiiForums mobile app
Sawa sawa, ninekuelewa aisee!
 
Back
Top Bottom