Crystal clear
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 809
- 339
You will get over it
Huwezi kuyafahamu vizuri mapenzi kama hayajakujeruhi.....Sikuwahi kujua kama mapenzi yanaweza jeruhi kiasi hiki aisee, kiasi cha kuona dunia imesimama. Nilikuwa tu nasikia na kusoma tu kama hadithi. Dah mtu uliyempa Moyo wako kwa dhati kabisa yeye anakuchukulia poa khaaa sijui inawezekanaje jamani.
Hata siamini Mungu tu anipe nguvu niweze muondoa akilini ili nisonge mbele. Maana nampenda sana hadi nashindwa kuelewa sababu tu. Usithubutu kukutwa na hali hii katika maisha yako, ni uzoefu mchungu mno.
Hivi huwa kuna uwezekano kuwa na uhusiano halafu mmoja wenu awe tu malaika asimkosee mwenzie kabisa? Akimkosea mwenzie kosa tu dogo mawasiliano yanakatika? Lakini wakati huo yeye anakukosea sana tu na unamsamehe bila kujali kwa vile tu unampenda?
Kama unajua hauko serious kwanini sasa usababishe shida kwa mwenzio kiasi hiki jamani? Kwanini jamani drama hizi. Sina majibu sahihi nina maumivu makali mno! Njooni mnisaidie nitokeje hapa please.
Mmmh ama kweli kuishi kwingi kuona mengi, nimeamini hata kivuli chako chaweza kukusaliti siku moja. Nimeamua kusema huku labda naweza pata nafuu kwa kutoa nyongo hii ila siyo rahisi kabisa.
Naombeni nasaha zenu
Kwani umeshafika umri wa kustaafu ?Kama ulikuwepo
kwanini waumia kwa mdada na sio mkaka bibieHuwa najisikia uchungu sana mdada akiumizwa na mapenzi, pole sana mkuu cha kufanya jitahidi upunguze mawasiliano nae vitu vinavyokukumbusha kuhusu yeye km inawezekana vichome moto,jione una thamani maana hapo unajiona hufai tyr, ipe nafsi yako thamani na upendo km ukiumia sana ruhusu machozi yatoke,
Nimekuuliza swali hili,bado hujajibu,ni kosa gani ambalo wewe umetenda mpaka jamaa kaamua kuachia ngazi?????Labda tungejua kwanza ni kosa gani wewe ulilotenda mpaka ameshindwa kukusamehe. Tuambie tujue uzito wa kosa lako kulingana na adhabu alokupa
pole sana...u love where u loved...mapenzi ya kweli ni kama kioo...unatakiwa upate unachokitoa ukisema i care basi iwe kwa vitendo n.k...ukiona upo kwenye uhusiano one sided bila basi mapema usisubiri miujiza jiodoe mapema kabla maumivu hayajakupata....kwa sasa tuliza akili kabisa upone majeraha na kujipanga upya kupambana na maisha maana kuumizwa sio mwisho wa maisha yako..hilo ni somo..jitahidi kutomtafuta tena maana hilo litakuchelewesha kupona...yale yote yanayoweza kukumbusha juu yake kaa nayo mbali sana...