Ushauri wenu, nimejeruhiwa sana na mapenzi

lonelygal

JF-Expert Member
Apr 11, 2017
208
166
Sikuwahi kujua kama mapenzi yanaweza jeruhi kiasi hiki aisee, kiasi cha kuona dunia imesimama. Nilikuwa tu nasikia na kusoma tu kama hadithi. Dah mtu uliyempa Moyo wako kwa dhati kabisa yeye anakuchukulia poa khaaa sijui inawezekanaje jamani.

Hata siamini Mungu tu anipe nguvu niweze muondoa akilini ili nisonge mbele. Maana nampenda sana hadi nashindwa kuelewa sababu tu. Usithubutu kukutwa na hali hii katika maisha yako, ni uzoefu mchungu mno.

Hivi huwa kuna uwezekano kuwa na uhusiano halafu mmoja wenu awe tu malaika asimkosee mwenzie kabisa? Akimkosea mwenzie kosa tu dogo mawasiliano yanakatika? Lakini wakati huo yeye anakukosea sana tu na unamsamehe bila kujali kwa vile tu unampenda?

Kama unajua hauko serious kwanini sasa usababishe shida kwa mwenzio kiasi hiki jamani? Kwanini jamani drama hizi. Sina majibu sahihi nina maumivu makali mno! Njooni mnisaidie nitokeje hapa please.

Mmmh ama kweli kuishi kwingi kuona mengi, nimeamini hata kivuli chako chaweza kukusaliti siku moja. Nimeamua kusema huku labda naweza pata nafuu kwa kutoa nyongo hii ila siyo rahisi kabisa.

Naombeni nasaha zenu
 
Hahahahaa....welcome to the world! Zile series za kikorea kwa hapa Bongo hazi-apply kabisa mkuu.

Ila pole sana aise, hii ndiyo dunia yetu. Cha muhumu chukulia poa tu, but next time ukiona mambo hayasomeki wewe anza kujiondoa mapema taratibu taratibu ili maji yakimwagika isiwe pigo sana.

Utasahau tu....endapo ukidhamiria.
 
Huwa najisikia uchungu sana mdada akiumizwa na mapenzi, pole sana mkuu cha kufanya jitahidi upunguze mawasiliano nae vitu vinavyokukumbusha kuhusu yeye km inawezekana vichome moto,jione una thamani maana hapo unajiona hufai tyr, ipe nafsi yako thamani na upendo km ukiumia sana ruhusu machozi yatoke,
 
The good thing is that, you are now making progress kwa sababu bila kupitia hiyo hali huwezi kujifunza. So, move on mkuu. Kuwa busy na ishu zako za maana things will be very fine soon na utampata wako!!
 
Back
Top Bottom