Ushauri wenu: Nilimuahidi, nifanyaje?

Ushauri wenu: Nilimuahidi, nifanyaje?

Isikuhangaishe
Huyo ni mke mtu haihitaji akili ya kiwango cha lami kujua kama kumtimizia mahitaji yake ni kosa au si kosa.
Achana naye tena kuwa na msimamo usije haribu ndoa ya mtu
Mkuu kumbuku aliahidi lakini! Na ahadi ni deni!

Suluhisho ni kumfungulia hiyo saluni mkuu. Labda tu kama kuna vipengele mliwekeana katika makubaliano yenu.

Mfano, kama angeolewa basi usingetekeleza ahadi yako. Ila kama hiyo ahadi haikuwa na masharti yoyote basi wewe fanya kama ulivyoahidi. Ni wajibu wako kwakuwa uliahidi.
 
Eeh ulimuahidi hutamuacha hivihivi... japokua haingii akilini wewe timiza ahadi tena anaimumbushia.. timiza tu mmalizane
 
Kashaolewa tayari huyo...Achana nae...sio ahadi zote ni deni...Fanyia shughuli nyingine za kimaendeleo hiyo pesa ikusaidie
 
Habari zenu wana wa MMU!!! Kwa heshima kubwa, naombeni msaada wa mawazo.

Mimi ni mume wa mtu. Ila kabla sijaoa nilikuwa na mpenzi ambaye nilidumu nae kwa takribani miaka 4, lakini bahati haikuwa yetu, hatukuweza kuoana.

Nilipomueleza kuwa naoa mwanamke mwingine, aliumia sana na alilia sana. Katika kupooza, nilimpa ahadi kuwa sitamuacha hivi hivi. Nikamwambia achague, nimfanyie nini? Yeye akachagua, nimfungulie saluni ya kike, na baada ya kufanya quotation tukabaini kuwa shilingi milioni 2 zingetosha. Mimi kiasi hicho cha pesa, ninakimudu.

UGUMU UNAANZIA HAPA.

Huyu dada (mpenzi wa zamani), alipata mwanaume akaolewa kwa ndoa kabisa. Baada ya ndoa yake, amekuwa akinipigia mara kwa mara, na mara zote anaulizia ahadi yangu kwake (kumfungulia saluni).

Kila nikimueleza kuwa, wewe sasa ni mke wa mtu nitakufunguliaje saluni? Hanielewi. Na amekuwa akinifuata, hadi kazini kwangu.

NIFANYAJE? Ni kweli niliahidi, na nilikuwa na nia hiyo. Ila, kwa sasa ni mke wa mtu. Ni hatari kwa mustakabali wa maisha ya ndoa yake na kwangu pia
Usijaribu wewe ameshakuwa mke wa mtu. We usimfikirie yeye tu, jaribu kufikiri jamaa yake akijua.

Sent from my H8501 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom