Yaani acha tu, alafu wanalaanigi wanawake.Dah miaka 4 yoote alikuwa plan B yako?
Nyie viumbe hamnaga aibu kweli.
Eti!!Hiyo pesa si bora ununue dagaa mle na mkeo.
Utamfungulia saluni wewe kama nan!? Huku mumewe akiwa wap!?.
Acha hizo bro
Ataachana naye vipi wakati anamfuata mpaka ofisini? Bro umesema una uwezo, lipa deni block mawasiliano. Akikufuata tena hapo anataka mengine.Achana nae broo...hiyo ni hatari licha ya kuwa,ulimuahid...kumfungulia saloon kwanza kutaendeleza enzi lenu istoshe ameshaolewa
HahahaEti!!
Halafu faida akale na mumewe
Hivi wewe kama mke wako aliahidiwa huko nyuma na jamaa utakubali huyo jamaa atimize ahadi aliyo muahidi mke wako.Mkuu kumbuku aliahidi lakini! Na ahadi ni deni!
Suluhisho ni kumfungulia hiyo saluni mkuu. Labda tu kama kuna vipengele mliwekeana katika makubaliano yenu.
Mfano, kama angeolewa basi usingetekeleza ahadi yako. Ila kama hiyo ahadi haikuwa na masharti yoyote basi wewe fanya kama ulivyoahidi. Ni wajibu wako kwakuwa uliahidi.
Habari zenu wana wa MMU!!! Kwa heshima kubwa, naombeni msaada wa mawazo.
Mimi ni mume wa mtu. Ila kabla sijaoa nilikuwa na mpenzi ambaye nilidumu nae kwa takribani miaka 4, lakini bahati haikuwa yetu, hatukuweza kuoana.
Nilipomueleza kuwa naoa mwanamke mwingine, aliumia sana na alilia sana. Katika kupooza, nilimpa ahadi kuwa sitamuacha hivi hivi. Nikamwambia achague, nimfanyie nini? Yeye akachagua, nimfungulie saluni ya kike, na baada ya kufanya quotation tukabaini kuwa shilingi milioni 2 zingetosha. Mimi kiasi hicho cha pesa, ninakimudu.
UGUMU UNAANZIA HAPA.
Huyu dada (mpenzi wa zamani), alipata mwanaume akaolewa kwa ndoa kabisa. Baada ya ndoa yake, amekuwa akinipigia mara kwa mara, na mara zote anaulizia ahadi yangu kwake (kumfungulia saluni).
Kila nikimueleza kuwa, wewe sasa ni mke wa mtu nitakufunguliaje saluni? Hanielewi. Na amekuwa akinifuata, hadi kazini kwangu.
NIFANYAJE? Ni kweli niliahidi, na nilikuwa na nia hiyo. Ila, kwa sasa ni mke wa mtu. Ni hatari kwa mustakabali wa maisha ya ndoa yake na kwangu pia
presumption of marriage 2yrs amlipe miaka yote si amempotezea mda? Na kusababisha kuolewa na mwanaume asiempenda?Haikuwa mipango ya Mungu
Kwani amelazimisshwa????presumption of marriage 2yrs amlipe miaka yote si amempotezea mda? Na kusababisha kuolewa na mwanaume asiempenda?
Wewe uoni ameolewa kwa stress?