Habari zenu wana wa MMU!!! Kwa heshima kubwa, naombeni msaada wa mawazo.
Mimi ni mume wa mtu. Ila kabla sijaoa nilikuwa na mpenzi ambaye nilidumu nae kwa takribani miaka 4, lakini bahati haikuwa yetu, hatukuweza kuoana.
Nilipomueleza kuwa naoa mwanamke mwingine, aliumia sana na alilia sana. Katika kupooza, nilimpa ahadi kuwa sitamuacha hivi hivi. Nikamwambia achague, nimfanyie nini? Yeye akachagua, nimfungulie saluni ya kike, na baada ya kufanya quotation tukabaini kuwa shilingi milioni 2 zingetosha. Mimi kiasi hicho cha pesa, ninakimudu.
UGUMU UNAANZIA HAPA.
Huyu dada (mpenzi wa zamani), alipata mwanaume akaolewa kwa ndoa kabisa. Baada ya ndoa yake, amekuwa akinipigia mara kwa mara, na mara zote anaulizia ahadi yangu kwake (kumfungulia saluni).
Kila nikimueleza kuwa, wewe sasa ni mke wa mtu nitakufunguliaje saluni? Hanielewi. Na amekuwa akinifuata, hadi kazini kwangu.
NIFANYAJE? Ni kweli niliahidi, na nilikuwa na nia hiyo. Ila, kwa sasa ni mke wa mtu. Ni hatari kwa mustakabali wa maisha ya ndoa yake na kwangu pia