Habar wakuu, naombeni ushauli wakubwa
Nimechanganyikiwa sana, mimi nina mwanamke wangu mchaga, najua ananipenda sana na huwa ananisaidiaga mambo mbalimbali madogo madogo
Sasa tangu wiki iliyopita analalamika kwamba anadaiwa milioni 2.5 yaan milioni mbili na nusu, kwamba alikopa mwaka jana na alikuwa anatumia na mwanaume wake kabla ya mimi, sasa naona wiki yote hii hana raha.
Na mimi kwasasa sina hiyo hela, akanishawish tuweke gari langu bond mil.3 ili yeye alipe kule baada ya mwezi mmoja analudusha, halafu lile gari tutauza hela nyingine tutafungulia biashara ya baa mimi nikakubali kishingo upande sana
Kila siku naona hana raha, mpaka leo tumetoka tuneenda sehemu tumekula tumekunywa, mara kaanza nisiongee na mtu mara hivi vituko kibao
tukapanda gari tukaondoka njiani vituko mara hivi kugombana akafikia kauli mimi naruka, me nikasema kama mwanamke kweli ruka hapo nipo speed 40 ghafla nikaona mtu kafungua mlango wa gari karuka kweli, nikasikia yowe moja tuuuh
me kiukweli sikusimama kabisa maaana nilipata hasira mpaka nikafika home, mpaka sasa sijui hali yake maana sasa 6 usiku ndo imetokea tena karuka kwenye lami
Maswali :
Najiuliza huyu mwanamke Ana strees zake za madeni anataka kunipa kesi ya mauaji au ndo wivu ?
Hata kama wivu mbona tunagombanaga sana haijawahi tokea hii
Ushauri wenu ndugu zangu