Ushauri wangu kwa watu wanaotafuta wachumba mitandaoni

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
724
551
Nianze kwa kusema kuwa si lengo langu kukatisha tamaa watu ila ninashauri tu hasa kulingana na kilichonipata.

Mimi niliwahi kupata mchumba kupitia mitandao ya kijamii. Baada ya kuchat kwa takribani mwaka mmoja nikajiridhisha kuwa ninampenda. Tukapanga kuonana. Ajabu baada ya kuonana nikagundua kuwa alikuwa tofauti sana na jinsi alivyokuwa amenieleza na kujifafanua hata kwenye picha!

Zaidi ya yote alikuwa muongo. Akidai hana watoto na kumbe alikuwa nao.
KIMSINGI KAMA KWELI UMEMPENDA MTU JITAHIDI MUONANE USO KWA USO. MAANA NI AFADHALI MTU UNAYEMFAHAMU KULIKO UNAYEMDHANIA!!! MIMI WANGU HATUKUENDELEA KWANI BAADA YA KUFIKA KWAKE NILIKUTANA NA HALI AMBAZO NISINGEWEZA KUVUMILIANA NAZO!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom