Kwa mambo mazuri na makubwa uliyoyafanya huko 'Isles' uliko kama Rais wao na 'Mikakati' kabambe ya Maendeleo kuelekea kuifanya Zanzibar kuwa Dubai ya Afrika Mashariki kama GENTAMYCINE nakushauri acha kuwa na nia ya kuja kuwa Rais wa 'Mainland' kwa ama 2025 au 2030 tafadhali.
Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi bakia tu huko huko Zanzibar (Isles) ili nawe utengeneze Historia yako ambayo itakufanya uje Ukumbukwe Vizazi na Vizazi hadi kukufanya uje kuitwa Baba wa Zanzibar ya Maendeleo na Mabadiliko tofauti na Waliokutangulia ambao Wengi walijikita zaidi katika Siasa, Chuki na Ubaguzi wa Unguja na Pemba.
Unakubalika na Wazanzibari Wote kwa aina ya Uongozi wako na Siasa uifanyayo huko hivyo wala usije huku Bara (Mainland) ambako najua kwa jinsi tulivyo na Nongwa na Visununu 'vilivyotukuka' tunaweza hata kukufanya uikimbie Ikulu na ukapumzike zako tu Masaki katika Nyumba aishiyo sasa Baba yako.
Ufanyie Kazi huu Ushauri na ukubali tu.