Ushauri wangu kwa Mh Dk. Kigwangalla

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
Habari za leo Watanzania wenzangu wote ambao mtatumia muda wenu mfupi sana kusoma maoni yangu haya ya kumsaidia MH Hamis Kigwangala Waziri wa Mali Asili na Utalii (mzee wa field).

Mapema jana nikiwa ninapitia magazeti nilikutana na gazeti la Jamhuri lenye kichwa cha habari kilichoandikwa kwa wino mweusi kikisema CAG AMCHUNGUZA DK. KIGWANGALLA. Nilianza kusoma undani wa habari nikakutana na tuhuma nzito zinazoelekezwa kwa Mh Waziri. Ninasema tuhuma nzito kwa kuwa tangu nimfahamu Mh Kigwangalla nilimuweka kwenye kundi la vijana Wazalendo, hodari, shupavu na shujaa katika kazi zao. Nilianza kumfuatilia Kigwangalla tangu enzi za mgomo wa madakitari mpaka anakuwa Mbunge baada ya MH Bashe aliyeshinda kura za maoni kutoteuliwa na vikao vikuu vya CCM.

Tuhuma za kiuchunguzi zinazoelekezwa kwa Mh Kigwangalla na gazeti la Jamhuri ni za matumizi mabaya ya fedha za Wizara ambapo msingi wa tuhuma ni matumizi mabaya ya ofisi ya Umma. Nilipata hamu na ari ya kusoma makala ndefu ya Jamhuri hasa nikiwa ninakumbuka kalipio kali alilolitoa Mh Rais akiwa likizo mkoani Geita kuwa anampa Waziri na Katibu wake siku tano wawe wanasalimiana. Hivyo kalipio la Rais lilinipa hamu ya kusoma vizuri gazeti ili kupata walau kiini cha Rais kuwapa ushauri wawili hao.

Jamhuri linaonyesha Mh Kigwalla amekuwa anatumia fedha nyingi za wizara bila utaratibu maalumu kwa maelezo kuwa anatangaza vivutio vya utalli. Jamhuri linamtuhumu kuwa amekuwa anawabeba wasanii na kuzunguka nao kama sehemu ya kutangaza vivutio ili hali anaandaa mazingira ya uchaguzi wa 2025, Jamhuri inatanabaisha undani wa hili.Jamhuri linasema kuna kipindi ameshawahi kumtumia mwandishi ndege kutoka Arusha kwenda Dar ambapo ndege hiyo ilikaa uwanjani kwa zaidi ya saa nane ikimsubiria mwandishi huyo.

Baada ya kusoma gazeti jana asubuhi jioni nikiwa nimetulia nyumbani nilianza kuona Mh Kigwangalla ameanza kushutumu gazeti kwenye akaunti zake za twitter na instagram. Majibu/Shutuma za Dk. Kigwangalla zikanifanya nitumie muda wangu huu kumushauri mambo kadhaa. Ushauri hautaenda kwa Mh Hamis Kigwangalla(mb), bali kwa MH Kigwangalla Waziri.

Waziri Kigwangalla katika kuonyesha kujaribu kujibu tuhuma zake ambazo kwa mjibu wa Gazeti la Jamhuri si tuhuma bali nituhuma zilizo kwenye uchunguzi amepaniki. Majibu ya Mh Kigwangalla si majibu sahihi kwa tuhuma nzito kama zile. Majibu yakeyanaongeza kesi nyingine ya Jamhuri. Mh Kigwangalla amesema anaingia vitani bila kujali anaenda kupigana na nani. Amesema hatachagua silaha ya kwenda nayo vitani na amesema asiye mjua afuatilie historia yake. Sina mashaka na majibu haya ya Dk. Kigwangalla, nimepata hofu aliposema hawa watesi wake wa sasa walishataka kupambana na Waziri aliyepita. Inasemekana waziri aliyepita aliona isiwe taabu akaamua kutoa fedha nyingi kwa watesi hawa wa Kigwangalla. Ninadhani hii ni hatua ya kwanza ambayo Kigwangalla anapaswa kuvisaidia vyombo vya usalama kujua kiasi gani waziri alitoa? Alitoa kwa na nani na kwa sababu gani? Kwa nini aziri alihonga? Ni mhujumu uchumi? Ninadhani Mh Kigwangalla hapa ndipo anaweza kulisaidia taifa kupona maana kama Waziri anaweza kuhonga, je vita ya uujumu uchumi Mh JPM nani wa kumusaidia? ‘’ Kuna jamaa wa gazeti fulani wanaotumiwa na watesi wangu, waliwahi kumuandama Waziri fulani wa Maliasili na Utalii huko siku za nyuma mpaka akawapa hela ndiyo wakaacha, wakaanza kumsifia. Mimi siyo mtu wa aina hiyo! #HK’’

Kuonyesha kuwa hili kundi ni hatari, Mh Kigwangalla analalamika walijaribu kutaka kumfanyia mbaya wakashindwa. Lakini ninajiuliza kwa nini Mh alisubiria hadi leo? Kuna mahali aliripoti wakashindwa kuwakamata? Hawa watu wananguvu kiasi gani, wana nguvukama za Samsoni tunaemsoma kwenye Biblia? Ona Mh Kigwangalla alichoandika kwenye twitter yake jana “Waliwahi kupanga mbinu za kunidhuru, pengine kuniua Mungu akanisalimisha, walishindwa kuniua, hawatoniangusha leo, naingia vitani kwa silaha zote, usiombe kunifikisha hapa, Mimi hupigana vita bila kujali nani atadhurika, alietaka vita ameipata”

Lakini wakati Mh Kigwangalla akijibu haya mapigo jana leo Jamhuri limeibuka na mkazo wa stori yake ya jana huku likiwa limemhoji Tale na Nyerere. Tale anaonyesha kukubaliana na hoja ya Jamhuri na kulalamka kuwa walitumia fedha zao huku Nyerere akisema ni haki kwa kuwa wanatangaza vivutio.

Ushauri wangu wa mwisho kwa Mh waziri, Kwanza nikubaliane naye kuwa wizara hii inachangamoto kubwa. Inawezekekana changamoto tunaileta wenyewe kutokana na mambo yaliyopo huko. Lakini kujenga hoja kuwa umekuza utalli haifanyi kuhalalisha tuhuma zinazokuja kwako. Kukuza utalii kwa kutumia fedha bila utaratibu maalumu ni uhujumu uchumi kama kweli tuhuma ziko sahihi.

Jambo la pili, Wewe ni waziri na miiko ya uwaziri unaijua vizuri. Kitendo cha kujibu tuhuma mtandaoni, tena tuhuma nzito ni kutoithamini nafasi uliyonayo. Na umesema unaenda kupigana ijapo hujasema vita yako itakuwa na sura ya Uwaziri au ya u Kigwangalla? Ninadhani njia nzuri ili uweze kupigana vizuri na damu au risasi zisije zikawagusa watumishi wengine wa serikali kwa nia njema ungejiuzulu ili kuruhusu uwanja sawa wa mapigano. Kujiuzulu si fedhehe bali ni ushujaa kwa mtu mzalendo kuonyesha kukerwa na yanayomchafua. Ninaamini ukijiuzulu utajipa nafasi ya kujitathimini na kuangalia kesho yako. Mzee Mwinyi alishawahi kujiuzulu na akapata Urais, hivyo kuachia nafasi kunakupa legality machoni kwa watu na inamuondolea Rais kila mara kufkiria namna ya kutumbua. Rais alishasema kutumbua ni moja ya kazi ngumu, tumsaidie wakati mwingine kwa kujiondoa.

Mwisho kabisa mwalimu kwenye kitabu chake cha TUJISAHIHISHE aliwahi kuandika kuwa unapokuwa kiongozi ukiona unasemwa semwa bila kujali tuhuma ni za kweli au si za kweli unapaswa kuwajibika ili kuonyesha uzalendo.
 
Mimi namuunga mkono Kigwangala , Gazeti la JAMHURI linamchafua sana, Manyerere Jacton anatumika na mafisadi walioko wizara ya utalii na maliasili kumchafua , hili gazeti linajulikana kwa kazi hiyo.
 
Nimeona twitter pascal mayalla kamsharii kama gazeti lenyewe ni jamhuri ni bora ajibu tuhuma, hata kama wanatumiwa ila kuna 90% ya ukweli, jamaa wanaandika habari za uchunguzi kweli kweli wana uhakika na walichokiandika ataomba poo mwenyewe...

Chombo cha habarii kisichoogopa wenye mamlaka(yeye waziri) na mawaziri wenzake wapo kimyaa, awe makini ataliwa kichwa kutafuta au kutaka kumshirikisha kwa ajili ya kuonewa huruma na raisi kwenye hili haitamsaidia

Kwa post hii hapa ninaamini kabisa kigwangwala hana imani tena na anajua exactly alichokifanya
Screenshot_20200122-114915_Instagram.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
... nchi ya majungu hii; kuanzia mkubwa hadi mdogo ni majungu professionals!
 
Nimeona twitter pascal mayalla kamsharii kama gazeti lenyewe ni jamhuri ni bora ajibu tuhuma, hata kama wanatumiwa ila kuna 90% ya ukweli, jamaa wanaandika habari za uchunguzi kweli kweli wana uhakika na walichokiandika ataomba poo mwenyewe...

Chombo cha habarii kisichoogopa wenye mamlaka(yeye waziri) na mawaziri wenzake wapo kimyaa, awe makini ataliwa kichwa kutafuta au kutaka kumshirikisha kwa ajili ya kuonewa huruma na raisi kwenye hili haitamsaidia

Kwa post hii hapa ninaamini kabisa kigwangwala hana imani tena na anajua exactly alichokifanyaView attachment 1330527

Sent using Jamii Forums mobile app
Walishirikiana na Twiga kutaka kumuua
 
Kigwangala bado mtoto sana, hapo amevuliwa nguo amebaki uchi, hajui afanye nini, mwambieni kuwa ukivuliwa nguo mbele za watu chuchumaa chini halafu omba watu wakuletee nguo, usikimbizane nao
 
Nimeona twitter pascal mayalla kamsharii kama gazeti lenyewe ni jamhuri ni bora ajibu tuhuma, hata kama wanatumiwa ila kuna 90% ya ukweli, jamaa wanaandika habari za uchunguzi kweli kweli wana uhakika na walichokiandika ataomba poo mwenyewe...

Chombo cha habarii kisichoogopa wenye mamlaka(yeye waziri) na mawaziri wenzake wapo kimyaa, awe makini ataliwa kichwa kutafuta au kutaka kumshirikisha kwa ajili ya kuonewa huruma na raisi kwenye hili haitamsaidia

Kwa post hii hapa ninaamini kabisa kigwangwala hana imani tena na anajua exactly alichokifanyaView attachment 1330527

Sent using Jamii Forums mobile app
Analialia nini sasa, si aje nje ya Box tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Why revealing all this now? Na kwanini hajiuzulu. Something is cooking huenda anajua au ana wasiwasi he will soon be out. Maoni yangu naona hajakoma a kisiasa. Watu wa aina hii wangesalia tu kwenye taaluma zao wangeuwa more productive to society...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom