Ushauri wangu kwa Magereza, Chadema na Viongozi wake

Nadhani CHADEMA wanastahili lawama zaidi kuliko Jeshi la Magereza, sehemu zote za Majeshi ya ulinzi na usalama zina taratibu zake, na unaonywa kabisa madhara utakayokumbana nayo pindi utapovunja taratibu hizo.

Askari hafikiri kama raia na wala hatendi kama raia,ikumbukwe pia huyu askari anamafunzo na kakabidhiwa silaha za namna ya kudhibiti vurugu, juu ya yote yeye ni mtu anayesimamia sheria kutendeka.

CHADEMA wanamdudu wa kupenda kupigwa na vyombo vya dola, labda hili ndio SUM ya sera za chama chao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upuuzi mtupu polepole yeye si aliingia mpaka ndani wakati umefika hatuogopi chochote.#Tume huru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naona ni kama vile askari wa Tanzania wanapewa mafunzo ya kutumia maguvu na ukatili zaidi kuliko hekima na busara. Nina waogopa sana hawana muda wa kutumia akili. Ni vizuri wananchi kyjitenga na kukaa mbali nao kwa usalama wa maisha yao. Roho nyingi zimepotea na wengi kujeruhiwa kwasababu ya matendo yao ya kikatili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani CHADEMA wanastahili lawama zaidi kuliko Jeshi la Magereza, sehemu zote za Majeshi ya ulinzi na usalama zina taratibu zake, na unaonywa kabisa madhara utakayokumbana nayo pindi utapovunja taratibu hizo.

Askari hafikiri kama raia na wala hatendi kama raia,ikumbukwe pia huyu askari anamafunzo na kakabidhiwa silaha za namna ya kudhibiti vurugu, juu ya yote yeye ni mtu anayesimamia sheria kutendeka.

CHADEMA wanamdudu wa kupenda kupigwa na vyombo vya dola, labda hili ndio SUM ya sera za chama chao.

Sent using Jamii Forums mobile app
"Askari hafikirii kama raia wala hatendi kama raia"

Mambo kama haya yanapatikana tu kwenye hizi nchi za kimaskini.

Huu ni umaskini wa akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM IMEKUWA TABU JAMANI HUYU MKOLONI SIJUI TUNAMUONDOAJE. WATANZANIA TUMPE TALAKA HUYU CCM
Ni kulipa kisasi tu October Bila hivo hali itakuwa mbaya sana kuanzia mwakani njaa itazidi,ajira nyingi zitakufa,wasiojulikana watarudi Kwa kasi ya 4G,ufukara utaongezeka sana,kodi zitapindishwa biashara zitakufa.Tukimuondoa mkoloni Furaha yetu itarejea ajira zitaongezeka sababu waliokimbiza nje mitaji yao kukwepa kuishi kishetani watairudisha ajira zitaongezeka, wasiojulikana hawatokuwepo,ndoa zitaimarika sababu Pesa zitakuwapo

Tujitahidi tuondoe hii korona tusikosee tena,kila aliyeumizwa alipe kisasi October
 
Taratibu haziwezi kubadilika kwa kuangalia sura za watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona zilibadilika kwa ajili ya wakina Polepole? Hapa wa kulaumiwa ni Magereza peke yao. Kwani wakina Bulaya walionyesha nia ya kuwadhuru askari wa Magereza? Au kuvunja milango ya Magereza ili waingie kuwafungulia wafungwa waliokuwemo? Hii false equivalency ni hatari sana. Raia wanapoonewa ni wajibu wetu ku unequivocally kuwasema wanapofanya hivyo. Na wajibu huo ni mkubwa zaidi kwa wale wanao wasimamia. Kuna ugumu sana kwa uongozi wa Magereza au serikali kusema kuwa hawakustahili kupigwa vile na kuwachukulia hatua waliofanya hivyo?

Amandla....
 
Akienda Humphrey Polepole anaingia ndani ya Uzio wa Gereza na Msafara wa Magari, Akiambatana na kundi la Waandishi wa habari pamoja na Wapiga Picha.

Ila Wakienda CHADEMA unawashauri Wangekaa hata Umbali wa Kilomita Moja Toka Gerezani.

Hizo Sheria, Utulivu na Unyeti wa Eneo mbona unabagua?

Acheni Double Standard ni Upumbavu uliokithiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sidhani kama Polepole alienda na kundi kubwa la watu namakelele na kugonga geti kwa lazima.
Sidhani Kama polepole anaweza kuyafanya hayo Lazima aliomba kuingia na akaruhusiwa kuingia Kama Polepole alikataliwa na akaingia kwalazima na hakupewa kipigo basi kuna shida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zikufurahishe wewe kama nani?

Taratibu za magereza sio kama kuuza ramba ramba, zimfurahishe kila mtu.
 
Sio kweli; hata huko Segerea wameenda kumpokea Mbowe kwa sababu ya matokeo ya kesi ya uongo iliyotengenezwa, Chadema kwenda kudai kiapo ilikuwa haki yao, hawakufanya vurugu, vurugu walianzisha polisi na mabomu yao ya machozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe umeleta UZI ukiwa biased na umekuwa na majibu yako mfukoni, ulitakiwa kufanya tafiti ya kutosha sio unakuja na maelezo ya pande moja.

Naomba unijibu au unitajie siku yoyote CDM walikubali kutendewa haki? Unataka kusema always wao wanatendewa ndivyo sivyo?
 
Hakuna anayefurahia hao watu kupigwa, ni jukumu lao kulinda usalama wao, hakuna haja ya kushindana na kina Polepole kwenye viwanja vya magereza, hao wote tunajua wanabebwa na vyombo vya usalama na wao wamekiri, sasa viongozi wa Chadema hawawezi kushindana na marungu ya polisi na askari magereza, wataumizwa tu, wao wamezoea kushindana kwa hoja uraiani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi!! Maadamu viongozi wa CDM wanafahamu fika hawana uhusiano mzuri na vyombo vya dola basi wawe makini.

Wasijilinganishe na wenzao wa Ccm wanaobebwa na kupendelewa kupitiliza pia si lazima kila mara washindane nao maana wataishia kuumia tu.
 
Wise words
Wakuu Salaam.

Nikiri wazi, nimelazimika kuandika huu uzi baada ya mabishano makali kati ya roho yangu na kichwa changu; roho ikiniambia usiandike, na kichwa kikinilizamisha kuandika, hatimaye nimeamua kukipa kichwa ushindi hivyo kuamua kuandika.

Taarifa za viongozi wa Chadema kupigwa jana wakati walipokwenda kumchukua kiongozi wa chama Mh. Freeman Mbowe baada ya yeye kukamilisha taratibu za kulipiwa faini hazijanifurahisha, bado sijajua ni kwanini askari magereza waliamua kuwa "too harsh" kiasi cha kuwasababishia maumivu na majeraha katika miili yao.

Inaripotiwa kwamba, baada ya viongozi wa Chadema kufika maeneo ya gereza palitokea mabishano kati yao na askari magereza yaliyosababisha askari aliekuwa zamu kupiga filimbi ya kuashiria hali ya hatari, iliyosababisha askari wengine kufika eneo la hatari ili kuongeza nguvu kwa mwenzao, hili lilisababisha baadhi ya viongozi wa Chadema kupigwa na kuumizwa, ambapo sasa inaripotiwa wapo kituo cha polisi Stakishari.

Nikiri wazi, bado nasisitiza nguvu iliyotumika kuwatawanya viongozi wa Chadema na wapenzi wao ilikuwa kubwa kupitiliza, hasa ukizingatia waliotuhumiwa kufanya vurugu hawakuwa na silaha yoyote ambayo ingesababisha kuhatarisha hali ya amani kwa kiwango kikubwa, hivyo askari magereza walichokifanya hakika hakijampendeza mpenda haki yeyote, wapunguze matumizi ya nguvu kupitiliza.

Lakini pia nalazimika kuwashauri viongozi wa Chadema wawe makini hasa wanapofika maeneo nyeti kiusalama nchini, hasa wanapokwenda kuwachukua au kuwatembelea viongozi wao, gerezani in particular.

Sote tunafahamu unyeti wa maeneo ya magereza nchini, yanahitaji ulinzi na utulivu wa uhakika kwa muda wote wa masaa ishirini na nne kwa siku (24 hours a day). Hivyo nakuwa mgumu kuamini kwamba viongozi wa Chadema walipigwa tu punde baada ya kufika Segerea pasipo kupewa maelekezo yoyote ambayo naamini kwa namna moja au nyingine walikuwa wagumu kuyafuata, hali iliyosababisha wao kupatwa na majanga yaliyowafika.

Naamini kwamba, kama wangeonesha ushirikiano toka mwanzo kwa kutii maagizo na maelekezo waliyopewa, hali hii isingefikia hapa ilipofika ambapo tunaambiwa Mh. Esther Bulaya alipigwa mpaka kuzimia.

Hili lililowapata linasononesha mioyo ya wazazi, ndugu, jamaa, na marafiki wote wa viongozi wa Chadema nchini, hakuna anayependa kuona wakifikwa na madhila kama hayo yaliyowapata hapo jana, hivyo ni vyema kwa mtazamo wangu, viongozi wa Chadema wao binafsi, wawe wa kwanza kuchukua tahadhari kulinda usalama wao, badala ya kuacha kila jambo litokee bila kujali athari za kile kitachoweza kuwapata baadae.

Bado ninaamini, walikuwa na uwezo wa kumpokea Mbowe popote hata kilomita moja mbali na gereza, kwasababu kwanza alishaachiwa, pili nae alikuwa anaelekea maeneo ya makao makuu ya chama, hivyo kumuona Mbowe hiyo jana kwao ilikuwa ni lazima, bila kuathiri utulivu wa eneo la gereza kwa namna yoyote.

Ni vyema kila mtu achukue tahadhari kwa upande wake, kila mmoja popote alipo ajue anawajibika kulinda usalama wa mwingine bila kusababisha maumivu kwa yeyote.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani CHADEMA wanastahili lawama zaidi kuliko Jeshi la Magereza, sehemu zote za Majeshi ya ulinzi na usalama zina taratibu zake, na unaonywa kabisa madhara utakayokumbana nayo pindi utapovunja taratibu hizo.

Askari hafikiri kama raia na wala hatendi kama raia,ikumbukwe pia huyu askari anamafunzo na kakabidhiwa silaha za namna ya kudhibiti vurugu, juu ya yote yeye ni mtu anayesimamia sheria kutendeka.

CHADEMA wanamdudu wa kupenda kupigwa na vyombo vya dola, labda hili ndio SUM ya sera za chama chao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni mpuuzi na upuuzwe. Wakienda wa Ccm mpaka na macamera ndani. Hao hawahatarishi amani. Wakienda wa Cdm hao wanahatarisha amani ?!. Ujinga gani huo !!

Nchi haziendeshwi hivyo. Kuiga mambo ya Rwanda hakutaisaidia nchi yetu kuwa nzuri na ya mfano. Na awamu hii itaacha aibu kwa taifa badala ya mafanikio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati wewe filimbo ilivyopigwa ulitoka nduki balaa
Haki Na Uhuru ni vitu vinavyotakiwa Kudaiwa kwa kila hali hata ikibidi kugharimu Uhai, HAKI HAIOMBWI.

Kuendelea kuwachekea na kuwabembeleza hawa Wapuuzi ni kuwapa uhuru wa kufanya wayafanyayo.

Acha Waendelee kutesa, Kuteka, Kupiga na Kupoteza yoyote wanayeona wanamhitaji lakini tunahesabu, na tunashukuru Kwamba Familia zao zipo huku huku Mitaani na Wao Tunakutana nao katika Bar Hizi hizi za Mitaani kwetu.

Muda utafika nasi tutachora mstari.

Hujapigwa ukazimia kama Esther Bulaya ndo maana umeweza kuandika ujinga huu.

Hujavunjwa mkono kama Mdee ndo maana unajipa moyo usiokuwa nao. Yaliyowakuta ukiwauliza leo watakupa story tofauti.

Zingatia ushauri wa Mtoa Mada utapona na utaheshimika.

Lisu kawadanganya mkachezee majeshi kwa faida ya ukimbizi wa kisiasa. Kuchezea majeshi hata Mabeberu hawatawaunga mkono!!
 
Wewe ni mpuuzi na upuuzwe. Wakienda wa Ccm mpaka na macamera ndani. Hao hawahatarishi amani. Wakienda wa Cdm hao wanahatarisha amani ?!. Ujinga gani huo !!

Nchi haziendeshwi hivyo. Kuiga mambo ya Rwanda hakutaisaidia nchi yetu kuwa nzuri na ya mfano. Na awamu hii itaacha aibu kwa taifa badala ya mafanikio

Sent using Jamii Forums mobile app
Bwashee, hii ni Serikali ya CCM, siyo ya CHADEMA!! Mwenye uwezo wa kuchungulia na kufuatilia kazi ya Serikali ni CCM.

Siku CDM ikishika dola utakuwa ni wakati wake nayo kuingia popote. Kwa sasa fuateni utaratibu.
 
Wanaweza kubambikiziwa tu makosa na usisahau ilikuwa inafahamika kuwa wataenda kumpokea Mbowe wakati anatoka Magereza.

Pia,tambua kuwa mpaka sasa tumesikia tu kutoka upande mmoja(upande wa Magereza ambao ndio watuhumiwa) hivyo tusubiri pia kusikia kutoka kwa viongozi wa CHADEMA(wahanga) kabla ya kuhukumu yoyote.
Unawezaje kuwatuhumu magereza kwa kutekeleza wajibu wa kisheria kutunza gereza. CDM wakue waache utoto ktk issue za msingi wanapodai haki zao wakumbuke pia wajibu wao ktk sheria za nchi.

Hivi wabunge hao akina Mdee na Bulaya unataka kusema hawajui ni kwa nn maeneo ya magereza yametengwa mbali na makazi ya wananchi?

Hawajui kwa nn Jeshi la magereza lilianzishwa na kupewa vitendea kazi?

Natamani kuona siku moja wanapata ridhaa ya wananchi kutuongoza na wakiachia kila kitu kisela. Kama kutakuwa na nchi hapo. Ni viongozi vijana lkn malimbukeni wanaokosa busara. Wabadilke wataendelea kuumia.

Zaidi zaidi nmefurahi kuona leo utoto wao wameenda kufanyia taasis ingine na ime wawajibisha accordingly maana ingekuwa polisi ingeonekana ni chuki ya polisi kwa CDM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haki Na Uhuru ni vitu vinavyotakiwa Kudaiwa kwa kila hali hata ikibidi kugharimu Uhai, HAKI HAIOMBWI.

Kuendelea kuwachekea na kuwabembeleza hawa Wapuuzi ni kuwapa uhuru wa kufanya wayafanyayo.

Acha Waendelee kutesa, Kuteka, Kupiga na Kupoteza yoyote wanayeona wanamhitaji lakini tunahesabu, na tunashukuru Kwamba Familia zao zipo huku huku Mitaani na Wao Tunakutana nao katika Bar Hizi hizi za Mitaani kwetu.

Muda utafika nasi tutachora mstari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unadai haki magereza?
Kule kuna haki ya wafungwa au mahabusu!
Nadhani kipigo ilikuwa halali kwenu
 
Unayosema ni sahihi kabisa. Tatizo ni kwamba kuna uonevu mkubwa wanafanyiwa CHADEMA, kiasi kwamba tunashindwa hata kujua wapi kilistahili nini. La pili nafikiri watesi watakuwa walitoa maelekezo hayo, baada ya kuona kuwafunga imefeli. Hakuna mazingira yanayoweza kupelekea mbunge kupigwa mpaka kuvunjwa. Amini amini nakwambia muda si mrefu huyo askari atapandishwa cheo.

Back
Top Bottom