Ushauri wangu kwa Magereza, Chadema na Viongozi wake

Ushauri wangu kwa Magereza, Chadema na Viongozi wake

jd41

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Posts
3,756
Reaction score
4,849
Wakuu Salaam.

Nikiri wazi, nimelazimika kuandika huu uzi baada ya mabishano makali kati ya roho yangu na kichwa changu; roho ikiniambia usiandike, na kichwa kikinilizamisha kuandika, hatimaye nimeamua kukipa kichwa ushindi hivyo kuamua kuandika.

Taarifa za viongozi wa Chadema kupigwa jana wakati walipokwenda kumchukua kiongozi wa chama Mh. Freeman Mbowe baada ya yeye kukamilisha taratibu za kulipiwa faini hazijanifurahisha, bado sijajua ni kwanini askari magereza waliamua kuwa "too harsh" kiasi cha kuwasababishia maumivu na majeraha katika miili yao.

Inaripotiwa kwamba, baada ya viongozi wa Chadema kufika maeneo ya gereza palitokea mabishano kati yao na askari magereza yaliyosababisha askari aliekuwa zamu kupiga filimbi ya kuashiria hali ya hatari, iliyosababisha askari wengine kufika eneo la hatari ili kuongeza nguvu kwa mwenzao, hili lilisababisha baadhi ya viongozi wa Chadema kupigwa na kuumizwa, ambapo sasa inaripotiwa wapo kituo cha polisi Stakishari.

Nikiri wazi, bado nasisitiza nguvu iliyotumika kuwatawanya viongozi wa Chadema na wapenzi wao ilikuwa kubwa kupitiliza, hasa ukizingatia waliotuhumiwa kufanya vurugu hawakuwa na silaha yoyote ambayo ingesababisha kuhatarisha hali ya amani kwa kiwango kikubwa, hivyo askari magereza walichokifanya hakika hakijampendeza mpenda haki yeyote, wapunguze matumizi ya nguvu kupitiliza.

Lakini pia nalazimika kuwashauri viongozi wa Chadema wawe makini hasa wanapofika maeneo nyeti kiusalama nchini, hasa wanapokwenda kuwachukua au kuwatembelea viongozi wao, gerezani in particular.

Sote tunafahamu unyeti wa maeneo ya magereza nchini, yanahitaji ulinzi na utulivu wa uhakika kwa muda wote wa masaa ishirini na nne kwa siku (24 hours a day). Hivyo nakuwa mgumu kuamini kwamba viongozi wa Chadema walipigwa tu punde baada ya kufika Segerea pasipo kupewa maelekezo yoyote ambayo naamini kwa namna moja au nyingine walikuwa wagumu kuyafuata, hali iliyosababisha wao kupatwa na majanga yaliyowafika.

Naamini kwamba, kama wangeonesha ushirikiano toka mwanzo kwa kutii maagizo na maelekezo waliyopewa, hali hii isingefikia hapa ilipofika ambapo tunaambiwa Mh. Esther Bulaya alipigwa mpaka kuzimia.

Hili lililowapata linasononesha mioyo ya wazazi, ndugu, jamaa, na marafiki wote wa viongozi wa Chadema nchini, hakuna anayependa kuona wakifikwa na madhila kama hayo yaliyowapata hapo jana, hivyo ni vyema kwa mtazamo wangu, viongozi wa Chadema wao binafsi, wawe wa kwanza kuchukua tahadhari kulinda usalama wao, badala ya kuacha kila jambo litokee bila kujali athari za kile kitachoweza kuwapata baadae.

Bado ninaamini, walikuwa na uwezo wa kumpokea Mbowe popote hata kilomita moja mbali na gereza, kwasababu kwanza alishaachiwa, pili nae alikuwa anaelekea maeneo ya makao makuu ya chama, hivyo kumuona Mbowe hiyo jana kwao ilikuwa ni lazima, bila kuathiri utulivu wa eneo la gereza kwa namna yoyote.

Ni vyema kila mtu achukue tahadhari kwa upande wake, kila mmoja popote alipo ajue anawajibika kulinda usalama wa mwingine bila kusababisha maumivu kwa yeyote.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaweza kubambikiziwa tu makosa na usisahau ilikuwa inafahamika kuwa wataenda kumpokea Mbowe wakati anatoka Magereza.

Pia,tambua kuwa mpaka sasa tumesikia tu kutoka upande mmoja(upande wa Magereza ambao ndio watuhumiwa) hivyo tusubiri pia kusikia kutoka kwa viongozi wa CHADEMA(wahanga) kabla ya kuhukumu yoyote.
 
Wanaweza kubambikiziwa tu makosa.

Pia,mpaka sasa tumesikia tu kutoka upande mmoja hivyo tusubiri kusikia kutoka kwa viongozi wa CHADEMA waliopigwa.
Regardless of all that, ukishajua unaeenda kuonana nae hamna mahusiano mazuri kati yenu, ni vyema ukaenda kwa tahadhari, ili kuhakikisha usalama wako pia, japo najua walioumizwa watakuja na maelezo yao, ila kwenye hili, kila mmoja alikuwa na ulazima wa kuhakikisha usalama wa mwenzake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akienda Humphrey Polepole anaingia ndani ya Uzio wa Gereza na Msafara wa Magari, Akiambatana na kundi la Waandishi wa habari pamoja na Wapiga Picha.

Ila Wakienda CHADEMA unawashauri Wangekaa hata Umbali wa Kilomita Moja Toka Gerezani.

Hizo Sheria, Utulivu na Unyeti wa Eneo mbona unabagua?

Acheni Double Standard ni Upumbavu uliokithiri.

Hakuna anayefurahia hao watu kupigwa, ni jukumu lao kulinda usalama wao, hakuna haja ya kushindana na kina Polepole kwenye viwanja vya magereza, hao wote tunajua wanabebwa na vyombo vya usalama na wao wamekiri, sasa viongozi wa Chadema hawawezi kushindana na marungu ya polisi na askari magereza, wataumizwa tu, wao wamezoea kushindana kwa hoja uraiani.

Chadema should not miss their target, adui yao ni CCM, sio askari magereza, wasipoteze muda kushindana na watu waliozoea amri tu, wataumizwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna anayefurahia hao watu kupigwa, ni jukumu lao kulinda usalama wao, hakuna haja ya kushindana na kina Polepole, hao wote tunajua wanabebwa na vyombo vya usalama na wao wamekiri, sasa viongozi wa Chadema hawawezi kushindana na marungu ya polisi na askari magereza, wataumizwa tu, wao wamezoea kushindana kwa hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haki Na Uhuru ni vitu vinavyotakiwa Kudaiwa kwa kila hali hata ikibidi kugharimu Uhai, HAKI HAIOMBWI.

Kuendelea kuwachekea na kuwabembeleza hawa Wapuuzi ni kuwapa uhuru wa kufanya wayafanyayo.

Acha Waendelee kutesa, Kuteka, Kupiga na Kupoteza yoyote wanayeona wanamhitaji lakini tunahesabu, na tunashukuru Kwamba Familia zao zipo huku huku Mitaani na Wao Tunakutana nao katika Bar Hizi hizi za Mitaani kwetu.

Muda utafika nasi tutachora mstari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani CHADEMA wanastahili lawama zaidi kuliko Jeshi la Magereza, sehemu zote za Majeshi ya ulinzi na usalama zina taratibu zake, na unaonywa kabisa madhara utakayokumbana nayo pindi utapovunja taratibu hizo.

Askari hafikiri kama raia na wala hatendi kama raia,ikumbukwe pia huyu askari anamafunzo na kakabidhiwa silaha za namna ya kudhibiti vurugu, juu ya yote yeye ni mtu anayesimamia sheria kutendeka.

CHADEMA wanamdudu wa kupenda kupigwa na vyombo vya dola, labda hili ndio SUM ya sera za chama chao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa namna ambavyo matukio mfululizo ya hivi karibuni yenye kuhusiana na Mh. Mboye yalivyojitokeza, kuna kila haja ya yeye kuchukua tahadhari kubwa. Wote tu mashahidi kuhusu yaliyotokea wakati wa mikutano yake akiwa jimboni kwa Hai.

Jana pia tulishuhudia nini kilichowatokea baadhi ya wanachama wa CDM waliojitokeza kwenda kumlaki baada ya kuachiliwa kutoka magereza. Yote yanatupa sura moja, nayo ni si nyingine bali "organized crimes" katika mikusanyiko ya wafuasi wake.

Hili jambo si la bahati mbaya hata kidogo, bali kuna watu wapo nyuma yake, wenye nia mbaya kwake wenye kumtaka kumsukuma kuhamasisha tahaluki ya makusudi, ili aingie ktk mtego wa kukosa uvumilivu na hatimaye kuwaruhusu wafuasi wake wajibu mapigo. Na akiingia katika mtego huo, atabambikwa kesi nyingine ambayo itampelekesha mpaka 2025.

Ni vyema akabuni mikakati mingine yenye kuondoa ushahidi wa mazingira kwake binafsi ama kwa viongozi wanaokuepo eneo husika. Kwa basi pale yatokeapo matukio mithili ya hayo, yeye ajisafishe kwa kumasisha utulivu hadharani na kusepa, lakini wawepo watu maalum waliondaliwa kuwashikisha adabu waleta vurugu wote waliopo ktk mikutano yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado hujaijua chadema vizuri moja ya mikakati yao ni kama hayo wanayoyafanya
Kutafuta kuanzisha vurugu kisha likisha tokea kama hili la kupigwa na kuwekwa ndani tayari huruma kwa jamii kuwa wameonewa wakati taratibu zote wanazijua..siasa za kiharakati hizo
 
Hivi walioenda kuwapokea akina Mdee,Bulaya,Matiko siku ya kwanza nao walipigwa? Au hakuna aliyeenda?
 
Bado hujaijua chadema vizuri moja ya mikakati yao ni kama hayo wanayoyafanya
Kutafuta kuanzisha vurugu kisha likisha tokea kama hili la kupigwa na kuwekwa ndani tayari huruma kwa jamii kuwa wameonewa wakati taratibu zote wanazijua..siasa za kiharakati hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli; hata huko Segerea wameenda kumpokea Mbowe kwa sababu ya matokeo ya kesi ya uongo iliyotengenezwa, Chadema kwenda kudai kiapo ilikuwa haki yao, hawakufanya vurugu, vurugu walianzisha polisi na mabomu yao ya machozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa namna ambavyo matukio mfululizo ya hivi karibuni yenye kuhusiana na Mh. Mboye yalivyojitokeza, kuna kila haja ya yeye kuchukua tahadhari kubwa. Wote tu mashahidi kuhusu yaliyotokea wakati wa mikutano yake akiwa jimboni kwa Hai.

Jana pia tulishuhudia nini kilichowatokea baadhi ya wanachama wa CDM waliojitokeza kwenda kumlaki baada ya kuachiliwa kutoka magereza. Yote yanatupa sura moja, nayo ni si nyingine bali "organized crimes" katika mikusanyiko ya wafuasi wake.

Hili jambo si la bahati mbaya hata kidogo, bali kuna watu wapo nyuma yake, wenye nia mbaya kwake wenye kumtaka kumsukuma kuhamasisha tahaluki ya makusudi, ili aingie ktk mtego wa kukosa uvumilivu na hatimaye kuwaruhusu wafuasi wake wajibu mapigo. Na akiingia katika mtego huo, atabambikwa kesi nyingine ambayo itampelekesha mpaka 2025.

Ni vyema akabuni mikakati mingine yenye kuondoa ushahidi wa mazingira kwake binafsi ama kwa viongozi wanaokuepo eneo husika. Kwa basi pale yatokeapo matukio mithili ya hayo, yeye ajisafishe kwa kumasisha utulivu hadharani na kusepa, lakini wawepo watu maalum waliondaliwa kuwashikisha adabu waleta vurugu wote waliopo ktk mikutano yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimewashauri wachukue tahadhari; maeneo au idara, taasisi nyingi za serikali, viongozi wa Chadema wanaonekana kama wahalifu, hata kama hawajakosea chochote, hivyo ni vyema wao binafsi sasa wachukue tahadhari kwa manufaa yao.

Siwafundishi uoga, nataka waendelee kuwa jasiri, but wasilazimishe mabishano kati yao na vyombo vya usalama kila wakati, kuumizwa kwao haitupendezi wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo linatokea pale kukiwa na masharti tofauti na upande mwingine mfano chukulia hivi kweli Kiongozi wa Chadema anaweza kukubaliwa kuitisha press ndani ya Magereza kama alivyofanya Hamphrey Polepole?

Mbona wao waliruhusiwa kuingia hadi ndani kumchukua Mashinji kwa nini wao wakubaliwe na Chadema wanapewa masharti kama ulivyosema wangesikiliza masharti waliyopewa kwani Magereza panatakiwa utulivu wa hali ya juu?

All in all kuna ubaguzi wa hali ya juu nchini especially inapotokea issue ya Chadema lazima kuwe na sintofahamu.CCM na Polepole walipoenda kumchukua Mashinji hawajapangiwa rote ya kupita lakini Chadema walipangiwa Rote wapitie Mbezi kwa nini?
 
Walienda nje ya muda ambao watu hawaruhusiwi kuwaona na kuwachukua wafungwa/mahabusu? au walienda usiku wa manane ikatafsiriwa kama wanataka kuwatorosha wafungwa, maana kipigo hadi mtu kuzimia siyo mchezo..
 
Hivi wale walioenda kuwapokea kina Bulaya mwanzo,utaratibu wao ulikuaje? Naomba kufahamishwa.
Tunaweza kua tunalaumu Chadema/Magereza bila kujua ukweli.
macson
 
Regardless of all that, ukishajua unaeenda kuonana nae hamna mahusiano mazuri kati yenu, ni vyema ukaenda kwa tahadhari, ili kuhakikisha usalama wako pia, japo najua walioumizwa watakuja na maelezo yao, ila kwenye hili, kila mmoja alikuwa na ulazima wa kuhakikisha usalama wa mwenzake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umeongea sawa, lakini nadhani ungehoji pia hizo sharia huwa zinafanya kazi upande mmoja tu !!???,
juzi wafuasi wa chadema walikwenda kumpokea Mh, Msigwa pale gerezani, ghafla wakakutana na wafuasi na wanachama wa ccm nao pia wakiwa wametumwa kwenda kumpokea/kumchukua Mh Msigwa, cha kushangaza, wafuasi wa chadema walizuiliwa kuingia kwenye himaya za gereza ilhali wale wa ccm wakaruhusiwa kuingia, na bahati nzuri Mh Msigwa akakataa kuchukuliwa na wafuasi wale wa ccm akaamua kutembea kwa miguu mpaka sehemu ambapo walikuwa wamesubiria wafuasi wa chademaa na akaungana nao, sasa naamini kuna maswali ya kujiuliza hapo ..
 
Back
Top Bottom