USHAURI: Walimu wakatwe mishahara tuwaongezee Wahudumu wa Afya

Hawa wahudumu hiii kazi wanayofanya Ni overtime au Ni kazi waliyoisomea na wakaomba ajira kuwa wanataka kuhudumu katika kada ya afya?Mtu anatimiza wajibu wake unaona Kama anajitolea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutokana na hari iliyopo duniani kwa sasa ni dhahiri tumeona umuhimu wa wauguzi wa sekta ya afya na pia ni watu wanaohitajika kulindwa na kutunzwa kwa hari yoyote ile ili wasiwe na manung'uniko na wanachokifanya.

Turudi kwenye mada,nimeona nitoe ushauri kwa serikali yetu Tukufu kuwa waalimu wote Tanzania nzima,wakatwe mishahara yao na kinachopatikana kiongezewe kwa wauguzi waliokatika shughuli nzito ya kupambana na ugonjwa kama Corona huku waalimu wakiwa mapumzikoni bila kazi yoyote.

Pia ugonjwa huu ukiisha na waalimu wakirudi katika shughuli za kikazi ndio walejeshewe mshahara wao wa mwanzo na wauguzi warudi katika kiasi walichokuwa wanalipwa sasa.

ASANTENI

Sent using Jamii Forums mobile app
Boresha maisha ya daktari nesi bila kuharibu maisha ya mwingine,unaposomea udaktari unesi ukae ukijua Kuna siku utakuwa unahudumia wagonjwa kama wa Corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakatwe tu,maanaWamezidi mno unyumbu,hawa si ndiyo wasimamizi wa chaguzi zote,na wakipewa 20,000=wanapindua matokeo.
We jamaa hujui chochote kuhusu Uchaguzi.Hata mie zamani nilikuwa na mawazo Kama yako kuwa wale wanaosimamia Uchaguzi vituoni ndio wanaopindua matokeo.
Yaani nikiona mtu anasema wanaosimamia Uchaguzi vituoni ndio huwa wanapindua matokeo huwa naona Kama sijui mjinga wa wapi sijui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nazani cha moto wamekipata miaka 5 jiwe kafunga vioo kama hawajui vile ila cha kushangaza utawaona kweny UCHAGUZI wanavyo pindua meza kumpitasha Tena jiwe sijui wanaubongo wa namna gan hawa viumbe
Nilikuwa na mawazo Kama yako zamani.Na sikuishia tu kuwa na mawazo Kama hayo,nilipata ujasiri wa kudadisi hayo matokeo huwa yanapinduliwa namna gani kwenye kituo Cha kupigia kura?
2010 nilijitosa kufanya utafiti wangu,pia ,2015 nilichokiona na ninachoamini kwenye kituo matokeo Wala huwa hayapinduliwi hata robo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama walimu inapendekezwa kua wakatwe moshahara eti kisa wako tu nyumbani hawafanyi kazi yoyote(na inajulikana asiyefanya kazi na asile),basi na wale wote ambao kwa nsmna moja au nyingine,wapunguziwe kiasi flani cha mishahara yao, mfano;mawaziri, wabunge, makatibu wakuu n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani mishahara ya walimu ni mikubwa kuliko ya madaktari/wahudumu wa afya?
Mtoa mada umetumia criteria gani?
Kwanini usiseme wahudumu wa afya waongezewe tu mishahara kwa kipindi hiki?
Je walimu wangekuwa wamekaa miezi 3 nyumbani ungesemaje? Watu acheni uchawi.
Wivu ni uchawi mbaya sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutokana na hari iliyopo duniani kwa sasa ni dhahiri tumeona umuhimu wa wauguzi wa sekta ya afya na pia ni watu wanaohitajika kulindwa na kutunzwa kwa hari yoyote ile ili wasiwe na manung'uniko na wanachokifanya.

Turudi kwenye mada,nimeona nitoe ushauri kwa serikali yetu Tukufu kuwa waalimu wote Tanzania nzima,wakatwe mishahara yao na kinachopatikana kiongezewe kwa wauguzi waliokatika shughuli nzito ya kupambana na ugonjwa kama Corona huku waalimu wakiwa mapumzikoni bila kazi yoyote.

Pia ugonjwa huu ukiisha na waalimu wakirudi katika shughuli za kikazi ndio walejeshewe mshahara wao wa mwanzo na wauguzi warudi katika kiasi walichokuwa wanalipwa sasa.

ASANTENI

Sent using Jamii Forums mobile app
unajua maana ya permanent employee?
 
Mbona maisha ni magumu zaidi,afadhali ya shuleni,sababu tunakunywa chai ya bure,chakula cha mchana bure ambayo ni michango ya watoto,tukikatwa mishahara tena mbona tutafariki,hayo ni majukumu yao wapambane,wakizidiwa tutawaongozea na majeshi pia nako kuna wataalam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutokana na hari iliyopo duniani kwa sasa ni dhahiri tumeona umuhimu wa wauguzi wa sekta ya afya na pia ni watu wanaohitajika kulindwa na kutunzwa kwa hari yoyote ile ili wasiwe na manung'uniko na wanachokifanya.

Turudi kwenye mada,nimeona nitoe ushauri kwa serikali yetu Tukufu kuwa waalimu wote Tanzania nzima,wakatwe mishahara yao na kinachopatikana kiongezewe kwa wauguzi waliokatika shughuli nzito ya kupambana na ugonjwa kama Corona huku waalimu wakiwa mapumzikoni bila kazi yoyote.

Pia ugonjwa huu ukiisha na waalimu wakirudi katika shughuli za kikazi ndio walejeshewe mshahara wao wa mwanzo na wauguzi warudi katika kiasi walichokuwa wanalipwa sasa.

ASANTENI

Sent using Jamii Forums mobile app
We K tu
 
Back
Top Bottom