Ushauri Wakuu Fridge kwa bajeti ya Around 400K

Ushauri Wakuu Fridge kwa bajeti ya Around 400K

Nafuatilia kwa ukaribu nataka nikadake kafriji kakibachela kadogo tu
 
used nyingi hazina 'thermostat, linawaka moja kwa moja hivyo kukosa kujizima kunachangia umeme kwenda mwingi au rubber zikiisha linaruhusu hewa kutoka na kufanya kuendelea kuwaka kwa mda mrefu
Mimi ninalo used,linakula umeme balaa,nimeachana nalo kwa sasa,kuna uwezekano wa modification yyt ya kulifanya litumie kwa kiasi kidogo?
 
Ulimaanisha matumizi ya kiseja au kisela?

Ok kama ni kiseje natumai upo na mtu hapo mnaishi pamoja bila ndoa. Basi tafuta Jokofu simple lipya kabisa unapata

Kama ni kisela basi hapo ina maana upo mwenyewe tu labda anakuja na kuondoka mtu basi hapo ata 300K unapata jokofu simple dogo fresh jipyaa kabisa.

Brand tafuta Nikai, European au Boss hizi naziona nzuri kwa mtazamo wangu

NB: Kamwe! Usinunue jokofu la MTUMBA/USED pia Kamwe usinunue jokofu kubwa kama kabati kisa ufahari. Utajutia matumizi mabaya ya fedha zako
 
Tafuta 300K unapata kafriji safi kapya simple rangi inawaka kama ya Range Rover sport, wanaviita friji mayai hata umeme havijui kula, yaani kafriji flani ukifunga mlango unaweza hisi umekaumiza [emoji23]
Teh Teh Teh mkuu umetisha... K/koo bila shaka ?
 
Yah, unashuka kule chini kwenye machimbo usiulizie huju juu watakupiga hela nyingi

Kwenye machimbo ndio maeneo gani, pale maduka ya mtaa wa China Plaza!!! Kama unatoka Benjamin Mkapa Secondary!!
Maana pale ndio naonaga mafriji kwa nje
 
Kwenye machimbo ndio maeneo gani, pale maduka ya mtaa wa China Plaza!!! Kama unatoka Benjamin Mkapa Secondary!!
Maana pale ndio naonaga mafriji kwa nje
Walanguaji wale nyoosha ile road kama unaenda mnazi mmoja ila haufiki mnazi mmoja anzia congo pale cheza left na right mitaa hiyo ndio kuna fridge za bei nzuri yaani wholesalerna Dealer hasa usidili na wabongo deal na Wahindi wabongo ni madalali hivo akikwambia bei laki 7 basi ujue hapo ni laki 6 hadi 5 na nusu.
 
kanunue yale ya kichina sio mabaya kuliko kununua used. mimi nilalo bruhm nilinunu laki 4 kamili milango miwili lipo poa
Mkuu unaeza ukatusaidia hata picha ili angalau tupate mwanga zaidi
 
Mkuu unaeza ukatusaidia hata picha ili angalau tupate mwanga zaidi
hii hapa
IMG_20190502_003734.jpeg
 
Back
Top Bottom