Ushauri wako wa dhati unaweza kunifanikishia sana. naomba nisaidie.

Tasia I

JF-Expert Member
Apr 21, 2010
1,223
193
JF heshima kwenu,
kutokana na utaalam, uzoef, exposure n.k naomba kwa dhati kabisa
mnishauri.
Siku zote hua natamani sana niachane na kazi ya kuajiriwa. na ni ndoto yangu kujiajiri na kuwaajiri watu wengine siku moja
haswa kuptia biashara.
Kutokana na kipato changu, sina uwezo wa kusema nitaanza investment kuubwa sana
kwasababu ya capita. lakini kwa hapa nilipofikia siku sio nyingi naweza kua na kiasi cha milioni zaidi ya kumi na sio zaidi ya 12.
naombeni mnisaidie mawazo.

Ni biashara gani nayoweza kufanya kwa hela hii, na ni sehem gani?
Kama mtu akiweka na mchanganuo hata kama sio kwa kina nitasaidika zaidi.
Sichagui saana sehem yakufanyia endapotu biashara ipo na inalipa.

Ahsanteni woote.


 
Kikawaida Mjasiriamali hujaribu kufanya yale ambayo wengine hawawezi kufanya,ninachotaka kukushauri ni kwamba Nchi yetu bado ni nchi inayohitaji watu wanaoweza kuikomboa kutoka katika mgandamizo mkubwa wa uchumi unaofanywa ama kusababishwa na watu wasiojua vema matumizi ya rasilimali za Nchi yetu hali inayosababisha uchumi wa Nchi yetu kushikiliwa na wageni kutoka bara hindi(india) kwa kiasi kikubwa.

Kabla sijakushauri chakufanya ningependa nikushauri ufikiri kwanza namna gani unaweza wewe kwa nafasi yako kutatua japo kwa sehemu baadhi ya matatizo yanayo wakabili watanzania kwani kwa kufanya hivyo unaweza kujipatia njia ya kuendeshea hicho kiasi cha fedha ulicho nacho ambacyo naamini kinatosha kukufanya ujihisi upo katika nchi ya neema,kwa mfano wakati nchi ipo katika tatizo la umeme wewe ni shahidi kuwa wapo waliojipatia mabilioni ya shilingi kwakile walichoita ni kutatua matatizo ya watanzania (dont take it negatively)Nikupe mfano mwingine ni kuhusu tatizo la usafiri hapa Nchini,wakati watanzaia wengi tulikuwa na nafikiri bado tuanasoma ili tupate kazi wenzetu kutoka china walikuja wakafanya survey wakagundua kwamba kama wakileta bodaboda hapa itakuwa the big deal bila kuchelewa wakazimwaga kama njungu in terms of quantity but not quality kwakuwa walijua TBS ya hapa kwetu haijui kuhusiana na hilo.

Wakati zinaingia hapa Nchini walioona mabli walizichangamkia na waka make money coz demand ilikuwa kubwa kuliko supply wakati watu wanashtuka mahitaji ya bodaboda yanakuwa sawa na wasambazaji wa huduma hiyo so the most important thing hapa ni kutambua fursa na kuzitumia bila kuchelewa.

Wakati nataka nikushauri chakufanya ngoja nikupe mfano mmoja hivi then utaona ni namna gani tanzania tunahitaji kuamka na unaheri kukimbilia huku ubarikiwe sana,yeah kuna wajasiriamali wa kichina wapo chanika wanajiita EGG-ENERGY nenda kwenye goooogle utawaona utaona wanachofanya then utajua tanzania katiak vyou vyetu tunazalisha wanasiasa matapeili na sio wajasiriamali kwani kama wangekuwepo tungeweza kufanya kile wanachifanya hawa wachiuna kule chanika.

Ninachotaka nikuambie ni kwamba kitu pekee kinachoweza kutukwamua Watanzania tuanaoelemewa na kuendelea kumezwa na sera za kibepari USHIRIKA ndiyo njia pekee itakayoweza kutukwamua livyovyote vile iwe kiuchumi kijamii na vinginevyo,JF imegunadua hilo dat why, we have introduce JE saccos so please come and join us,it is safe place.

India ni moja kati ya Nchi zinazoendelea kufanya vizuri katika uchumi lakini moja kati ya sababu kubwa ni kwamba walijua the value of cooperation.

What I would like to suggest you ni kwamba Katika Financial instuties hapa Tanzania nikiwa na maana ya Bank,saccos nakadhalika bado zinafanya vizuri saana kwasababu ya sera mbovu ya serikali yetu nikiwa na maana viwango vya riba ni vikubawa mno mno yani vinanufaisha wamiliki wa Bank hizo na sio wateja wa Bank hizo na hapa na zungumzia Pride huyu jamaa Pride anahitaji Competitor coz bado anaendelea kuwanyonya wananchi sasa na kushauri bora ukumbuke shuka mapema tafuta wenzako anzeni Saccos itangazeni baada ya muda mtamiliki Bank kubwa sana Nchini na Nje ya Nchi.

Kama haya ni mawazo magumu sana Ninakushauri tena kwa upole anza biashara ya nafaka yani mchele, maharage na mahindi anza kuuza hapa Dar kwa bei ya ushindani yani kama faida kwa kila Kg ni shilingi 150 basi wewe kubali kupata 100 kwa kila Kg nataka ni kwambie itakusaidia na kukufanya wewe kuwa kwenye operation katika hali isiyo kukatisha tamaa.

Unless otherwise unahitaji upembuzi yakinifu ambao bila shaka wan JF Hawatasita kukupatia.

God bless you

Naomba nisilaumiwe kwa makosa ya kiuandishi
 
Mkuu Richardbr nashukuru, nimesoma ushauri wako na kuuelewa.
asante sana.
niwasubirie wana JF wengine wanipe mawzo yao af mwiho nita conclude na kujua nini cha kufanya wakati ukifika.
karibuni wengine nanyi mnipe maujanja.
 
Back
Top Bottom