Naomba ushauri jinsi ya kumuacha huyu Mwanamke mwenye upendo wa dhati

Kraftwerk

JF-Expert Member
Mar 11, 2019
227
321
I hope hamjambo ndugu zangu wote wana JF.

Naomba kutanguliza samahani kwa yoyote nitakae mkwanza juu ya hili naomba ushauri wenu nifanye nn? Mnivumilie sio mwandishi mzuri sana. Katika mishe zangu za kila siku nilitokea kuonana na mdada fulani kiukweli mzuri wa kila kitu na mwenye kazi yake na sehemu yake ya kuishi na mwenye dini haswa na mwenye kujistiri.

Kikweli baada ya kumuona nilitokea kuvutiwa naye na kuongea naye na kuchukua number yake na alivutiwa na mimi tangu siku ya kwanza tu kuongea naye she’s was so happy kuongea na mimi.

Tuliendelea kuongea kawaida as friends after 3 weeks nijaribu kufikisha hisia zangu juu yake nieleze kiasi gani nimevutiwa nae na kutokea kumpemda toka the first day kuonana nae.

Tuliingia kwenye mahusiano rasmi ya kimapenzi. Kiukweli sikuwa nimempenda zaidi ya kumtamani mwili wake. Kadri siku zinavyozidi kwenda nikiona anazidi kunionesha kunipenda na kujail zaidi kuhusu mimi kuletewa zawadi kama t-shirt, saa na viatu nikiwa sijawahi kumpa chochote na zaidi hali yangu ya kiuchumi nimemzidi kwa kila kitu

After many days tulikutana kimwili zaidi ya mara tatu after that nilianza kuwa busy hata nikiona simu yake nahisi kama ananisumbua hata kujibu text nashindwa na hachoki kutuma texts wala kupiga anaishia kulia kila siku. Sometimes naumia kumuona hivyo ila i want her to move on na maisha yake kizazaa kilianza hapa.

Kwa yote niliyofanyia hakuweza kuniacha wala kuniambia sikutaki aliendelea kunivumilia mengi niliyofanya sidhani kama kuna mwanamke anaweza kuvumilia na kuendelea kuwa na mwanaume huyo. Niumia zaidi kumuona akiteseka niliamua kumwambia tuachane hataki kusikia hilo wala kuelewa alisema siwezi kuachana na wewe na weka akilini mwako. Niliamua kumblock number zake maybe angekuweza ku-move on ila hali kutokea hilo alianza kunitafuta na kila number anaweza hata akaomba hata number ya mpita njia anipigie mimi na kuanza kulia hata mbele za watu kwanini nimemblock.

Kila siku anasema mimi siwezi kukuacha kamwe na nipo tayari kwa kila kitu hata ukioa mwanamke mwingine zaid yangu nipo tayari kukuzalia ila kuwa na mwanaume mwengine siwez btw nimeshindwa kumuacha wala kuniacha na hakuwahi kula hela yangu hata siku moja zaid ya kulipia hotel tulale. Naomba radhi juu ya hili ni hisia tu.

NAOMBA USHAURI NIFANYE NINI NA SIPO TAYARI KUWA MUME WAKE NA ANAJUA HILO
 
Siku zote hit and run huwa haiwi ivyo na wewe uliingia kwa lengo hilo. Kosa ulilofanya ulijenga kibanda halafu unashtuka ushamaliza kujenga na mwenzako keshahamia na ndio maana hata wewe unashindwa kutoka kwa sababu mmeshakua na sababu za kuwa pamoja na sio breakup kwa sasa.

Muhimu la kukushauri kaeni chini umueleze kila kitu ikiwezekana hata sababu za uongo zitakazomfanya akae mbali na wewe ikifanikiwa hiyo hakikisha unakaa mbali na usipate hata nafasi ya kukaa mbele ya upeo wa macho yake itamsaidia kukusahau haraka.

Lakini najiuliza swali, kwanini unamkataa mwanamke anakulilia kabisa? Au ni single maza unajaribu kukwepa majukumu

Ila hakikisha humfanyii hivi mwanamke mwingine hawa viumbe wakipenda wanaweza hata kuua.
 
Mkuu ni pm namba yake nimkanye kwa tabia yake mbaya,baada ya wiki moja atakupigia simu kukuchekelea na sio kukulilia tena
 
Siku zote hit and run huwa haiwi ivyo na wewe uliingia kwa lengo hilo. Kosa ulilofanya ulijenga kibanda halafu unashtuka ushamaliza kujenga na mwenzako keshahamia na ndio maana hata wewe unashindwa kutoka kwa sababu mmeshakua na sababu za kuwa pamoja na sio breakup kwa sasa.

Muhimu la kukushauri kaeni chini umueleze kila kitu ikiwezekana hata sababu za uongo zitakazomfanya akae mbali na wewe ikifanikiwa hiyo hakikisha unakaa mbali na usipate hata nafasi ya kukaa mbele ya upeo wa macho yake itamsaidia kukusahau haraka.

Lakini najiuliza swali, kwanini unamkataa mwanamke anakulilia kabisa? Au ni single maza unajaribu kukwepa majukumu

Ila hakikisha humfanyii hivi mwanamke mwingine hawa viumbe wakipenda wanaweza hata kuua.

Hapa sio single mother n she’s only 24 years.
 
Back
Top Bottom