Ushauri wako .... Nani aanzishe maongezi?

Ushauri wako .... Nani aanzishe maongezi?

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Nimekaa nalo mda mrefu limenitesa, naomba nilitoe kwenu waungwana;

Nilikuwa na rafiki (wa kike); tuliheshimiana sana, tulidumu kwenye urafiki kwa zaidi ya miaka miwili pasipo kuingiliwa na tamaa za mwili. Baada ya muda uzalendo ulitushinda tukaanza kuhudumiana. Siku moja nikatoka naye out, wakati tumekaa akatokea jamaa yangu tukakaa meza moja, tukaendelea kubadilishana mawazo kama kawaida.
Baada ya miezi kama mitatu hivi, mawasiliano kati yangu na huyo m/mke yakawa yamepungua, mara nimpigie asipokee, mara sms hapokei; nikaamua kumpotezea pia.

Mwaka na nusu hivi; akarudisha mawasiliano; akanambia ana maongezi na mimi na yuko hotel fulani niende tuonane. Nilipoenda namkuta yuko mezani kakaa peke yake ila meza jirani kuna binti amepakata kichanga.

Aliponiona alinitazama sana usoni kwa kunikazia macho; nikamuuliza kulikoni akadai atanieleza ....

Baadaye akasema nimsamehe, nikamuuliza kwa lipi, akanambia alipitiwa na shetani akatenda tendo na rafiki yangu na ndo kilichomfanya apotee kwenye mawasiliano. Nikamuuliza rafiki yangu yupi, akadai atanieleza baadaye.

Nikamwambia wala hilo si kosa - ni maamuzi tu;

Sasa m/mke huyo anapenda sana mambo ya outing, lakini rafiki yangu alomzalisha hapendi - hivyo mara nyingi anapenda nitoke naye out japo kwa maongezi kama ilivyokuwa mwanzoni kabla ya kuingia kwenye mahusiano ya kimwili - mi naona noma, m/mke huyo anamwambia rafiki yangu anijulishe kwamba amenikosea - rafiki hataki kusema chochote.

Je! ni nani anapaswa kuweka mambo wazi hili huyo rafiki yangu ajue kwamba mi tayari najua kwamba kazaa na huyo m/mke? a) Mimi b) M/mke c)Rafiki yangu. NAWASILISHA
 
Ah mkuu msamehe tu. Wanawake wa siku hizi wana mitego sana na wengi wetu we aint that strong. I've been on both sides of the fence so I know what I am talking about. Usipende kuweka ukaribu wa demu wako na washkaji, watamkamua tu. Huu u-magharibi wa "shemeji lets go for a drink sijui let's go for a movie" hapana aise. Ah, follow your heart dude. Bros before "hos" dude, bros before "hos"
 
Binafsi sioni kama ana kosa lolote; case inakuja pale yeye anapotaka kuendeleza ukaribu na mimi wakati rafiki yangu huyo yupo na kibaya zaidi hamjali, mi nimjali mtoto wakati najua kabisa kwamba sio wa kwangu. M/mke anafika hatua analia hadi namhurumia lakini ninachohitaji ni kuhakikisha wote watatu tumekaa na kuliweka sawa hili; nani aanzishe mchakato huo wa maongezi
 
Ondoa huo ukaribu anaotaka Tutor B na mweleze kabisa ushazaa na rafiki yangu mind your business kama ni kutoka mwambie mtoke na rafikio akiwepo au na wewe ukiwa na mtu wako na sio kukuwekeza mazingira tutoke wawili tuu na shetani alinipitia hapo hakuna cha shetani maana alikuwa na akili zake wakati anafanya hiccho kitendo
 
Last edited by a moderator:
Ni huyo rafiki yako uliyesema pale mwanzoni kuwa alikuja wakati uko na huyo dada outing mkakaa nae meza moja? Sasa we unatakaje kwani hapa mi sijaelewa mkuu, si jamaa alishakuzidi maarifa akalala na mpenzi wako na akamzalisha juu! We ulitakaje labda, uendelee na huyo dada au udumishe urafiki na jamaa yako au vyote?
 
Nashukuru kwa ushauri wako rafiki yangu wa muda mrefu, najua wewe usingefanya kama huyu alivyofanya - ila binafsi wala hainiumizi kichwa.
 
Nashukuru kwa ushauri wako rafiki yangu wa muda mrefu, najua wewe usingefanya kama huyu alivyofanya - ila binafsi wala hainiumizi kichwa.

Muhimu mkuu Tutor B kuwa makini tuu na wewe usijeishia kusema shetani alinipitia nikafanya nae utakuwa umerudi k ule kule kwa rafikio
Mweleze wazi kuwa ana mtoto na rafikio na amheshimu na masuala yako na wewe yalishaisha huwezi kurudi nyuma ulikotoka
 
Last edited by a moderator:
anayetaka suluhu ni huyo dada na ndiye atakayeanzisha mazungumzo.... awaite nyote na aseme anachoona kwake kitampa amani ya moyo ila kalikoroga vibaya
 
anayetaka suluhu ni huyo dada na ndiye atakayeanzisha mazungumzo.... awaite nyote na aseme anachoona kwake kitampa amani ya moyo ila kalikoroga vibaya

Huyo dada anadai eti mwenye mtoto hataki mimi nijue; na anamtishia kwamba akijua kwamba nimejua hatatoa huduma yoyote kwa mtoto na hatahitaji tena mawasiliano na huyo mdada.
 
Muhimu mkuu Tutor B kuwa makini tuu na wewe usijeishia kusema shetani alinipitia nikafanya nae utakuwa umerudi k ule kule kwa rafikio
Mweleze wazi kuwa ana mtoto na rafikio na amheshimu na masuala yako na wewe yalishaisha huwezi kurudi nyuma ulikotoka
Thanx Great thinker!
 
Ni huyo rafiki yako uliyesema pale mwanzoni kuwa alikuja wakati uko na huyo dada outing mkakaa nae meza moja? Sasa we unatakaje kwani hapa mi sijaelewa mkuu, si jamaa alishakuzidi maarifa akalala na mpenzi wako na akamzalisha juu! We ulitakaje labda, uendelee na huyo dada au udumishe urafiki na jamaa yako au vyote?

Nataka uwazi uwepo ili mdada wa watu awe huru.
 
kwani mlikuwa na mkataba gani mpaka muyaongee hayo? si mlihudumiana tu? yaacheni kama yalivyo
 
Back
Top Bottom