Nimekaa nalo mda mrefu limenitesa, naomba nilitoe kwenu waungwana;
Nilikuwa na rafiki (wa kike); tuliheshimiana sana, tulidumu kwenye urafiki kwa zaidi ya miaka miwili pasipo kuingiliwa na tamaa za mwili. Baada ya muda uzalendo ulitushinda tukaanza kuhudumiana. Siku moja nikatoka naye out, wakati tumekaa akatokea jamaa yangu tukakaa meza moja, tukaendelea kubadilishana mawazo kama kawaida.
Baada ya miezi kama mitatu hivi, mawasiliano kati yangu na huyo m/mke yakawa yamepungua, mara nimpigie asipokee, mara sms hapokei; nikaamua kumpotezea pia.
Mwaka na nusu hivi; akarudisha mawasiliano; akanambia ana maongezi na mimi na yuko hotel fulani niende tuonane. Nilipoenda namkuta yuko mezani kakaa peke yake ila meza jirani kuna binti amepakata kichanga.
Aliponiona alinitazama sana usoni kwa kunikazia macho; nikamuuliza kulikoni akadai atanieleza ....
Baadaye akasema nimsamehe, nikamuuliza kwa lipi, akanambia alipitiwa na shetani akatenda tendo na rafiki yangu na ndo kilichomfanya apotee kwenye mawasiliano. Nikamuuliza rafiki yangu yupi, akadai atanieleza baadaye.
Nikamwambia wala hilo si kosa - ni maamuzi tu;
Sasa m/mke huyo anapenda sana mambo ya outing, lakini rafiki yangu alomzalisha hapendi - hivyo mara nyingi anapenda nitoke naye out japo kwa maongezi kama ilivyokuwa mwanzoni kabla ya kuingia kwenye mahusiano ya kimwili - mi naona noma, m/mke huyo anamwambia rafiki yangu anijulishe kwamba amenikosea - rafiki hataki kusema chochote.
Je! ni nani anapaswa kuweka mambo wazi hili huyo rafiki yangu ajue kwamba mi tayari najua kwamba kazaa na huyo m/mke? a) Mimi b) M/mke c)Rafiki yangu. NAWASILISHA