asakuta same
JF-Expert Member
- Mar 1, 2011
- 14,829
- 5,041
Nataka uwazi uwepo ili mdada wa watu awe huru.
kwanini umjali namna hiyo , kwani jamaa alimbaka mkuu?
Nataka uwazi uwepo ili mdada wa watu awe huru.
ndivyo ilivyo, je nimweleze huyo rafiki yangu ili asitelekeze kiumbe na huyo mdada au ninyamaze? alafu kibaya jamii inajua kwamba mi ndo mhusika wa kiumbe - nami kwa umri wangu nimekaa nalo kichwani mwangu sitaki kukubali wala kukanusha.
Binafsi sioni kama ana kosa
lolote; case inakuja pale yeye anapotaka kuendeleza ukaribu na mimi
wakati rafiki yangu huyo yupo na kibaya zaidi hamjali, mi nimjali mtoto
wakati najua kabisa kwamba sio wa kwangu. M/mke anafika hatua analia
hadi namhurumia lakini ninachohitaji ni kuhakikisha wote watatu tumekaa
na kuliweka sawa hili; nani aanzishe mchakato huo wa maongezi
kwanini umjali namna hiyo , kwani jamaa alimbaka mkuu?
Hivi huyo ni rafiki yako kweli? kama alikuchukulia mpenzi wako atashindwa nini kumchukua mkeo? mimi naona hafai kuwa rafiki. any way huyo dada ingekuwa mimi wote ningeachana nanyi afu natunza mtoto wangu kivyangu. Maana inavyoonekana ni kama amepoteza direction kwa yule aliezaa nae hamtaki nawe pia umtaki, kwako huna makosa coz yeye ndie alikusaliti ila ninachosema ni kuwa ataendelea kulia mpaka lini hana kazi ya kufanya? Yeye ni mama yapaswa awe imara.
Nimekaa nalo mda mrefu limenitesa, naomba nilitoe kwenu waungwana;
Nilikuwa na rafiki (wa kike); tuliheshimiana sana, tulidumu kwenye urafiki kwa zaidi ya miaka miwili pasipo kuingiliwa na tamaa za mwili. Baada ya muda uzalendo ulitushinda tukaanza kuhudumiana. Siku moja nikatoka naye out, wakati tumekaa akatokea jamaa yangu tukakaa meza moja, tukaendelea kubadilishana mawazo kama kawaida.
Baada ya miezi kama mitatu hivi, mawasiliano kati yangu na huyo m/mke yakawa yamepungua, mara nimpigie asipokee, mara sms hapokei; nikaamua kumpotezea pia.
Mwaka na nusu hivi; akarudisha mawasiliano; akanambia ana maongezi na mimi na yuko hotel fulani niende tuonane. Nilipoenda namkuta yuko mezani kakaa peke yake ila meza jirani kuna binti amepakata kichanga.
Aliponiona alinitazama sana usoni kwa kunikazia macho; nikamuuliza kulikoni akadai atanieleza ....
Baadaye akasema nimsamehe, nikamuuliza kwa lipi, akanambia alipitiwa na shetani akatenda tendo na rafiki yangu na ndo kilichomfanya apotee kwenye mawasiliano. Nikamuuliza rafiki yangu yupi, akadai atanieleza baadaye.
Nikamwambia wala hilo si kosa - ni maamuzi tu;
Sasa m/mke huyo anapenda sana mambo ya outing, lakini rafiki yangu alomzalisha hapendi - hivyo mara nyingi anapenda nitoke naye out japo kwa maongezi kama ilivyokuwa mwanzoni kabla ya kuingia kwenye mahusiano ya kimwili - mi naona noma, m/mke huyo anamwambia rafiki yangu anijulishe kwamba amenikosea - rafiki hataki kusema chochote.
Je! ni nani anapaswa kuweka mambo wazi hili huyo rafiki yangu ajue kwamba mi tayari najua kwamba kazaa na huyo m/mke? a) Mimi b) M/mke c)Rafiki yangu. NAWASILISHA
Kwanza kabisa nakupa pole kwa hayo yaliyokukuta. Kuwa mtu wa kufikiri na si wa kufikiriwa, kumbuka huyo mwanamke na rafiki yako ni wasaliti na hawakutaka kabisa wewe ujue ndiyo maana mwanamke akakata mawasiliano muda wote huo, rafiki yako naye mpaka sasa hataki ujiwe mahusiano yao na huyo mama mtoto wake.
Kwanza kabisa huyo mwanamke alikudharau ndiyo maana katembea na rafiki yako uliyemtambulisha kwake, na rafiki yako pia ni mnafiki kutembea mpenzi wako huku akiwa anajua, inasikitisha maana rafiki yako ni mkaidi na hajutii alichofanya ndiyo maana mpaka sasa hataki ujuwe.
Ushauri: Simama kama mwanaume kuna mambo mengi ya kufanya yenye maana kuliko huo mchezo wa kuigiza mnaoucheza ninyi nyote watatu. Mwanamke huyo hakupendei kitu chochote zaidi ya muda wako unaoupoteza kwa ajili yake na outing za kinafiki maana angekuwa anathamini outing zako asingekusaliti. Kula wale wengine attention utowe wewe, huo ni uzuzu, fungua macho mkuu huyo kisha bugi sasa anataka na wewe ubugi mfanane.
i would advice you to end just there, as she is a committed mother of your friends kid; dont even try to think of revenging to your friends behaviours; this is just my opinion, but u r free to follow your heart!
sasa wewe una wasiwasi wa nini, we achana naye huyo dada usije jitia nuksi bure maana atazidi kukuzoea hadi utakapokuwa na mpenzi wako akakuletea majanga maana mazoea naye yatakuwa yamezidi...hajatulia huyo KAA NAYE MBALI!
Sasa kama huyo mwanamke kashaolewa.wewe unamfuata nini wakati hadi mtoto anaye; ni jambo tu la kawaida maana haina haja tena.vunginevyo ni wewe unajipa presha na mitoko isiyokua chachu.
Nashukuru kwa kuelewa japo nakushangaa kwa kuendelea kukumbatia mnafiki na kumuita rafiki, nahisi bado hujatambua maana ya urafiki au inawezekana wewe bado kijana mdogo unaendeshwa na story za mtaani kuwa huwezi vunja urafiki kisa mwanamke. Wote ni wapuuzi na wanafiki chamsingi ni kuwasamehe na kuachana nao badala ya kuendelea kumkumbatia ipo siku atakuja zaa na mkeo siku ukioa. Au anakupa vimisaada? hata Bible inasema ajifanyiae marafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe ila yupo rafiki wa kweli ambatanae na mtu kuliko ndugu. Usiendekeze urafiki usiokuwa na manufaa kwako, kuwa makini, simama imara jiamini kila kitu kinawezekana.Umenishauri vyema na nitavua hali ya huruma na kuuvaa ukatili, kuanzia sasa sitokuwa na mawasiliano kwa wote; najua nitaweza na maadam w/end ndo hiyo inakuja, J.tatu nitaku-PM nikwambie kitakachokuwa kimeendelea kwenye w/end hii. Nitawakutanisha pasipo wao wote kujua ili nisome nyuso zao zitatoa majibu gani. Binafsi naona si vyema kuvunja mahusiano na rafiki wa kiume kwa sababu ya mwanamke mpuuzi kama huyo.
Nashukuru kwa kuelewa japo nakushangaa kwa kuendelea kukumbatia mnafiki na kumuita rafiki, nahisi bado hujatambua maana ya urafiki au inawezekana wewe bado kijana mdogo unaendeshwa na story za mtaani kuwa huwezi vunja urafiki kisa mwanamke. Wote ni wapuuzi na wanafiki chamsingi ni kuwasamehe na kuachana nao badala ya kuendelea kumkumbatia ipo siku atakuja zaa na mkeo siku ukioa. Au anakupa vimisaada? hata Bible inasema ajifanyiae marafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe ila yupo rafiki wa kweli ambatanae na mtu kuliko ndugu. Usiendekeze urafiki usiokuwa na manufaa kwako, kuwa makini, simama imara jiamini kila kitu kinawezekana.
Nakubaliana nawe; je unajua tulikuwa na biashara ipi mimi na huyo m/mke tofauti na mahusiano ya kimapenzi?