Ushauri wa Shemeji Yangu

Ushauri wa Shemeji Yangu

Habari za Jumapili wadau

Kuna sintofahamu kuhusu usalama wa privacy zetu humu lakini watajua wenyewe. Watakuwa wameshauza ramani ya vita kwa adui. Sasa hatuandiki tena habari wanazozitafuta. Shauri zao....twende kwenye mada.

Mke wa best yangu, rafiki yangu wa kufa na kuzikana, siku moja nilimueleza kitu naye akanishauri bila kumuomba ushauri, au niseme alitoa maoni yake.

Ilikua tunapita mahali karibu na duka, rafiki yangu akaingia dukani kununua baadhi ya vitu mimi nikabaki na shemeji tukitembea mdogo mdogo ili tusije mwacha jamaa mbali. Kipindi hicho wana mwaka 1 tu wa ndoa yao.

Nikamwambia shemeji mi nataka kuoa ila mwanamke ninayetaka kumuoa hayuko tayari kwa sasa, nataka kuforce. Kimsingi mwanamke huyo ameshamaliza masomo na ameshaanza kazi ana kipato cha kujikimu lakini hayuko tayari kwa ndoa muda huu. Akaniuliza sababu ni nini? Nikamjibu mwanamke anasema anahisi ana deni kwa familia yake, yaani anawaza kuijengea, kuihudumia, na kuipa sapoti na hasa mama yake mzazi. Kwa hiyo hadi atakapoona familia hiyo ipo kwenye hatua anayoitaka ndio awe tayari kwa ndoa.

Akahoji, hayo yatachukua muda gani? Jibu langu likawa kwa kweli sijui. Akaniambia, shem huyo mwanamke achana naye. Ndio yule xxx (akamtaja) uliesema mwanafunzi wa chuo? Sasa mtu umekuwa naye miaka yote hiyo alisema umngoje amalize masomo sasa hivi ameanza drama zingine .

Akaendelea, sikia shem, watu mnapofunga ndoa miaka ya mwanzoni mnakomaa sana kujijenga kimaisha. Kama mna viwanja muanze kukomaa kujenga mnajibana hivyo hivyo mnakwenda. Sasa mtu ambaye anawaza kwao, kila kitu kwao, afanye maendeleo na familia yake kwanza ndio aangalie ndoa hamtafika popote. Hii hata kama mwanaume ana mawazo ya leo kwao, kesho kwao, kila kitu kwao hamtafanya lolote. Familia zipo tu na msaada kwa familia hauishi leo wala kesho. Inabidi mkomae mjiimarishe kwanza kisha ndio muangalie kuna nini kimesalia...ina maana ye' anawaza kuendeleza kwao huyo mtashauriana naye jambo gani sasa?

Akauliza, kwani huko kwao ni familia ya shida? Nikamjibu hapana. Familia ya kawaida tu si tajiri lakini sio masikini. Yeye mwenyewe, dada yake na mdogo wao wa mwisho mzee wao kamudu kuwasomesha private tangu shule za msingi na wanaishi vizuri tu. Na mama yake ni mjasiliamali pia ila ndio hivyo tu anataka kuonekana ni hero of the family. Akasema, atakupotezea muda huyo. Oa mwanamke mkae mpange mipango yenu mwanamke anayewaza kwao kila kitu na wakati yuko kwenye ndoa hamtafanya la maana. Ni miaka kadhaa imepita, lakini mpaka leo nayakumbuka maneno yake shemeji.

Siku moja nilijifanya kukomaa naye kuwa mi nataka kupeleka posa kwao la sivyo napiga chini. Alichonijibu....kama unaniacha kisa nimekataa ndoa ni sawa tu. Sipo tayari kwa kweli. Siwezi kukimbilia ndoa baadae inishinde. Nikamuuliza kinamshinda nini? Hana majibu.

Nikapiga chini kimya kimya. Hakugundua. Alikuja kushtuka hatuko kama zamani. Why this, why siku hizi uko kimya, why hivi mara vile. Sikumpa majibu yaliyoeleweka. Soon kidogo nikapata deal nikaenda Sierra Leon nikakaa miaka 2, akawa hanipati kwa simu ukawa ndio mwisho wetu.
Yan mzee stori ndio imeanza halaf na ww ndio umemaliza kuandika!?
 
So
TUENDELEE....

Lakini siku hizi simuoni pale, yuko wapi? Nikahoji. Mwanangu we, bint yangu yule ni mbishi sana. Alipata bwana mzungu alikua anampa hela akataka kujenga huku. Sisi tulimuambia pale nyumbani kuna eneo kubwa tu bado lina nafasi hizo pesa tungejenga pale angalau tungeona kafanya la maana. Sasa huku katupa hela na hakuna kitu. Lakini ajipange tu, atajenga hapa palipobaki. Nikachombeza. "Uwezo huo anao? Kazi pale kasimamishwa huu mwezi wa 3 sasa hivi na kila week anareport polisi. Amefanya nini? Nikauliza. "Kufanya kazi kwenye mazingira ya pesa ni hatari....inasemekana kuna upotevu wa pesa za mteja wao ulitokea na wao ndio watu waliokuwa wanahusika na hiyo account basi yeye na wenzie 3 hawana kazi sasa"
"Mzungu si bado yupo, atamsaidia" Nikasema. "Baba hilo lizungu hata halipo sasa hivi, sijui alimpa nini mwanangu mzee yule unajua alikua anataka kuacha kazi kabisa yaani" Poleni sana. "Asante baba ndio kuzaa huku, nawe kama una bint utakuja kujionea mwenyewe. Mi nikasema ni kuomba Mungu tu. Hawa mabint ni mtihani sana. Basi the meeting was adjourned, lakini mpaka hapa nikawa nishathibitisha tayari kuwa huyu ni mama mkwe.

Tukampa lift bi mkubwa njiani tukipiga story mbili tatu. Tulipofika Kigamboni pale uwanja wa Machava jirani kabisa na kwao akasema mi mnishushe hapa. Ni kweli kabisa ni pale pale nyumbani kwao x wangu.

Nasubiri nimsurprise siku ya kufanya business.

Kwa maelezo niliyoyapata kwa bi mkubwa, demu yuko vile vile kama nilivyomuacha.

Naisubiri Jumanne.
So surprise ni kumuonesha umeoa, pili wewe ndo mnunuzi wa Mali zake?
Dunia hiiiiiii.....
Anyway aliyataka mwenyewe ila pia ni mpango wa Mungu may be msingefika popote.
 
So
So surprise ni kumuonesha umeoa pili wewe ndo mnunuzi wa Mali zake?
Dunia hiiiiiii.....
Anyway aliyataka mwenyewe ila pia ni mpango wa Mungu may be msingefika popote.
Mamsapu wangu sijamuoa rasmi. Ni week ijayo tulikua tupeleke posa. Ila kuna jambo kubwa limetokea kwa upande wao kifamilia tumeahirisha till month end.
 
Mabinti wakishapata vihela kidogo wanajisahau kabisa, halafu kuna wale wana vikauli eti kuolewa siyo lazima sana. Teh huyu subiri jua lianze kuzama akifika 28-30 wenzake washawekwa ndani ye bado anasugua benchi ndio ataanza kuwakumbuka ma EX alowachezea.

Mwanamke fanya nyodo zite ila kuolewa kunakupa heshima usijekusema hutakuja kuolewa.
 
Back
Top Bottom