Ushauri wa Shemeji Yangu

Ushauri wa Shemeji Yangu

Sasa tuendelee....au tulale mpaka kesho?
 
Uhamiaji wamefika so amekimbia..
Hahaha mimi huyo Rais wenu haniwezi kwa purity ya uraia. Wakati wao inasemekana ni wahamiaji toka Urundi mimi mababu zangu ni waanzilishi wa mji fulani hapa Tz.
 
Endeleza basi mkuu
Hahaha mimi huyo Rais wenu haniwezi kwa purity ya uraia. Wakati wao inasemekana ni wahamiaji toka Urundi mimi mababu zangu ni waanzilishi wa mji fulani hapa Tz.
 
INAENDELEA.....

Basi mimi nikiwa zangu huko Sierra Leone wadau wangu waliokuwa wanamfahamu wakawa wananiambia yanayoendelea huku. Maana alikua anafanya kazi sehemu fulani ofisi ya public. Alikua akiuliza Meraki yuko wapi siku hizi, hata pale dukani kwake simuoni. Nilienda nikamkuta mama mmoja akadai yeye ni mama yake na Meraki akaniambia mwanawe amesafiri kidogo.

Ni kweli dukani kwangu nilimuacha mama yangu mzazi, uzuri hakumuambia exactly niko wapi. Na washkaji hawakumuweka wazi nilipo.

Kumbe akapata bwana mzungu, baada ya kuona mimi sina uelekeo naye tena. Mzungu alikuja huku kwa project ya miezi 3 na shirika moja la kimataifa. Ni mmarekani ila kituo chake cha kazi ni Thailand. Ndipo walipokutana na kuanza kudate.

Dada alianza kubadilika. Akawa mlevi sana inasemekana unga na shisha alikua anavuta. Akawa teja kabisa. Alikua na pesa sana akanunua viwanja double kule Kibada, 50x100 viwili na kuanza harakati za ujenzi. Kabla mambo yaive, mzungu akawa anarudi Thailand. Wakakubaliana waondoke wote.

Wazazi wakagoma. Hawezi kuondoka na mtu bila ndoa. Ndipo ikabidi mama yake amhoji, wakati unasoma mwanangu uliniambia kuna mtu anaitwa Meraki yuko wapi? Mbona ulikua ukinisimulia ni kijana mzuri tu....ikabidi atoboe siri Meraki hajui yuko wapi. Anahisi alishamwacha ndipo akaangukia mikono ya mzungu. Mama akagoma, akasema kwanza huyo mzungu ni mkristo na wala hajakuoa, na wala sisi hatumfahamu unawezaje kuondoka naye?

Ikabidi Mmarekani ajipeleke kwa wazazi wa binti kuwaaminisha. Haikufua dafu. Mzungu ikabidi aondoke, wabaki wanawasiliana tu. Uchumi wake ukarudi pale pale two squared kama zamani. Ila ulevi hakuacha na akapata mimba. Alinusurika kufa wakati wa kujifungua, alikimbizwa toka Amana mpaka Muhimbili ambapo alilazwa siku 17. Mtoto akakosa, Alhamdulillah alibaki salama.

Mwaka huu January nilinunua eneo kule Kibada. Juzikati hapo dalali yule akanipigia bwana kuna eneo jirani na uliponunua pale kwenye matofali kunauzwa. Nikamwambia mbona eneo kubwa sana lile ntaliweza? Akasema ni nusu yake inauzwa. Nikamwambia tuonane leo Jumapili.

Leo nikawasha kitoy changu na mamsapu pembeni tukaenda. Kufika nikamkuta dalali na mama mmoja. Haraka haraka nikamfananisha na x wangu lakini sikutilia maanani. Katika maongezi si ndio akasema eneo hili ni la bint yangu tukikubaliana atakuja kuweka saini. Machale yakanicheza. Ikanibidi nichokonoe. "Mama, bint yako ndio yule xxx (nikirefer anakofanya kazi). Ndio, kwani unamfahamu? Akajibu mama. Nikamwambia nimeona mnafanana, yule dada namfahamu. Mamsapu akanikata jicho.

ITAENDELEA.....
 
endeleza stori...

nasaha toka kwa jamaa yangu tena jana iyo

zipompa najua tumetoka familia duni ila pale wanapo pata shida ya laki 5 we wape 2.5 onesha kuchangia ila kukomaa kumaliza matatizo ya nyumbani bila kujijenga nawe kdg kdg itakugharimu mbeleni

hapo ni baada ya mke wake (mfanyakazi) kukomaa kulipa madeni ya mama yake kisiri huku akiwapiga tafu na wadogo zake kodi na matumizi mengine kisirisiri

mshahara wa shemu hauonekani kwa jamaa mpaka anajuta kuoa
 
Huyo demu ana miakili sana....kwanza unaweka kwenu fresh ndio unaangalia ndoa. Ndugu kwanza mke/mume baadae afterall anacho offer mume/mke ni kugegedana tuu hamna zaidi ya hilo ila mchuma janga ula na wakwao. Demu ana miakili hatari.
 
Huyo demu ana miakili sana....kwanza unaweka kwenu fresh ndio unaangalia ndoa. Ndugu kwanza mke/mume baadae afterall anacho offer mume/mke ni kugegedana tuu hamna zaidi ya hilo ila mchuma janga ula na wakwao. Demu ana miakili hatari.
Akili gani? Unajua kilichomtokea huko mbele?
 
TUENDELEE....

Lakini siku hizi simuoni pale, yuko wapi? Nikahoji. Mwanangu we, bint yangu yule ni mbishi sana. Alipata bwana mzungu alikua anampa hela akataka kujenga huku. Sisi tulimuambia pale nyumbani kuna eneo kubwa tu bado lina nafasi hizo pesa tungejenga pale angalau tungeona kafanya la maana. Sasa huku katupa hela na hakuna kitu. Lakini ajipange tu, atajenga hapa palipobaki. Nikachombeza. "Uwezo huo anao? Kazi pale kasimamishwa huu mwezi wa 3 sasa hivi na kila week anareport polisi. Amefanya nini? Nikauliza. "Kufanya kazi kwenye mazingira ya pesa ni hatari....inasemekana kuna upotevu wa pesa za mteja wao ulitokea na wao ndio watu waliokuwa wanahusika na hiyo account basi yeye na wenzie 3 hawana kazi sasa"
"Mzungu si bado yupo, atamsaidia" Nikasema. "Baba hilo lizungu hata halipo sasa hivi, sijui alimpa nini mwanangu mzee yule unajua alikua anataka kuacha kazi kabisa yaani" Poleni sana. "Asante baba ndio kuzaa huku, nawe kama una bint utakuja kujionea mwenyewe. Mi nikasema ni kuomba Mungu tu. Hawa mabint ni mtihani sana. Basi the meeting was adjourned, lakini mpaka hapa nikawa nishathibitisha tayari kuwa huyu ni mama mkwe.

Tukampa lift bi mkubwa njiani tukipiga story mbili tatu. Tulipofika Kigamboni pale uwanja wa Machava jirani kabisa na kwao akasema mi mnishushe hapa. Ni kweli kabisa ni pale pale nyumbani kwao x wangu.

Nasubiri nimsurprise siku ya kufanya business.

Kwa maelezo niliyoyapata kwa bi mkubwa, demu yuko vile vile kama nilivyomuacha.

Naisubiri Jumanne.
 
Hicho cha mbele ni independent event.
Nobody knows tomorrow brother. Angekubali nimuoe unajua ningekuwa naye wapi? Leo mi nna kwangu pakuishi, kitoy na several businesses. Ndoa ni baraka. Tena basi mwanamke anaombwa anakataa?

Tumezoea wanaume ndo tunaulizwa unanioa lini? Sio mdada unakataa mtu aliye tayari kwa ndoa kisa "ulipe fadhila za wazazi" nani kakuambia fadhila za wazazi zinalipwa?

Wazazi wafanyie wema tu, huwezi kuwalipa kamwe hata ufanye nini. Mwemye masikio na asikie.
 
Nobody knows tomorrow brother. Angekubali nimuoe unajua ningekuwa naye wapi? Leo mi nna kwangu pakuishi, kitoy na several businesses. Ndoa ni baraka. Tena basi mwanamke anaombwa anakataa?

Tumezoea wanaume ndo tunaulizwa unanioa lini? Sio mdada unakataa mtu aliye tayari kwa ndoa kisa "ulipe fadhila za wazazi" nani kakuambia fadhila za wazazi zinalipwa?

Wazazi wafanyie wema tu, huwezi kuwalipa kamwe hata ufanye nini. Mwemye masikio na asikie.
Wewe jamaa una akili sanaa...
 
Back
Top Bottom