Mkuu binafsi sijapuuza ni kweli kuna sehemu Malinyi ardhi ni 5000 Kwa ekari ila nilisikia ya hapo Mbingu ni ghari kidogo na kupata ni issue ila sehemu kubwa ya Malinyi ardhi bado ipo
Pia kwa habari ya mbegu za kuanzia ni kweli vituo vya utafiti wanazo, kama kile cha Minazi DSM ninakumbuka miaka kama 12 iliyopita walionyesha teknolojia ya kubeba mashina/ mbegu za migomba kwa mamia nani ya kichupa kidogo. Hivyo kwa wanaoenda kulima mbali wanaweza kupata mbegu na teknolojia hiyo ya kusafirisha mbegu toka kwao.
Tayari vijana wangu wako kazini, lazima nirudi na jibu la maana hapa jukwaani.
Ni kweli, ni gharama sana pale Mbingu, hata juzi nimeongea na bosi wa MOCOA kasema, kipande hapa Mbingu ni balaa. Hii vita simalizii jf hapa, naenda huko huko hata kama ni Chita.
Hata kama ni hafifu, ww nipe tu. Kama ratiba yangu itakaa vizuri mwaka huu nitatia mguu Mahenge.
Mkuu, naomba unielekeze vizuri zaidi kuhusu kilipo kituo hiki, pamoja na namba zao za simu kama unazo. Nataka kuwasiliana nao.
Asante.
Simu yao nilishafuta kitambo, ila ukiwa mwenge dar, fuata njia ya kwenda Coca Cola, mkono wako wa kuume mbele kidogo, uliza ofisi za mbegu bora za kilimo ( zamani ilijulikana sana kwa miembe/minazi bora).
Mkuu Chita kuna Kambi pale na Jeshi la wananchi na ni walimaji wazuri...... wasije wakakuwekea 'usiku' kuekeza...!!
Wale ni jkt sio jw, hawa tutashirikiana kukimbiza nguruwe pori mkuu. Wakiwa majirani zako usiwazuie kuficha pololo lao bandani kwako, ukiwazibia wanakubambika kesi !!!!!!!!!!!!!
Hapo kwenye red kaka umenikumbusha mbali, kumbe msamiati huo bado upo kwenye matumizi huko jakata. Nakuaminia kaka!
Mkuu, naomba unielekeze vizuri zaidi kuhusu kilipo kituo hiki, pamoja na namba zao za simu kama unazo. Nataka kuwasiliana nao.
Asante.
Waliokosa jakata bahati yao mbaya, kuna siku nikiwa poultry coy Ruvu, ilibidi nimeze mayai mawili mabichi fasta kufuta ushahidi !!!!!!!!
Kwii kwii kwiiii,....... siku hiyo pololo liligoma kaka, ilibidi mayai yakapasukie tumboni kama chatu, walahi umenikumbusha mbali! Nilimtaimu jamaa kombati yake alikuwa ameanika nilivokuja kuivaa niliitupa kubaini ilivyokuwa imejaa Chawa, chawa walikuwa wamepewa jina fulani nimelisahau....
haaa haaa haaaa
dah ... jkt kiboko
nilienda kuiba zabibu nyeupe pale kwenye shamba la zabibu makutupora jkt ... afande akatokea nilijidumbukiza kwenye shimo refu kutoka ikawa ishu, ikabidi nivue kombati nilichane chane ili kutengeneza kamba ya kupandia
Kule tulikuwa hatuibi, ila tulikuwa tunajifunza mbinu nzuri na mbaya za kuishi uraiani. Kwa hiyo baada ya jakata unachagua mbinu nzuri na zile mbaya unaziacha kule kule jakata.Kupitia jakata nilijifunza kula mihogo mibichi na viazi vitamu na hata hoho mbichi kumbe zinaliwa mbichi, hiyo ni jkt.I hope umesha acha wizi mkuu
Kule tulikuwa hatuibi, ila tulikuwa tunajifunza mbinu nzuri na mbaya za kuishi uraiani. Kwa hiyo baada ya jakata unachagua mbinu nzuri na zile mbaya unaziacha kule kule jakata.Kupitia jakata nilijifunza kula mihogo mibichi na viazi vitamu na hata hoho mbichi kumbe zinaliwa mbichi, hiyo ni jkt.
Nchi yetu ina mabonde mengi yafaayo kulima migomba na hatimaye tunaweza vuna ndizi, kuna nyika nzuri ambazo zikilimwa kwa kumwagilia tunaweza pata zao lingine la biashara. Zipo aina nyingi sana za migomba na hata hybrid zipo. Migomba ni annual plant, sina hakika sana kama ni binual. Mkungu mzuri pale mahakama ya ndizi Mabibo unafikia Tsh 20,000/ ( hii bei ni ya mwezi wa pili 2013, sijui leo), kule Mbingu mwezi huo huo ilikuwa ni Tsh 5000/ kwa wakulima.
Eka moja huoteshwa migomba kama 500 ikiwa spacing itakuwa 3m x 3m. Kama ukiwa na eka kumi za mgomba huko Mahenge/Kilosa utakuwa na migomba 5000, na kama utavuna mikungu 300 kwa mwezi utapata 1,500,000/ ukiwa shambani na ukapata 10,000,000/ kama utafikisha Mabibo. Hapa nazungumzia mshale/mzuzu.
Gharama za matunzo si kubwa, na magonjwa si mengi, zaidi sana ni maji na thinning ili kupata mazao bora, mbolea ni muhimu.
Najua kuna watalaamu wengi sana wa kilimo, mimi nimechokoza maada ili kwa pamoja tuishambulie na kutoka na kitu kizuri kwa faida yetu sote, kukiwa na kosa nisamehewe bure. Kwa sasa Wachina wanajenga daraja la mto Kilombero, twendeni Mahenge tukalime mgomba.