Ushauri wa Harusi ya gharama ndogo

Ushauri wa Harusi ya gharama ndogo

Nendeni kanisani au kwa shehe baada ya hapo mnasepa zenu hotelini. haki ya nani hata laki mbili hazifik
hahaha,..huo ndo mpango mzima,mengine ni mahangaiko na mahangaiko ya wanadamu.
 
Tafuta resort/hotel/baa yenye garden, kisha fanya yafuatayo...
1. Nunua nyama ya ng'ombe kilo 30 --- sh 180,000
2. Nunua bia/soda chupa 2 kila mtu --- sh 200,000
3. Nunua ndizi mzuzu --- sh 50,000
4. Nunua keki --- sh 100,000
5. Nunua shampeni chupa 10 --- sh 100,000
6. Tafuta mtu mwenye mziki --- sh 200,000
7. Kama huna rafiki mwenye v.camera, kodisha --- 200,000
8. Tafuta mchoma nyama na jiko na mkaa --- 70000

Jumla 1,000,000/=

Achana na mambo ya Mc, Tarumbeta wala mapambo. Usiweke jukwaa, viti visipangwe, itakuwa kama cocktail party... Kadi za mwaliko tengeneza mwenyewe, au fanya kwa sms... Marafiki zako uwataarifu kuwa mtu akifika ukumbini, kama anaweza achangie kununua kinywaji chochote..., kama ni chupa moja hya, kama ni kreti haya... Marafiki zako wataimba, watawarushia maua, watajenga tunnel kwa mikono yao nyie mtapita chini yake n.k, ili mradi itakuwa shamrashamra. Mtakata hiyo keki, na mtahakikisha mmewalisha wote, shampeni kumi zitafunguliwa na watu tofauti na zitaongeza shmrashamra, nyama za kuchoma na ndizi zitakuwepo mda wote jikoni, mtu anaenda kujichukulia anavyotaka, vinywaji vitasambazwa kwenye meza moja, mtu anajichukulia anavyotaka, ndugu jamaa na marafiki watakuwa na wasaa wa kuongea chochote wanachojisikia kuongea (kusiwe na formality), mtacheza sana mziki... nk...
Natamani ningekuwa na uwezo wa kukutumia mkanda wa arusi yangu ilivyokuwa simple, but ilipendeza...

laki si pesa
milioni si mtajii?
Harus ya milioni kweli au watu 100 tu mkuu?
Kama ni ivo sawa.
Na life ili la kidigital kila kitu bei juu
simple zipo but sio milion arusi kweli.
 
laki si pesa
milioni si mtajii?
Harus ya milioni kweli au watu 100 tu mkuu?
Kama ni ivo sawa.
Na life ili la kidigital kila kitu bei juu
simple zipo but sio milion arusi kweli.
Watu 40...
 
Kwanza mdogo wangu; hongera kwa hatua ulofikia ya kukubali kuungana na mwenzi wako kuwa mwili mmoja.
Ushauri wangu uko vipi;
Kwanza usikubali kufanya mambo ambayo yatakuingiza hasara na kukufanya uanze maisha mapya kwa kulipa madeni yasiyo ya lazima. Horodhesha marafiki zako wa karibu (naamini wanaweza kufika 40/50); Mwambie na mwenzako afanye hivyo hivyo; mtapata horodha ya watu wasiopungua 100. Kati ya hao mia waite 50 kwenye kikao kidogo na uwaeleze unataka kufanya nini; usikubali kupokea michango ya ufadhili kutoka pembeni; watumie marafiki zako wa karibu tu.

Mtakaa na kupanga bajeti ambayo nakushauri izingatie mambo yafuatayo:-
Tafuta hotel ambayo watakupa ukumbi free. Utafanikiwa kwa kufanya utafiti wa kwa siku mauzo yake ni Tshs. ngapi?
Hapo hapo hotelini kanunue kila kitu pale kwa bei mtakayokubaliana. Hotel nyingi siku hizi zina mziki mzuri tu; si wa kelele wala wa kuserebuka.
Gharama za usafiri kwa maharusi, mavazi n.k hizo mjigharimie wenyewe.
Ndani ya marafiki zako / mume wako - hapatakosa mtu anayeweza kuendesha sherehe ndogo hiyo.
Nakuhakikishia utatumia gharama kidogo na sherehe itafana sana; ila kumbuka baada ya harusi yenu utalaumiwa na wengi kwa kutokuwashirikisha kwenye sherehe hiyo. .
Ukitaka nikupatie bajeti ya kimahesabu niko tayari.

We jamaa kama sio prof basi ni docta!upo deep sana.
 
Kwanza nakupongeza kwa uamzi huo ulioufanya maana naelewa ni wewe ndo umekuwa chachu ya kufanya hivyo.
Mabinti wengi wa kisasa wanataka lisherehe likubwa la kutetemesha jiji eti kwa sababu ni tukio la mara moja na halijirudii bila kujua kuna nini baada ya sherehe.
Naamini hata ndoa yako ITAKUWA YA MAFANIKIO MAKUBWA SANA.
BIG UP.
MSALIMU SHEMEJI YANGU.
 
Hongera kwa kupata mwenza na hongera pia kwa kuamua kufanya sherehe ya gharama ndogo bila kusumbua watu na kadi za michango. Wacha na mimi nikupe uzoefu wangu kidogo ambapo tulifanya harusi ya kaka yetu kwa gharama kidogo na ikapendeza kuliko zote ambazo tulishawahi kufanya . Gharama zetu zilikuwa kama ifuatavyo:
Harusi ilifanyika desemba hapa DSM na waalikwa walikuwa 50
1. Ukumbi – Tulifanyia nyumbani kwa mzazi ambapo pana garden kubwa na nzuri
2. Video & Still picture – 300,000 (Nimemsahau jina yuko sinza picha bora kwelikweli)
3. MC + Muziki – 300,000 (tulikodi vyombo vya kanisani MC akaja na CD zake)
4. Mapambo +viti+meza+covers = 500,000 (tulimsomesha moja kutoka kwa wapambaji wenye majina)
5. Chakula – 500,000 (Caterer wa ukweli chakula cha kiwango)
6. Vinywaji(baridi +vikali) = 400,000 ( vikali- maduka ya jeshi, baridi maduka ya jumla)
7. Wahudumu – 5 @ 10,000 (tuliwaomba wahudumu wa hotel ya jirani waliokuwa off)
8. Kadi za Mwaliko – 70,000 (vivid Creations - mikocheni)
9. Mapambo bi harusi + maids+wazazi (Mpambaji alikuja home) – 150,000
10. Usafiri – magari binafsi ya familia
JUMLA = 2,350,000/=
(Bajeti yetu ilikuwa 2.5M (Maharusi walitoa 1M, wadogo wa bw. harusi 1.5M, pia maharusi na maids walijigharimia wenyewe mavazi)
 
ni vyema ungetoa pendekezo unataka kufanya harusi yenye gharama ndogo kwa kianzio cha Shilingi ngapi ili niweze kukupa bajeti yake na kisha unataka iwe na watu wangapi kwenye sherehe ukisema hivyo tutaweza kukushauri namna ya kufanya
Habarini za majukumu wana JF

Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya, jamani mimi ninakaribia kuolewa, ila kutokana na hali ya maisha tumekubaliana na mwenzangu tufanye harusi ya gharama ndogo.


Nimeamua kuomba ushauri wa jinsi ya kufanya sherehe hiyo kwa gharama ndogo sana, kwanzia mavazi mpaka chakula nisaidien wana jukwaa.


Karibuni.
 
ni PM nitakupa ushauri halafu mm nina huduma za kutengeneza keki kwa bei ndogo na kati, natengeneza kadi za harusi, ni mpambaji na vilevile ni MC hivyo waweza kuniPM nitakupa ushauri wa namna ya kufanya na nitawasiliana nawe usijali
Habarini za majukumu wana JF

Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya, jamani mimi ninakaribia kuolewa, ila kutokana na hali ya maisha tumekubaliana na mwenzangu tufanye harusi ya gharama ndogo.


Nimeamua kuomba ushauri wa jinsi ya kufanya sherehe hiyo kwa gharama ndogo sana, kwanzia mavazi mpaka chakula nisaidien wana jukwaa.


Karibuni.
 
Gharama kwenye ndoa/Harusi zinaweza kupungua kulingana na mazingira.kama unafanyia mjini gharama ni kubwa mno kuliko kijijini kwani kuna gharama ambazo zinaepukika kama ukumbi,n.k

Kwa ushauri tu ni kwamba gharama za harusi mjini ni kubwa kuliko za kijijni.
 
Ubarikiwe sana, Mungu akunyooshea njia zote za baraka kwako, umenisaidia sana kaka.
 
TUKO, naomba nione mkanda wako plz kama inawezekana, plz nimependa sana hii, natamani nam nifanye kama yako.
 
Habarini za majukumu wana JF

Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya, jamani mimi ninakaribia kuolewa, ila kutokana na hali ya maisha tumekubaliana na mwenzangu tufanye harusi ya gharama ndogo.


Nimeamua kuomba ushauri wa jinsi ya kufanya sherehe hiyo kwa gharama ndogo sana, kwanzia mavazi mpaka chakula nisaidien wana jukwaa.


Karibuni.
hatupati feedback
 
Mabadiliko si kwenye siasa tu hata kwenye kawaida,mawazo au mila na desturi zinazotuzunguka kama hili.Mleta maada na wachangiaji mmetoa elimu ambayo jamii inatakiwa ielewe na kuanza kuitekeleza ili kuleta ladha ya mabadiliko.
 
True Love Ushaolewa?Tupe Mrejesho Harusi ilikuwaje na gharama yake ilitumika sh. ngapi?
Maisha ya Ndoa After Harusi Matamu...
 
Kama unaishi mjini huwezi kuepuka gharama maana ndoa ni ya kwako na mwenza wako ila sherehe ni ya wazazi wenu,ndugu,jamaa na marafiki,huwa ikifika hapo ni vigumu sana kuepuka gharama ila kama utapunguza uwepo wa niliowataja hapo inawezekana ikapungua kidogo sana kitu ambacho hakiwezi kubadili unachokihitaji.

Kweli aisee,kuna ndugu yangu ustadh alikua anakataaa mambo ya kwenda kene hall na miziki basi familia yake ikasema poa we usije ila utake usitake itafanyika tu,yaani sijui kwann kwenye sherehe hua huna nguvu japo wewe ndo unaoa
 
Uzi wa kitambo ila ushauri wa Tuko nimeukubali sana, heshima yako mkuu
 
Last edited by a moderator:
Jana ndo nimeshuhudia ndoa ya gharama nafuu kabisa kuliko zote. Bwana/Bibi arusi waliingia kanisani kwenye ibada ya kawaida, ibada ikaanza. Ibada ikamalizika viapo etc Mchungaji akatangaza kuwa: Kwa mamlaka aliyopewa na kanisa na kwa mujibu wa sheria ya ndoa 1971, natangaza Bw/Bi.... Wamekuwa mme na mke. Jamaa waka sign certificates.... akatoka na mke wake na kuelekea nyumbani kwao. Nilipojaribu kufuatilia Bi Arus ana LLM ya sheria na ni Wakili na Bw Arusi ni MSc holder na ana kazi nzuri. Si kwamba hawana pesa... Ila wao wamesema MUNGU kwanza....
 
Back
Top Bottom