UWOGA=UMASKINI
JF-Expert Member
- Dec 30, 2013
- 2,400
- 1,017
I like it
Mkuu, andaa unataka kufanya sherehe ya watu wangapi, na una sh ngapi?Habarini za majukumu wana JF
Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya, jamani mimi ninakaribia kuolewa, ila kutokana na hali ya maisha tumekubaliana na mwenzangu tufanye harusi ya gharama ndogo.
Nimeamua kuomba ushauri wa jinsi ya kufanya sherehe hiyo kwa gharama ndogo sana, kwanzia mavazi mpaka chakula nisaidien wana jukwaa.
Karibuni.
watu wangapi?Mimi nataka kufanya sherehe ya tshs 1m tu.
Watu 20 tuwatu wangapi?
Huu uzi ni mwaka 2013 si ajabu hata wameshazaa watoto watatu. Angalia tarehe ya uzi umepostiwa lini.Mkuu, andaa unataka kufanya sherehe ya watu wangapi, na una sh ngapi?
Watu 20 , na ningependa nifanyie mahali popote kuanzia tabata Segerea kuja maeneo ya gongo la mboto mpaka chanika kama kuna garden au hotel nayoweza kuitumia kwa shughuli hiyo.watu wangapi?
Inatosha mbona, niliwah kufanya kama hiyo, basi ukumbi hautahitaji mapambo. Na hauna ndugu yako mwenye uwanja au garden nzuri ukafanyie kwake?, then chakula utafute mtu wa kawaida uumpe hela kama laki tatu anunue vitu akupigie menu ya maana.Watu 20 , na ningependa nifanyie mahali popote kuanzia tabata Segerea kuja maeneo ya gongo la mboto mpaka chanika kama kuna garden au hotel nayoweza kuitumia kwa shughuli hiyo.
Nafikiri nikipata Garden , au Resort yenye garden mimi nikanunua vyakula toka kwao ndiyo ingenipendeza zaidi , maana natumia mfuko wangu mwenyewe.Inatosha mbona, niliwah kufanya kama hiyo, basi ukumbi hautahitaji mapambo. Na hauna ndugu yako mwenye uwanja au garden nzuri ukafanyie kwake?, then chakula utafute mtu wa kawaida uumpe hela kama laki tatu anunue vitu akupigie menu ya maana.
SMAAAARTTTTTafuta resort/hotel/baa yenye garden, kisha fanya yafuatayo...
1. Nunua nyama ya ng'ombe kilo 30 --- sh 180,000
2. Nunua bia/soda chupa 2 kila mtu --- sh 200,000
3. Nunua ndizi mzuzu --- sh 50,000
4. Nunua keki --- sh 100,000
5. Nunua shampeni chupa 10 --- sh 100,000
6. Tafuta mtu mwenye mziki --- sh 200,000
7. Kama huna rafiki mwenye v.camera, kodisha --- 200,000
8. Tafuta mchoma nyama na jiko na mkaa --- 70000
Jumla 1,000,000/=
Achana na mambo ya Mc, Tarumbeta wala mapambo. Usiweke jukwaa, viti visipangwe, itakuwa kama cocktail party... Kadi za mwaliko tengeneza mwenyewe, au fanya kwa sms... Marafiki zako uwataarifu kuwa mtu akifika ukumbini, kama anaweza achangie kununua kinywaji chochote..., kama ni chupa moja hya, kama ni kreti haya... Marafiki zako wataimba, watawarushia maua, watajenga tunnel kwa mikono yao nyie mtapita chini yake n.k, ili mradi itakuwa shamrashamra. Mtakata hiyo keki, na mtahakikisha mmewalisha wote, shampeni kumi zitafunguliwa na watu tofauti na zitaongeza shmrashamra, nyama za kuchoma na ndizi zitakuwepo mda wote jikoni, mtu anaenda kujichukulia anavyotaka, vinywaji vitasambazwa kwenye meza moja, mtu anajichukulia anavyotaka, ndugu jamaa na marafiki watakuwa na wasaa wa kuongea chochote wanachojisikia kuongea (kusiwe na formality), mtacheza sana mziki... nk...
Natamani ningekuwa na uwezo wa kukutumia mkanda wa arusi yangu ilivyokuwa simple, but ilipendeza...
Andaa kama mil 3.5Okay, tulipanga iwe ya kwanzia M 1 - 2 sizidi hapo ikiwezekana ipungue M 2, tutatumia za amfukon kwa kias kikubwa kwan mpaka sasa tunaona zoez la michango halitofanikiwa.
Waalikwa wasizid 50, Music kidogo na MC kwa ajili ya kunogesha shughuli, tusisahau Camera man, Na Vidio Camera.
Karibu tena kiongozi
Truelove, nikutie moyo juu ya mpango wenu na mumeo mtarajiwa. Ni kwamba inawezekana sana tena vizuri mkafanya sherehe ndogo kwa macho lakini kubwa ndani ya mioyo yenu wewe na mumeo na wageni wenu wachache kama 40 au 50 tu hapo unawaalika wageni wa upande wa mume 25 na upande wa mke 20 na watano ni mpiga picha na nk.Habarini za majukumu wana JF
Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya, jamani mimi ninakaribia kuolewa, ila kutokana na hali ya maisha tumekubaliana na mwenzangu tufanye harusi ya gharama ndogo.
Nimeamua kuomba ushauri wa jinsi ya kufanya sherehe hiyo kwa gharama ndogo sana, kwanzia mavazi mpaka chakula nisaidien wana jukwaa.
Karibuni.
Huo ndo ujinga wa vijana wengi ulipo, maisha ni yako eti sherehe ni yandugu na marafiki, shubamitiiiii!!!! kwanini bwana harusi/bibi harusi uhangaike na michango? kiufupi swala la kuchangishana limeshapita na wakati, andaa sherehe kadri ya uwezo wako lakini fikiria na kesho yako pia. Unakuta umeajiliwa unalipwa mshahara 800k ila harusi unafanya ya zaidi ya Milioni 20 na hapo umepanga chumba kimoja, si ujinga huo.Kama unaishi mjini huwezi kuepuka gharama maana ndoa ni ya kwako na mwenza wako ila sherehe ni ya wazazi wenu,ndugu,jamaa na marafiki,huwa ikifika hapo ni vigumu sana kuepuka gharama ila kama utapunguza uwepo wa niliowataja hapo inawezekana ikapungua kidogo sana kitu ambacho hakiwezi kubadili unachokihitaji.
Tutor B unatumia kinywaji gani ukute unaendlea nakuja kulipa,safi sana aiseeKwanza mdogo wangu; hongera kwa hatua ulofikia ya kukubali kuungana na mwenzi wako kuwa mwili mmoja.
Ushauri wangu uko vipi;
Kwanza usikubali kufanya mambo ambayo yatakuingiza hasara na kukufanya uanze maisha mapya kwa kulipa madeni yasiyo ya lazima. Horodhesha marafiki zako wa karibu (naamini wanaweza kufika 40/50); Mwambie na mwenzako afanye hivyo hivyo; mtapata horodha ya watu wasiopungua 100. Kati ya hao mia waite 50 kwenye kikao kidogo na uwaeleze unataka kufanya nini; usikubali kupokea michango ya ufadhili kutoka pembeni; watumie marafiki zako wa karibu tu.
Mtakaa na kupanga bajeti ambayo nakushauri izingatie mambo yafuatayo:-
Tafuta hotel ambayo watakupa ukumbi free. Utafanikiwa kwa kufanya utafiti wa kwa siku mauzo yake ni Tshs. ngapi?
Hapo hapo hotelini kanunue kila kitu pale kwa bei mtakayokubaliana. Hotel nyingi siku hizi zina mziki mzuri tu; si wa kelele wala wa kuserebuka.
Gharama za usafiri kwa maharusi, mavazi n.k hizo mjigharimie wenyewe.
Ndani ya marafiki zako / mume wako - hapatakosa mtu anayeweza kuendesha sherehe ndogo hiyo.
Nakuhakikishia utatumia gharama kidogo na sherehe itafana sana; ila kumbuka baada ya harusi yenu utalaumiwa na wengi kwa kutokuwashirikisha kwenye sherehe hiyo. .
Ukitaka nikupatie bajeti ya kimahesabu niko tayari.