Tafuta resort/hotel/baa yenye garden, kisha fanya yafuatayo...
1. Nunua nyama ya ng'ombe kilo 30 --- sh 180,000
2. Nunua bia/soda chupa 2 kila mtu --- sh 200,000
3. Nunua ndizi mzuzu --- sh 50,000
4. Nunua keki --- sh 100,000
5. Nunua shampeni chupa 10 --- sh 100,000
6. Tafuta mtu mwenye mziki --- sh 200,000
7. Kama huna rafiki mwenye v.camera, kodisha --- 200,000
8. Tafuta mchoma nyama na jiko na mkaa --- 70000
Jumla 1,000,000/=
Achana na mambo ya Mc, Tarumbeta wala mapambo. Usiweke jukwaa, viti visipangwe, itakuwa kama cocktail party... Kadi za mwaliko tengeneza mwenyewe, au fanya kwa sms... Marafiki zako uwataarifu kuwa mtu akifika ukumbini, kama anaweza achangie kununua kinywaji chochote..., kama ni chupa moja hya, kama ni kreti haya... Marafiki zako wataimba, watawarushia maua, watajenga tunnel kwa mikono yao nyie mtapita chini yake n.k, ili mradi itakuwa shamrashamra. Mtakata hiyo keki, na mtahakikisha mmewalisha wote, shampeni kumi zitafunguliwa na watu tofauti na zitaongeza shmrashamra, nyama za kuchoma na ndizi zitakuwepo mda wote jikoni, mtu anaenda kujichukulia anavyotaka, vinywaji vitasambazwa kwenye meza moja, mtu anajichukulia anavyotaka, ndugu jamaa na marafiki watakuwa na wasaa wa kuongea chochote wanachojisikia kuongea (kusiwe na formality), mtacheza sana mziki... nk...
Natamani ningekuwa na uwezo wa kukutumia mkanda wa arusi yangu ilivyokuwa simple, but ilipendeza...