Ushauri wa Harusi ya gharama ndogo

Ushauri wa Harusi ya gharama ndogo

TrueLove

Senior Member
Joined
Jan 12, 2012
Posts
124
Reaction score
38
Habarini za majukumu wana JF

Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya, jamani mimi ninakaribia kuolewa, ila kutokana na hali ya maisha tumekubaliana na mwenzangu tufanye harusi ya gharama ndogo.

Nimeamua kuomba ushauri wa jinsi ya kufanya sherehe hiyo kwa gharama ndogo sana, kwanzia mavazi mpaka chakula nisaidien wana jukwaa.

Karibuni.
 
Labda kwa kuanza ni vizuri kuanalyse kwamba gharama ndogo unayoiongelea ni ipi?maana kuna
laki 1-5
mil 1-5
mil 10 etc
then go mlipanga kufanya sherehe ya aina gani
1. watu wachange michango
2.au kutumia mfuko wenu

waalikwa wawe wangapi?

ni dinner tu watu wale waondoke au hadi music,stedi show,na ma mc?
 
Kama unaishi mjini huwezi kuepuka gharama maana ndoa ni ya kwako na mwenza wako ila sherehe ni ya wazazi wenu,ndugu,jamaa na marafiki,huwa ikifika hapo ni vigumu sana kuepuka gharama ila kama utapunguza uwepo wa niliowataja hapo inawezekana ikapungua kidogo sana kitu ambacho hakiwezi kubadili unachokihitaji.
 
Ndoa ya gharama ndogo ni wewe mwenyewe kuamua idadi ya watu unaotaka na aina ya vinywaji utakavyotumia ikiwezekana ushirikishe watu wachache sana katika mchakato wa kufanya maamuzi ya nini kifanyike katika shughuli nzima. humu watu watakusaidia kupata wapishi wazuri wa bei nafuu, ukumbi mzuri na mambo mengine wakati wewe tayari umeshaamua unataka nini siku ya ndoa yako. Otherwise msome vizuri Chemwali
 
Last edited by a moderator:
Okay, tulipanga iwe ya kwanzia M 1 - 2 sizidi hapo ikiwezekana ipungue M 2, tutatumia za amfukon kwa kias kikubwa kwan mpaka sasa tunaona zoez la michango halitofanikiwa.

Waalikwa wasizid 50, Music kidogo na MC kwa ajili ya kunogesha shughuli, tusisahau Camera man, Na Vidio Camera.

Karibu tena kiongozi
 
Kwanza mdogo wangu; hongera kwa hatua ulofikia ya kukubali kuungana na mwenzi wako kuwa mwili mmoja.
Ushauri wangu uko vipi;
Kwanza usikubali kufanya mambo ambayo yatakuingiza hasara na kukufanya uanze maisha mapya kwa kulipa madeni yasiyo ya lazima. Horodhesha marafiki zako wa karibu (naamini wanaweza kufika 40/50); Mwambie na mwenzako afanye hivyo hivyo; mtapata horodha ya watu wasiopungua 100. Kati ya hao mia waite 50 kwenye kikao kidogo na uwaeleze unataka kufanya nini; usikubali kupokea michango ya ufadhili kutoka pembeni; watumie marafiki zako wa karibu tu.

Mtakaa na kupanga bajeti ambayo nakushauri izingatie mambo yafuatayo:-
Tafuta hotel ambayo watakupa ukumbi free. Utafanikiwa kwa kufanya utafiti wa kwa siku mauzo yake ni Tshs. ngapi?
Hapo hapo hotelini kanunue kila kitu pale kwa bei mtakayokubaliana. Hotel nyingi siku hizi zina mziki mzuri tu; si wa kelele wala wa kuserebuka.
Gharama za usafiri kwa maharusi, mavazi n.k hizo mjigharimie wenyewe.
Ndani ya marafiki zako / mume wako - hapatakosa mtu anayeweza kuendesha sherehe ndogo hiyo.
Nakuhakikishia utatumia gharama kidogo na sherehe itafana sana; ila kumbuka baada ya harusi yenu utalaumiwa na wengi kwa kutokuwashirikisha kwenye sherehe hiyo. .
Ukitaka nikupatie bajeti ya kimahesabu niko tayari.
 
Okay, tulipanga iwe ya kwanzia M 1 - 2 sizidi hapo ikiwezekana ipungue M 2, tutatumia za amfukon kwa kias kikubwa kwan mpaka sasa tunaona zoez la michango halitofanikiwa.

Waalikwa wasizid 50, Music kidogo na MC kwa ajili ya kunogesha shughuli, tusisahau Camera man, Na Vidio Camera.

Karibu tena kiongozi

mbona hiyo pesa kubwa sana mdogo wangu? Watanzania ni wa2 wa ajabu. Kwanza nambie uko mji gani?
 
Habarini za majukumu wana JF

Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya, jamani mimi ninakaribia kuolewa, ila kutokana na hali ya maisha tumekubaliana na mwenzangu tufanye harusi ya gharama ndogo.

Nimeamua kuomba ushauri wa jinsi ya kufanya sherehe hiyo kwa gharama ndogo sana, kwanzia mavazi mpaka chakula nisaidien wana jukwaa.

Karibuni.

hongera
 
Hahhahah, Camaha, kama nawe upo njia moja Hongera.
 
Tutor B, mm niko Mwanza, kumbuka hiyo pesa ni kwanzia mavazi kaka.
 
Mbona hao wengi sana, mie nafikiria kuwa na watu 20 tu. Nitawaalika dinner na kila kitu nitagharamia.
 
napita tu dear
mi najitolea kuwa maid nitanunua kila kitu changu mwenyewe
Okay, tulipanga iwe ya kwanzia M 1 - 2 sizidi hapo ikiwezekana ipungue M 2, tutatumia za amfukon kwa kias kikubwa kwan mpaka sasa tunaona zoez la michango halitofanikiwa.

Waalikwa wasizid 50, Music kidogo na MC kwa ajili ya kunogesha shughuli, tusisahau Camera man, Na Vidio Camera.

Karibu tena kiongozi
 
Tutor B, mm niko Mwanza, kumbuka hiyo pesa ni kwanzia mavazi kaka.

Mwanza life ni simple sana; hata mimi niko Mwanza; nitakupa hesabu ambazo zitakusaidia kufanikisha suala lako.
Nipe muda kidogo nikimbie Mahakamani kusikiliza kesi ya Diwani Matata
 
Tutor B, mm niko Mwanza, kumbuka hiyo pesa ni kwanzia mavazi kaka.

Kwa Mwanza hiyo ela mbona inatosha kabisa na kubaki maana kuna kumbi nzuri tu za mpaka laki moja na wapambaji wa kiaina wasio na complication, kikubwa ni kuchukua michango kwa rafiki zako wale ambao mnasaidiana katika shida na raha kama alivyokuambia TutorB pia angalia na baadhi ya ndugu tu wakukusaidia ila wawe waelewa maana ndugu ndio husababisha harusi ikaharibika wakati mwingine
 
Last edited by a moderator:
Kubwa kweli ila amesema hiyo ela ni kuanzia mavazi mpaka sherehe

Mavazi kitu gani kiongozi; tatizo wa2 wanapenda kuiga; then wanakuja kuingia kwenye madeni yasiyo ya lazima. Utaiga sawa watu watakuchangia lakini kwenye zawadi wanatoa 1000/= pesa yote iliyochangwa wanaitumbua wenyewe.
Vitu ambavyo si vya lazima kuvigharamikia ni:-
MC
Music
Picha mnato;
Video picture;
Vitu hivi vipo tu mitaani; watu tuna kamela zinatumika kwenye matukio mbali mbali na si kwa biashara; ikitokea mshkaji wangu akawa na shughuli nabeba namsaidia; gharama kidogo itakuja kwenye editing - J&B Graphics wanaedit video kwa gharama nzuri na kazi ni ya uhakika.
 
Habarini za majukumu wana JF

Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya, jamani mimi ninakaribia kuolewa, ila kutokana na hali ya maisha tumekubaliana na mwenzangu tufanye harusi ya gharama ndogo.

Nimeamua kuomba ushauri wa jinsi ya kufanya sherehe hiyo kwa gharama ndogo sana, kwanzia mavazi mpaka chakula nisaidien wana jukwaa.

Karibuni.

ndoa ya mkeka ndo haina gharama kubwa
 
Back
Top Bottom