Ushauri wa haraka, wazazi wamegoma kurudi kijijini

The Magnificent

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
2,694
1,247
ndugu zangu wana Jf,
kuna rafiki yangu yamemkuta ya mwaka!
Ameoa miezi mitatu ilopita na wazazi wake wakaja kwenye harus mjini pamoja na shangaz yake,baada ya harusi sasa huu ni mwezi wa3 hawana dalili ya kurudi nyumbani wote watatu,yaani baba,mama na shangazi.
Jamaa ni mwalimu wa sekondari ya serikali hapa jijini,imefika kipindi kuendesha maisha imekuwa kazi sana na ameajiriwa mwaka huu,january.
Amekaa na wazazi wake pamoja na shangaz yake na kujaribu kuwaelewesha jinsi maisha ya mjini yalivyo,na ukizingatia anaish kwenye vyumba vya kupanga.mkewe hana kazi,ni mama wa nyumbani,wazaz wamesema hawaondoki kurudi nyumban na kumshauri aende yeye kijijini akauze mashamba aje na pesa mjini waendelee kuishi,wameendelea kudai kuwa wamemsomesha kwa shida kwa kuuza pombe haramu ya gongo na kama wangekamatwa na polisi yeye asingeipata hiyo kazi,amejaribu kuongea na ndugu yke mwngne alieko morogoro ili waende kule angalau abaki mmoja,hakuna anaetaka kutoka dar,rafiki yangu sasa maisha yanaelekea kumshinda na ameshakopa sana hadi anatia huruma.
Kilichobaki anaomba angalau msiba utokee huko nyumbani pengine wanaweza kurudi nyumbani.
Wakuu,ushauri wenu ni muhimu sana hapa,

nawasilisha!
 
Hapa kazi ipo,kwanza inaonekana wazazi wake hawana busara. Na ili tatizo kuna watu bado wanaliendekeza,wakidhani kuwa walivyoishi wao,ndivyo hata vijana wao wataishi hivyo.
Mimi ningemshauri jamaa atafute mtu mzima mwenye hekima hususani ndugu yake au mtu wa karibu na familia. Ili kwa pamoja waweze kuzungumza na hao wazazi wake. Ila na kumwomba Mungu wakati anajaribu kutimiza azma yake ya kuwarudisha kijijini ni Muhimu.
 
nitafikisha ujumbe mkuu,thanx
 
Ukidanganya usiwe msahaulifu
kuna sehemu umesema SHANGAZI YANGU that means ni wewe
Ushauri waombe watu wazima esp wazee wakusaidie kuwa-convince itasaidia
 
Hapo kuna kazi, ngoja nipumzike kidogo. Nitarudi nikupe ushauri.
 
hapa inabidi avae sura ya nyani.mbuzi hula kutokana na urefu wa kamba yake.wakilala njaa siku mbili hawatakaa hao.kwa sababu wanamkomoa na yeye awakomoe tu coz dawa ya moto ni moto.mia
 
hapa inabidi avae sura ya nyani.mbuzi hula kutokana na urefu wa kamba yake.wakilala njaa siku mbili hawatakaa hao.kwa sababu wanamkomoa na yeye awakomoe tu coz dawa ya moto ni moto.mia

duuh! Mkuu wewe unaweza kuwafanyia hayo wazazi wako waliokuzaa na kukulea kwa tabu?
 
Si useme tu kama ni wewe, mara shangazi yangu mara useme shangazi yake.....haya pole Mpwa
 
Duh! hii imekaa kidenja denja yaani. Baba na mama tayari ni mtihani. alafu na shangazi tena?
Mshauri aendelee kuongea nao, na kama walivo sema wengine atafute wazee watakao waelewesha.
Kwa upandemngine usitupilii kabisa lile wazo la mashamba, jaribu kuwaambia utauza mashamba, waje na wenyewe watafute nafasi dar na waishi kwa hela ya shamba hizo. labda wakielewa kua shamba ziko hatarini na warealize itawabidi kusurvive wenyewe wanaweza kufikiria tena...
Kuhusu shangazi jaribu kuongea na watoto wake. usichukulie problem yote kama ni moja, break it into pieces and solve it one at a time.
 
ujumbe umefika mkulu.
 
ila pia wazazi wametoa hoja za msingi..kwani wanadai waliuza pombe haramu gongo kwa ajili yake, alafu yeye anaendelea kula chips yai,baga,saradi na soseji wao wakila maboga na makungu huko kwao.tena nenda kawashauri wang'ang'anie hadi mwisho kama Gaddafi.
 
utakuwa haupo serious naamini.
 
Atafute watu wazima wa umri wa wazazi hao wamsaidie. Viongozi wa dini pia anaweza watumia .
Pia akae nao wapange namna atakavyowasaidia wakiwa huko bush ili wajisikie wanaishi maisha ya kistaarabu, sio kuuza piwa.
 
utakuwa haupo serious naamini.

no niko serious,we unaona ni haki wao waende kijijini yeye abaki? Tena ana kiajira ata kama fedha kidogo..lazima awe mkubwa sio analialia na kutaka waende..angeonekana wa maana kama akifanya mpango wa kumpeleka shangazi kijijini sio mama.tena ni inasikitisha sana pindi mama anafanyiwa hivo,wakati kipindi hicho wanajikopakopa kukupeleka shule unavaa kaptula zimetoboka leo unajifanya unajua saana kung'aa na kuwasaau wazazi.hao wazazi kwa vyovyote vile wamempima kijana wao na kugundua bila mbinu gyo kijana wao atawatosa.
 
hili suala la kubebeshana mizigo hata isiyo ya lazima ndiyo linaloturudisha nyuma kimaendeleo, Maisha ya mjini na kijijini ni tofauti kabisa , mjini mtu unakuwa na stress nyingi sana. kinachogomba hapa huenda wazazi wanadhania kwamba mjini kila mtu ana maisha mazuri, hivyo nao wanataka wastarehe kwa kupitia mgongo wa mtoto wao, Cha muhimu huyo jamaa atafute watu wenye heshima zao wanaoyajua maisha ya mjini ili wazazi waweze kupewa ushauri, kama ni kutoa msaada anaweza kuwasaidia wakiwa hukohuko kijijini.
 
Duh! Kuna wazazi hawana huruma jamani. Mmh! Kama amepanga vyumba vingi avirudishe vyote abaki na kimoja. Hao wazee wakikosa pa kulala akili itawakaa sawa.
 
Back
Top Bottom