Husninyo
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 23,724
- 9,188
Dah!:shock:
toa ushauri hapa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah!:shock:
toa ushauri hapa.
Ingekuwa rahisi ningefanya hivyo Husninyo. Hao ni Wazazi ambao ni Mungu wa Dunia huwezi kuwafukuza na jamaa ndio kwanza anayaanza maisha mfuko wake yeye na mkewe nanga inapaa sasa imagine kwenda kuongezewa tena matumbo mengine matatu tena katika nyumba ya kupanga!!! Gumu sana hili Husninyo, jamaa anaweza kuchanganyikiwa.
ni gumu ndio ila inapobidi bora mtu uwe na roho mbaya BAK hata kwa muda mfupi vinginevyo utashangaa hausongi mbele kimaisha. Au inawezekana huyu jamaa huwa hawasaidii wazee wake huko kijijini ndio maana wameamua kung'ang'ania mjini.
....Tukitilia maanani kwamba ndio ameanza kazi January 2011, basi inaelekea huko nyuma alikuwa hana uwezo wa kuwasaidia Wazazi wake....Ni kweli wakati mwingine inabidi kuwa na roho mbaya, lakini kuwafukuza Wazazi nyumbani kwako ni ngumu sana tena sana.
BAK kuna namna ya kuishi na watu hata kama haumpi msaada wa kifedha anakuwa anakubali uwepo wako na kuelewa hali yako ya kiuchumi ipo vipi. Jamaa kama hakuwa na msaada wa kifedha hapo nyuma, vipi msaada wa kimawazo? Vipi ushiriki wake yeye huko kijijini kwa matukio kama ya misiba? Vipi mawasiliano na wazazi wake yalikuwaje? Mi naamini wazazi ni waelewa sana ila jamaa atakuwa alitengeneza mazingira ya kuonekana ana kauwezo huku mdomoni anasema hana kitu.
Inawezekana amepata hiyo kazi ya kuajiriwa mwaka huu ila hapo nyuma alikuwa anaweza kuingiza japo kipato kidogo kwa shughuli zingine ila alishindwa kusaidia wazazi wake hata kwa hicho kidogo alichokuwa anapata.
mjali rafiki yako zaidi wakati wa shida. Ukiona mtu mpaka amekueleza mambo yake ujue ni namna gani ameona wewe waweza japo kumfariji. Wengi hufa nayo moyoni. Mpe pole jamaa.Nimeamua kukata mguu pale kwa jamaa make anatia huruma,,
mjali rafiki yako zaidi wakati wa shida. Ukiona mtu mpaka amekueleza mambo yake ujue ni namna gani ameona wewe waweza japo kumfariji. Wengi hufa nayo moyoni. Mpe pole jamaa.
mkuu,jamaa kanidokeza muda mfupi ulopita kwamba siku hzi ndo hawataki hata tv izimwe,hta umeme ukikatika hawaelewi wenyewe wanaamini ni hujuma ya mke wa jamaa ili wasiangalie tv.
Ukifuatilia stori za wale wazee unaweza jikuta mbavu huna,mengi nimeyashudia pale kwa jicho langu!
Nimeamua kukata mguu pale kwa jamaa make anatia huruma,sijui hata hao wanafunzi anawafundishaje,
Duh!! Kazi ipo, yaani hapa sijui ndo unafanyaje jamani!! Huyo shangazi mtu ye hana watoto hata waje kumchukua?
mkuu,jamaa kanidokeza muda mfupi ulopita kwamba siku hzi ndo hawataki hata tv izimwe,hta umeme ukikatika hawaelewi wenyewe wanaamini ni hujuma ya mke wa jamaa ili wasiangalie tv.
Ukifuatilia stori za wale wazee unaweza jikuta mbavu huna,mengi nimeyashudia pale kwa jicho langu!
Nimeamua kukata mguu pale kwa jamaa make anatia huruma,sijui hata hao wanafunzi anawafundishaje,
we wacheka wakati mwenzio anapata tabu? toa ushahuri hapa tuone kama watakubali kurudi!kanumba apewe hii kwa kweli...lol
Hapo sasa ndipo unachukulia nafasi ya kuwasoma na kujua ni vitu gani vinawakera hasa. Kama ni kukosa TV anaipoteza kabisa. Si ni kwa muda tu? Akupe umwekee alafu awaambie alikosa hela ya chakula imebidi auze.mkuu,jamaa kanidokeza muda mfupi ulopita kwamba siku hzi ndo hawataki hata tv izimwe,hta umeme ukikatika hawaelewi wenyewe wanaamini ni hujuma ya mke wa jamaa ili wasiangalie tv.
Usiseme kwa jicho lako, haipendezi. sema tu ulijionea mwenyewe. alafu hivi vitu sio vyakucheka, rafiki yako ana stress huyo!Ukifuatilia stori za wale wazee unaweza jikuta mbavu huna,mengi nimeyashudia pale kwa jicho langu!
Nimeamua kukata mguu pale kwa jamaa make anatia huruma,sijui hata hao wanafunzi anawafundishaje,
Ukidanganya usiwe msahaulifu
kuna sehemu umesema SHANGAZI YANGU that means ni wewe
Ushauri waombe watu wazima esp wazee wakusaidie kuwa-convince itasaidia
wengi wanazuga hivi hivi mara hoo lafiki yangu hana nguvu za kiume..mara kafumaniwa,mara kakaangu anapenda tigo.eti tumshauri..