Ushauri wa haraka na Dharura wadau

Mapato55

Member
Feb 7, 2015
12
7
Mimi ni kijana na hadi leo nimetazama nakala ya Cheti changu cha kuzaliwa nitatimiza miaka 31 mapema mwezi March lakini jambo la kushangaza mipango yangu inazunguka nainuka kwa muda kisha narudi tena kuanza moja maisha yangu hayaendi mbele.

Ipo hivi.

Nilihitimu Chuo cha Mafunzo ya ualimu kwa ngazi ya Cheti Msingi 2013 na kuanza ujasiriamali kwa ndugu yangu kwa miezi kadhaa kisha nikapata ajira serikalini 2014 na mwaka 2015 nikatoka Serikalini kwa matatizo yaliyokuwa nje ya uwezo wangu hapo ndipo taabu ilipoanzia, nilianza biashara ambayo awali ilienda vizuri lakini mapema mwaka 2016 ilipata changamoto hivyo nikaamua kuachana nayo na kuanza kufuatilia kurudi kwenye kazi ya serikali ijapo sikufanikiwa lakini sikukata tamaa sasa mapema mwaka 2018 nilipata ajira kwenye shule binafsi nikafundisha kwa muda na mwaka 2019 nikaomba tena ajira Serikalini na kupangiwa kituo cha kazi kwenye halmashauri tofauti na ile ya awali hivyo huko sikuambulia chochote zaidi ya kupoteza raslimali na Muda wangu.

Maana hapo nilipambana na kumsihi HR aniombee kibali cha kuendelea kutumia check na kwa Katibu Mkuu Utumishi na alikubali japo bado naendelea kufuatilia lakini bado ninapambana na mishe za kitaa nazo ndiyo hivyo nikizichanga kiasi zinaibuka changamoto zilizo juu ya uwezo wangu napoteza kila senti ninaanza moja

Uzoefu wa kazi nilizonazo Kufundisha S/Msingi (ENGLISH MEDIUM) /Utaalamu wa masuala ya Teknolojia /Utafiti wa Madini/Usimamizi wa Biashara.

Maana kwa Tathimini yangu Binafsi hasara niliyokwisha kuiapata sasa inafikia Tsh M 35,000,856.00/= hiii ni kwa mujibu wa mapato Ghafi kama ifuatavyo.

Kushughulikia kurejeshwa kwenye utumishi wa umma Safari za kutoka huku niko TO Dodoma 7 Trips Accurate TSH 240,000/= ambayo ni sawa na Tsh 1,680,000.00/= na Kuhama kutoka kituo binafsi kwenda kituo kipya na kutoka kituo kipya kurudi mtaani kupambana Tsh 2,470,000.00/= sasa Niliwekeza kilimo ijapo nilipanda matunda na miche ya mbao 2016 na 2017 ukame ulipukutisha amost Tsh.20,000,000.00/=

Hali hii inanitesa sana maana kila nikipata mchongo nikipanga kuanza jambo fulani kunaibuka tatizo mpango ninaokuwa nimeupanga unakutana na kikwazo hivyo niapoteza muda na fedha ninayo kuwa nimakusanya sioni maendeleo yoyote ya maana , kuna wakati nahisi kuchanganyikiwa japo mimi kwa asili ni jasiri sana ila kwa tathimini yangu naona hapa kama kwa fikra na mawazo yangu hayawezi kunikomboa wadau naomba sana ushauri wenu je nifanye nini hasa?

Hadi muda huu nina hofu na wasiwasi kuu sina pa kuanzia sioni nuru ni giza totoro.
 
Bila "friction" hakuna "motion"....kukwama na kuvuka vikwazo ni shule tosha y kujenga.
Ukianguka Simama jipanguse songa mbele.
 
Wewe hujashawishika na wazee wa Forever Living ukaacha kazi yako ya kwanza?
Tupe sababu ya kuacha kazi yako ya kwanza ili tujue tukusaidieje
 
Mimi ni kijana na hadi leo nimetazama nakala ya Cheti changu cha kuzaliwa nitatimiza miaka 31 mapema mwezi March lakini jambo la kushangaza mipango yangu inazunguka nainuka kwa muda kisha narudi tena kuanza moja maisha yangu hayaendi mbele.

Ipo hivi.

Nilihitimu Chuo cha Mafunzo ya ualimu kwa ngazi ya Cheti Msingi 2013 na kuanza ujasiriamali kwa ndugu yangu kwa miezi kadhaa kisha nikapata ajira serikalini 2014 na mwaka 2015 nikatoka Serikalini kwa matatizo yaliyokuwa nje ya uwezo wangu hapo ndipo taabu ilipoanzia, nilianza biashara ambayo awali ilienda vizuri lakini mapema mwaka 2016 ilipata changamoto hivyo nikaamua kuachana nayo na kuanza kufuatilia kurudi kwenye kazi ya serikali ijapo sikufanikiwa lakini sikukata tamaa sasa mapema mwaka 2018 nilipata ajira kwenye shule binafsi nikafundisha kwa muda na mwaka 2019 nikaomba tena ajira Serikalini na kupangiwa kituo cha kazi kwenye halmashauri tofauti na ile ya awali hivyo huko sikuambulia chochote zaidi ya kupoteza raslimali na Muda wangu.

Maana hapo nilipambana na kumsihi HR aniombee kibali cha kuendelea kutumia check na kwa Katibu Mkuu Utumishi na alikubali japo bado naendelea kufuatilia lakini bado ninapambana na mishe za kitaa nazo ndiyo hivyo nikizichanga kiasi zinaibuka changamoto zilizo juu ya uwezo wangu napoteza kila senti ninaanza moja

Uzoefu wa kazi nilizonazo Kufundisha S/Msingi (ENGLISH MEDIUM) /Utaalamu wa masuala ya Teknolojia /Utafiti wa Madini/Usimamizi wa Biashara.

Maana kwa Tathimini yangu Binafsi hasara niliyokwisha kuiapata sasa inafikia Tsh M 35,000,856.00/= hiii ni kwa mujibu wa mapato Ghafi kama ifuatavyo.

Kushughulikia kurejeshwa kwenye utumishi wa umma Safari za kutoka huku niko TO Dodoma 7 Trips Accurate TSH 240,000/= ambayo ni sawa na Tsh 1,680,000.00/= na Kuhama kutoka kituo binafsi kwenda kituo kipya na kutoka kituo kipya kurudi mtaani kupambana Tsh 2,470,000.00/= sasa Niliwekeza kilimo ijapo nilipanda matunda na miche ya mbao 2016 na 2017 ukame ulipukutisha amost Tsh.20,000,000.00/=

Hali hii inanitesa sana maana kila nikipata mchongo nikipanga kuanza jambo fulani kunaibuka tatizo mpango ninaokuwa nimeupanga unakutana na kikwazo hivyo niapoteza muda na fedha ninayo kuwa nimakusanya sioni maendeleo yoyote ya maana , kuna wakati nahisi kuchanganyikiwa japo mimi kwa asili ni jasiri sana ila kwa tathimini yangu naona hapa kama kwa fikra na mawazo yangu hayawezi kunikomboa wadau naomba sana ushauri wenu je nifanye nini hasa?

Hadi muda huu nina hofu na wasiwasi kuu sina pa kuanzia sioni nuru ni giza totoro.
Mkuu naomba Kama hutojari nipigie tupige soga ww tunaendana vitu vingi

Mimi mwenyewe ni mwalimu nimeacha kazi baada ya kuona malipo hayaendani na mazingira niliyokuwapo Ila nilikuwa na mtaji wa Kama 10m ukapukutikia kwenye kilimo saivi nimekuwa nikiipambana Ila najikuta narudi Tena ground lakini sikati tamaa , matumaini nayaona mbele na hio Hali unayopitia nimewahi pitia na naipitia ukizingatia Mimi na watu wa nyumbani Sina sapoti yoyote so napambana navojua na kitu kingine clue nyingi za marafiki naopata naona hawana future kama niliyonayo na mm hivohivo kupoteza 500k kwa mwezi ni kawaida Ila ningepata mtu mwenye Nia ya dhati kutoboa ajira hazina maana yoyote
 
Kwanini ukiacha kazi ya ualimu na Sasa hivi unarudi Tena kwa kuhonga na kupiga magoti .....unakula matapishi yako si ndio .....

Hapo tatizo ni kupata check number ,Hilo swala litakuchukua muda Sana ndugu ,najua mlolongo wake si wa kitoto hasa nyie mlioacha kazi na kurudi Tena ....

Mwisho kabisa ,acha kunyongonyea ,pambana ,maisha yakikuchapa ngumu wewe yachape teke ,yakisogeza kete wewe sogezi nyingine hakuna ,yakirusha ngumu wewe unarusha nyingine ...hakuna kuwa mnyonge kwenye hii nchi qa wazurumati na wahuni ....
 
Umeandika speed speed nmeshinda kukuelewa,

Sahv uko KAZIni, umeachishwa KAZI au ikoje?
 
Tatizo lako ni kutaka mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi. Wenzako tulijitahidi kuwa na subira, na hata sasa matunda tunayaona! Ingawa siyo ya kushangaza kivile.
 
Back
Top Bottom