Ushauri wa bure: Usioe career woman!

Ushauri wa bure: Usioe career woman!

Insecurity imekujaa, wacha wanaume wa ukweli waoe zao carrier women, hujui hata mtoto kua na akili mara nyingi sana anarithi kwa mama? nyie ndo mnaorudisha nchi nyuma.
Carrier woman mwingine huyu hapa na mihemuko yake. Taratibu mama naona hyo akili unayotambia hata huna, maana umeshindwa kungamua na kutafakari mambo, kama kweli sisi wa mawazo haya ndo tunarudisha nchi nyuma unaweza kueleza ni vipi Dubai na Quatar ni miongoni mwa nchi tajiri huku wanawake wanawake wakiwa hawafanyi kazi ukilinganisha na Uganda yenye sera ya 50 kwa 50 tangu miaka ya 1990 ikiwa nchi ya kwanza kua na makamu wa raisi mwanamke na bunge lililojaa wabunge wanawake lakini ni miongoni mwa nchi masikini kabisa ?!!
 
Aiseee..kwa hyo mnanishaur nimpige chini PHD wangu maana baadae nikimuoa atanishinda???
Aise kimbia unavyoweza, huyo hafai hata punje mkuu ukioa usinipe card sichangii ndoa nazojua zitavunjika
 
SIO KWELI. Mke wangu hana kazi ila anafuraha tele na ninampenda na kumtunza vema. Tafiti zinaonyesha pia kua wanawake wanaofanya kazi za kuajirima huku pia wameolewa wanaongoza kwa misongo ya mawazo kuliko wanawake waliolewa bila kua na ajira.

hiyo nadharia haipo mkuu.hakuna wanawake waliojaa msongo wa mawazo kama wanawake magoalkeeper.
wewe kama kwel wamjali na kumpenda mkeo goalkeeper basi nikupe pongezi sana
 
Pia naona angalau ukitaka kumuoa career lady basi awe hana mvuto,dizain hiyo huwa hawasumbui sana
 
Aise kimbia unavyoweza, huyo hafai hata punje mkuu ukioa usinipe card sichangii ndoa nazojua zitavunjika
Ila ni wife materials aiseee..na kananisikiliza kwa kila kitu..yaan kifupi hafanyi jambo lolote mpaka nimuambie afanye...
 
SIO KWELI. Mke wangu hana kazi ila anafuraha tele na ninampenda na kumtunza vema. Tafiti zinaonyesha pia kua wanawake wanaofanya kazi za kuajirima huku pia wameolewa wanaongoza kwa misongo ya mawazo kuliko wanawake waliolewa bila kua na ajira.
Yaani kweli unajivunia kuwa na mke asiye na kazi? Kama ulivyoanisha hapo juu....On a serious note....!!!
 
ni kutojitambua ndio kunafanya career zao zianze kuwayumbisha akili...otherwise sio wote wachache sana wanajielewa hata kama ni Phd Holder ndani anakuwa mke na mama bora
 
Me nadhani kiburi na dharau kwa mwanamke ni hulka binafsi ya mtu. It has nothing to do with wether the woman has a career or not. Maana hata sisi wanaume tupo wenye kazi na mishahara mizuri ila bado tunakwepa majukumu ya nyumbani.
 
Yes wapo. Hapa ninapofanya kazi wapo ni tena wakali kimvuto. Ni wasomi yes lakin wanaelewa nafasi zao majumbani kwao na wako responsible kwa waume zao.

Once again kama ulivyosema hawa ni rare breed. Waliobak wanakuwa wapole kipindi hawana kazi, ngoja wapate kazi ndio utaelewa
unasema vip wanaelewa nafasi zao kirahisi hivyo wewe unajua nyumba yao na mumewe wanaishi vip
 
Acha woga. Mbona tumeoa wafanyakazi na tuko poa tu mkuu. Sasa ndo kutuambia wauguzi, madaktari, mahakimu, waalimu na wengineo woote unaoenda kyomba huduma maofisini kwao wasiolewe kisa wewe una hofu na kuonyesha uanamme wako?
Hili ni jambo la ajabu kabisa.
Tuaisomeshe watoto au waliosoma wasifanye kazi?
Nisikuone karibu na binti yangu maana ntakufanya kitu mbayaaa we jamaa.
 
unasema vip wanaelewa nafasi zao kirahisi hivyo wewe unajua nyumba yao na mumewe wanaishi vip
Mwanamke anaejiheshimu sikuzote utamuona mienendo yake, ongea yake hata anavyoishi na jamii. Anavyoshirikiana na wafanya kazi wenzie unaona..
Haya mambo yako wazi kabisa. Hata kitabia utaona. Anaish vip na mumewe hilo sifaham kiundan ila huwa tuna utaratib wa family day.. waume zao ni washkaj zetu sana tu so tunabonga vitu kibao. Kama kungekuwa na dosar tungeshasikia vurugu mechi siku nyingi au miendenendo yake ingejulikana tu kuwa yukoje
 
Hii mada haina mashiko kila mmoja asimamie anachoona ni sahihi kwake.
 
Yaani kweli unajivunia kuwa na mke asiye na kazi? Kama ulivyoanisha hapo juu....On a serious note....!!!
Ndio, ulitaka nihubiri mambo nisiyoishi kwayo ?! Na ngoja nikwambie kitu, mke wangu hajawahi kulia kwa sababu yoyote ile maana swez kuruhusu majanzo YOYOTE yamfikie. Na hilo linamfanya aniheshimu kwa moyo wake wote.
 
Naomba tukubaliane kutokukubaliana.
Kila mmoja huwa ana ndoto zake au kuna aina ya maisha ambayo hupanga kuyaishi. Kila uchwao ni mapambano ya kufikia ndoto/maono uliyojipangia.

Kuoa/kuolewa ni sawa na kuwekeza au kununua hisa kwenye soko la hisa. Kuna mengi ya kuyatafaki kabla ya kuchukua uamuzi.
 
NAJIULIZA HIVI UNAONGEA YOTE HAYO UNAMTOTO WA KIKE KWELI WEWE!! MWANAO UNAMPANGO WA KUMSOMESHA HAMA LA!!! ME NADHANI USIMSOMESHE HATA DARASA MOJA ILI ASIJE AKASUMBUA WATU BAADAE.. HAKUNA KITU KABISAA
 
Back
Top Bottom