Ushauri wa Bure: TBC na Mkurugenzi TBC (TBC1). | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa Bure: TBC na Mkurugenzi TBC (TBC1).

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Radio Producer, Jun 16, 2011.

 1. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Heshima mbele wakuu,

  Kwenu TBC na Mkurugenzi TBC.

  Kwanza kabisa, mimi Radio Producer nawapa pole kwa majukumu mengi na magumu mnayoyapitia katika suala zima la kuifanya TBc isonge mbele. Kiukweli mimi napenda sana kutoa ushauri kwenye media houses mbali mbali. Natoa ushauri kuhusu programming, production, follow-up na mengine! Kwa elimu niliyonayo nimeona ninaweza kuwashauri au kutoa maoni yangu kwa TBC. Kama ninavyoelewa umuhimu wa FEEDBACK katika fani hii nina imani pia kuwa mtayapokea maoni na ushauri wangu! Hapa chini ndiyo ushauri wangu ulivyokaa:-

  1. Programming
  Ukweli ni kwamba mna vipindi vingi sasa na ni vizuri sana na vinasaidia sana. Nikifuatilia kote kote TBC1, TBC Taifa, TBC fm hata TBC2 ukweli mnajitahidi sana katika suala la vipindi kwa ujumla. Vipindi vyenu vina heshima, vinajali kanuni zote za uaandaaji wa vipindi na kwamba vinaweza kuangaliwa na watu wa umri tofauti tofauti.
  Tatizo au changamoto mliyonayo kwenye programming iko upande wa NEWS.
  Mnakosa kitu BALANCE, kiukweli hapa mna matatizo makubwa sana. Kwasasa hamfuati kabisa kanuni za uandishi wa habari ila mmejiingiza kwenye siasa. Hata habari zenu zote zimekuwa za kisiasa siasa tu! Juzi juzi nilikuwa naongea na moja ya wanafunzi waliofukuzwa UDOM, akaniambia "ninashangaa sana TBC walitoa madai tofauti na yale ambayo sisi tulikuwa tunayadai wakati wa mgomo, yaani tulishangaa kuona hivyo" Je, hivi nyinyi sources zenu za news mbona zimekuwa za upendeleo sana siku hizi? Hivi kwanini mpaka mbadilishe habari? mnaibadilisha ili kudanganya umma? kwa hili mmepotea njia kabisa!

  2. Credibility
  Jueni kabisa kwamba vyombo vya habari vinaongozwa na hiki kitu credibility. Sasa nyinyi mmepoteza sana credibility yenu kwa watu! Yaani kila mtu siku hizi ukifika wakati wa news ukiweka TBC anakwambia na wewe ni magamba? weka ITV au Star TV bwana. Yaani sijui kitengo chenu cha ufuatiliaji kinafuatilia kweli juu ya hili? Kama watu wanakwepa kuangalia news zenu kweli kabisa hamuoni kuwa mmepoteza credibility?

  Jilinganishe na TV zingine za nchi zingine, Angalieni hata ya wenzenu KCB1 iko tofauti mno na nyie. angalieni TV za nchi zingine mjifunze. Mmekuwa mnaficha ukweli na kutetea uovu hivi ndivyo ilivyo kwenye media kweli? Nyinyi ndiyo mnatakiwa myafichue maovu lakini leo ndo imekuwa kinyume. Ndiyo maana Jerry Muro yalimkuta hayo, kwa sababu hampendi ukweli.


  MAMBO YA KUZINGATIA.
  1. Jiondoeni kwenye siasa, wekeni news balance ziwe wazi kwa watu wote.
  2. Acheni kutetea chama tawala, simamieni haki katika nchi yetu, komboeni maisha ya wanyonge kwa kuionyesha jamii ukweli halisi.
  3. Fuateni kanuni za uandishi wa habari, achenikujifanya hamzijui.
  4. Jengeni kuaminika (credibility) kwa watanzania wote.
  5. Shida yenu kubwa ni hapo tu BALANCE ya NEWS na matukio mbali mbali.

  Asanteni kwa kunielewa.
  Radio Producer.
   
 2. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nilishaacha kuangalia news TBC1, utaangaliaje magamba?
   
 3. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mpaka wajivue magamba ndio watabadilika hawa, naona hawasomi wala kuelewa ishara za nyakati wanafikiri kama wakomunist walivyofikiri kuwapa wanachi taarifa za propaganda wakifikiri hawajui hali halisi
   
 4. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Wamo humu humu nadhani watakaa na kuliona hili!
   
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  wanaelewa wanachokifanya ila naona watunika vibaya.
  mimi sijaangalia taarifa ya habari ta tbc kitambo sana.
   
 6. X

  XOXOQY JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  yan kwenye familia yetu ukikutwa unaangalia taarifa ya habari TBC unapewa likizo ya kutoshika remote control ya tv mwezi mzima,alafu mwanzo wao wa habari lazima waanze na taarifa ya chama cha wavua magamba hata kama kuna tukio muhimu la kijamii la kuanza nalo!
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Tunahitaji kuichukua hii TBC sisi kama wananchi sababu sie ndo tunaiendesha kwa kodi zetu, so tunawajibu wa kuhakikisha tunapata kile kinacholingana na kodi zetu na si upuuzi wa mtiririko wa vipindi vya ccm
   
 8. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Mkuu Radio Producer,
  Umelongo ukweli kabisa,tatizo kubwa la serikali yetu wameshindwa kutofautisha kati ya Chama na serikali.Kila kitu kinachofanywa eti ni sera ya CCM usishangae wakikuambia kinachofanywa TBC1 wanatekeleza ilani ya CCM,
  Sio siri tena baada ya kuondoka Tido hii shirika linaelekea kufa linarudi enzi zile za TVT.
  Ikifika kipindi cha taarifa ya habari zile headline zinazopita chini yani zinatia hadi kichefuchefu,siju hawa jamaa wamelala usingizi.Taarifa zao ziko so biased hadi unashangaa.
  Watangazaji wake walivyokuwa viherehere juu ya mambo ya CCM kama wao ndio wasemaji wakuu.

  Cha msingi hapa warudishe Tido
   
 9. m

  mja JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i think kila mtu ana udhaifu wake, lakini TIDO pamoja na madhaifu yake, aliiweka TBC mahali fulani hasa katika credibility, ilikuwa juu sana, TBC ya sasa iangalie yale machace mazuri ya mkurugenzi aliyepita , yaendelezwe, na vile vile kama alivyosema Radio Producer, TBC angalienei wenzenu wanavyofanya, msiige ila mjifunze
   
 10. w

  wasp JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watangazaji kama Marin Hassan Marin na Jane Shirima ni vinara wa tutetea Chama Cha Magamba
   
 11. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mbona hata hizo mnazo sifia zinaweka kipa umbele maslahi ya mmiliki wake kwanza. Kama ukijua vizuri kwamba TBC ni mali ya Serikali iliyo wekwa na Chama tawala hapo unategemea nini? Kuna mahadiri fulani waliyo wekewa katika utangazaji wa habari za humu nchini, huwezi kufananisha vyombo vya watu binafsi na vya Serikali au kama hizi social networks, na hii si kwa Serikali ya Tanzania tu hata Serikali za magharibi kama Merikani wako makini sana wanacho tangaza kuhusu Serikali yao, sasa mtu ukilijua hilo basi wakati wa taharifa ya habari tune kwenye Channel mbadala ambazo unadhani zitakupa habari sahii. Maana humu nimeona mnaisifia sana TBC hisipokuwa taharifa ya habari! Kwa hiyo tusimuhulize Mkurungenzi wa TBC the OBVIOUS.
   
 12. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Ushauri wangu kwa Marin Hassan Marin, ajaribu kuachana na mambo ya kuwa too colourful it is unhealthy kwa chombo cha utangazaji wa Taifa - kuwa serious na maswali yako na usijaribu kutega watu hili watoe majibu unayotaka wewe au wakati mwingine waonekane wajinga. Natoa ushauri kwa nia nzuri tu, sina tatizo na wewe kama binadamu.
   
 13. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mbona hata hizo mnazo sifia zinaweka kipa umbele maslahi ya mmiliki wake kwanza. Kama ukijua vizuri kwamba TBC ni mali ya Serikali iliyo wekwa na Chama tawala hapo unategemea nini? Kuna mahadiri fulani waliyo wekewa katika utangazaji wa habari za humu nchini, huwezi kufananisha vyombo vya watu binafsi na vya Serikali au kama hizi social networks, na hii si kwa Serikali ya Tanzania tu hata Serikali za magharibi kama Merikani wako makini sana wanacho tangaza kuhusu Serikali yao, sasa mtu ukilijua hilo basi wakati wa taharifa ya habari tune kwenye Channel mbadala ambazo unadhani zitakupa habari sahii. Maana humu nimeona mnaisifia sana TBC hisipokuwa taharifa ya habari! Kwa hiyo tusimuhulize Mkurungenzi wa TBC the OBVIOUS.
   
 14. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Mkuu hata kama wanaelewa wanachokifanya lakini wamezidi sana hadi kuwa wanabadilisha habari?
   
 15. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Ni kama unaeleweka mara unazamia mbali mara unakaribia nilikuwa nataka kukudaka duh umeniponyoka nimeona nikuachie tu!
   
 16. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Ni kweli, huyu bwana yupo vizuri sana kwenye fani hii lakini sijui wanaogopa nini, wakikufukuza utapata kazi kwingine utafanya kwa heshima!
   
 17. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Yaani inauma kweli watu wenye uwezo mzuri kama hawa wanalia kwenye magamba jaman
   
 18. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Unasema kweli kabisa mkuu! yaani inaumiza kuona televisheni ya taifa inafanya mambo ya ajabu ajabu tu!
   
 19. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Yaani umazungumzia zile title za chini huwa zinanifanya nivimbe figo kabisa yaani sijui anayeandika ana akili timamu au ana timamu akili? Ukiangalia kama Title za Startv unazisoma unaelewa kinachoendelea, kwa kitaalamu zinacover 5W+H lakini hawa TBC hata 2W sidhani kama wanafika huko
   
 20. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Nahic pia itakuwa vizuri zaidi ikiingia serikali nyingine madarakani ni kutimua wafanya kazi wote na kuleta mbegu mpya!
   
Loading...