Ushauri wa bure kwa Waislam

Ushauri wa bure kwa Waislam

Status
Not open for further replies.

screentouch

Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
91
Reaction score
45
Ukiupenda chukua usipoupemda sepa.

Nawashauri waislam kwakuwa mahakama ya kadhi ni ibada waunde jumuiya ndogondogo za waislam ambazo watafanya ibada zao huko na watashitakiana ndoa zao huko na watapeana talaka huko. Ndoa zitasuluhishwa na Waislam wenyewe. Hii itakuwa rahisi kwakuwa waislam wote ktk jumuiya zao watakuwa wanafahamiana. Hii waendeshe kama idara fulani ndani ya jamii zao na hili ni jambo dogo sana ambalo halina sababu za msingi kuliweka kwenye katiba. Ni kama vile wakrisito walivyounda jumuiya zao wala hawakuomba ziandikwe kwenye katiba kwasababu walijua ni ibada yao sio jambo lakitaifa na hivyo halihitaji kuandikwa kwenye katiba.

Kuhusu mirathi tunazo mahakama za serikali iliyochaguliwa na wananchi wote ambazo zinafanya vizuri na zina utaratibu mzuri wakusimamia mirathi hivyo mirathi ya waislam itashughulikiwa huko. Sioni hoja wala sababu ya msingi waislam kutaka mahakama yao special kwa ajili ya mirathi wakati tayari kuna mahakama inasimamia mirathi hivyo hakuna ulazima wakuandika kwenye katiba.

Karibuni tujadili kwa hoja, matusi njoo PM tutukanane mpaka nikukomeshe.
 
hizo jumuiya kama zitakuwa hazitambuliwi kisheria zitakuwa hazina maana.huwezi kuunda jumuiya inayo towa taraka kwa waislam pindi wakiachana kisha ukienda mahakamani unaambiwa taraka hiyo batili.

mahakama ya kadhi haiwahusu nyinyi wakristo,tunahusika sisi waislam.

Sheria ya mirathi kwa waislamu mtoto wa asie zaliwa ndani ya ndoa haruhusiwi kurisi mali ya marehem.je mahakama za serikali inalitambuwa hilo?

Wakristo kwanini mnapinga mahakama ya kadhi wakati haiwahusu?tukisema mna husda nyinyi wakristo mtabisha?
 
Umeongea vizuri sana, na hapa ndiyo root causes ya tatizo lenyewe. Kwamba mahakama ya kadhi ni kwaajili ya waislamu tu. Kwamba wakiristu haiwahusu kabisa.

Sasa kama ni hivyo kwanini basi wakiristu na watu wengine wasiohusika na mahakama ya kadhi wagharamikie kuiendesha hiyo mahakama ambayo haiwahusu kabisa.

Mimi sina tatizo kama katiba itatambua uwepo wa mahakama ya kadhi. Lakini uendeshwaji wake na gharama zake uwe ni juu ya waislamu wenyewe.

Mpaka leo tunasikia malalamiko kutoka kwa waislamu wengi kwamba serikali iliwaundia BAKWATA. Kwanini tena leo mnataka serikali hiyo hiyo uwaundie MAHAKAMA YA KADHI?!

Hapa ndio kunapoleta mashaka makubwa
 
Hatupingi kuanzishwa tunachopinga ni kutumia kodi zetu kuwalipa hao makadhi wenu na kuliweka suala hili kwenye katiba yetu
 
Well said Bobuk ...take "like"!
 
Last edited by a moderator:
Hatupingi kuanzishwa tunachopinga ni kutumia kodi zetu kuwalipa hao makadhi wenu na kuliweka suala hili kwenye katiba yetu

Halafu unaweza kukuta hata VAT tu hujawahi kulipa! Unanunua kila kitu kwa wamachinga na mama ntilie.
 
Nikiwa kama muislamu naunga mkono mahakama ya kadhi iwepo kwa mujibu wa sheria. Lakini suala la kuiendesha kwa kodi ya jumla ndio siungi mkono, naona itapelekea kuendeshwa na pesa chafu za wauza pombe na nguruwe.
Mimi mawazo yangu ni kuunda kitengo maalumu ndani ya TRA ambacho kazi yake itakuwa kukusanya kodi ya kuendeshea mahakama ya kadhi tu. Kitengo hiki kiwe na kitu kama fomu hivi ambayo walipa kodi wakiislamu wenye TIN wata declare kwa hiyari yao kuongezewa percent ndogo kwenye kodi wanazolipa kuendeshea mahakama ya kadhi. Naamini waislamu ni walipa kodi wazuri na wanaipenda dini yao, hawawezi kupinga utaratibu kama huu.
 
hizo jumuiya kama zitakuwa hazitambuliwi kisheria zitakuwa hazina maana.huwezi kuunda jumuiya inayo towa taraka kwa waislam pindi wakiachana kisha ukienda mahakamani unaambiwa taraka hiyo batili.

mahakama ya kadhi haiwahusu nyinyi wakristo,tunahusika sisi waislam.

Sheria ya mirathi kwa waislamu mtoto wa asie zaliwa ndani ya ndoa haruhusiwi kurisi mali ya marehem.je mahakama za serikali inalitambuwa hilo?

Wakristo kwanini mnapinga mahakama ya kadhi wakati haiwahusu?tukisema mna husda nyinyi wakristo mtabisha?

Hii isshue itatucost sana....mana na nyie waislam mlivyokuwa mahodari wa kuoa na kuacha...am sure kila kitongoji mtataka kiwe na mahakam....badala ya kutoa hoja za maana kwenye katiba mpya mnazungumzia huu upuuzi....na nyie wengiwenu mlivyokuwa hamna elimu ya kutosha, mahakama ya kadhi ikiwekwa kwenyekatiba mtaisapoti tu hiyo katiba hatakama imejaa madudu.....na CCM kweli wamepata watu wajinga...mtaendeshwa nyie na maCCM hadi mtatia akili...we jiulize kitu hao hao ccm wakati wa ukusanyaji wa maoni ya rasimu walkuwa wanapinga mahakama ya kadhi...leo hii hawana saport bungeni kugain saport wakakumbuka kuna group la watu wasiojua kujenga hoja, wakawawekea kipengele cha mahakama...sasa hvi wote mshaanza kusaport ccm mshaitelekeza CUF......
 
Nikiwa kama muislamu naunga mkono mahakama ya kadhi iwepo kwa mujibu wa sheria. Lakini suala la kuiendesha kwa kodi ya jumla ndio siungi mkono, naona itapelekea kuendeshwa na pesa chafu za wauza pombe na nguruwe.
Mimi mawazo yangu ni kuunda kitengo maalumu ndani ya TRA ambacho kazi yake itakuwa kukusanya kodi ya kuendeshea mahakama ya kadhi tu. Kitengo hiki kiwe na kitu kama fomu hivi ambayo walipa kodi wakiislamu wenye TIN wata declare kwa hiyari yao kuongezewa percent ndogo kwenye kodi wanazolipa kuendeshea mahakama ya kadhi. Naamini waislamu ni walipa kodi wazuri na wanaipenda dini yao, hawawezi kupinga utaratibu kama huu.

Hapo kwenye red, umechemka dogo!
Ndiyo maana watu wanapiga Mahakama ya Kadhi kuingizwa ktk Katiba. Ikiwa mmeshindwa kuchanga hata sadaka kwa ajili ya mambo yenu ya maendeleo hili la Mahakama ya Kadhi mtaweza?
 
Nikiwa kama muislamu naunga mkono mahakama ya kadhi iwepo kwa mujibu wa sheria. Lakini suala la kuiendesha kwa kodi ya jumla ndio siungi mkono, naona itapelekea kuendeshwa na pesa chafu za wauza pombe na nguruwe.
Mimi mawazo yangu ni kuunda kitengo maalumu ndani ya TRA ambacho kazi yake itakuwa kukusanya kodi ya kuendeshea mahakama ya kadhi tu. Kitengo hiki kiwe na kitu kama fomu hivi ambayo walipa kodi wakiislamu wenye TIN wata declare kwa hiyari yao kuongezewa percent ndogo kwenye kodi wanazolipa kuendeshea mahakama ya kadhi. Naamini waislamu ni walipa kodi wazuri na wanaipenda dini yao, hawawezi kupinga utaratibu kama huu.

Na hao wafanyakazi wa TRA watakaowakusanyia kodi watalipwa mishahara na nani? Na bado hatujaongelewa ufisadi/wizi wa kodi hizo utakofanywa na wafanyakazi wa TRA wasio kuwa waaminifu?

Kwanini nyinyi waislamu humtaki kubeba wajibu na majukumu yanayohusu dini yenu. Tengeneza utaratibu huo wenyewe kwasababu mahakama ya kadhi ni suala la kiimani. Wakati kodi ni suala la lazima halina hiyari.
 
Katiba haina dini haitambui dini,so acheni ujinga wa kuingiza mambo yenu ya katiba,nendeni mkajadirini misikitini.
 
Tatizo la watu wa imani hii kwanza hawaelewani, na hawaelewi hata imani yao inataka nini na kwanini. Kukosa kuelewa huko kumewafanya wakose hoja na kukosa hoja ndioko kumewafanya wajisikie inferior bila sababu na hivyo ndiyo maana kila wakati, mahala pote huwa wako suspicious na defensive na ndiko kutumia mabavu kwa kila jambo.

Ushauri hawashauriki hasa katika mema. Hakuna kitu utawashauri wakubali hata kama hawana hoja. (mfano, kwa nini mahakama zao ambazo ni ibada wanataka ziwekwe na serikali badala ya kuzifanya taasisi zao za kidini misikitini kama vile makanisa wanafanya), watakachokuambia ni matusi, na kutishia kufanya fujo kwa kisingizo kwamba wao wako wengi eti kwa kuwa hawanaga uzazi wa mpango, na vile wanavyotoa zawadi kwa muislam akioa mkristo.
Lakini kwamba wanahoja, hakuna.

Jambo lingine hawa watu si rahisi kuwashauri kutenda mema kwa sababu dini yao haina nguzo ya upendo. Wewe ukiwashaurim upendo, amani na kusameheana, halafu mwingine awashauri chuki, fujo visasi na mauaji, utashangaa watakavyochangamkia tenda za chuki, fujo, visasi na mauaji. Wanafanya hivyo hadi misikitini wao kwa wao wanamalizana halafu wanasingizia Westerners na Wakristo eti ndio wanawashauri hivyo. Hawatakumbuka kama kuna ushauri wa upendo, amani na msamaha. Ni jambo la ajabu sana kama dini yao inawafundisha upendo na amani, inakuwaje wanakimbilia kuwatii makafir wanaowafundisha chuki, mauaji na ushetani wote wakati hao makafir maisha yao yamejaa amani.

Kikubwa ili serikali iweze kusimamia vizuri vichwa vya namna hii, ni vyema ikae kwenye nafasi ya juu ya imani zote ili isimamie na kudhibiti pale ushetani unapotokelezea kwenye misiikiti kama Lyatonga. Katiba ni ya watanzania wote, habari za kadhi, misikitini.
screentouch
 
Last edited by a moderator:
hizo jumuiya kama zitakuwa hazitambuliwi kisheria zitakuwa hazina maana.huwezi kuunda jumuiya inayo towa taraka kwa waislam pindi wakiachana kisha ukienda mahakamani unaambiwa taraka hiyo batili.
.

Sheria ya mirathi kwa waislamu mtoto wa asie zaliwa ndani ya ndoa haruhusiwi kurisi mali ya marehem.je mahakama za serikali inalitambuwa hilo?

Wakristo kwanini mnapinga mahakama ya kadhi wakati haiwahusu?tukisema mna husda nyinyi wakristo mtabisha?

Unaposema hazitatambuliwa kisheria, je ndoa mnazofungishana msikitini nazo ni batili? Mbona vyeti mnapeana huko miskitini a si ahakamani? Kuhusu watoto nje ya ndoa mnapowazaa mnataka wao warithi wapi? Au mnataka wawe wezi mitaani? Kuna mambo mengine yanahitaji busara kuyatatua na si kukaririshana kwa sharia. Je ungekuwa wewe ndo umezaliwa nje ya ndoa ungejisikiaje. Makosa wafanye wazazi wahukumiwe watoto... Tuweni na huruma inaniuma sana.
 
Waisilamu nchini wamekuwa wakiilamu serikali kwamba imewaundia chombo ambacho ni BAKWATA, na kwamba hawakitaki kwa kuwa hakijaundwa na waisilamu. Waisilamu hao hao wanaitaka serikali iwaanzishie chombo kinachoitwa Mahakama ya Kadhi. Sasa hapa naona kuna ujinga fulani. Unalalamika serikali kuwaingilia kwa kuanzisha BAKWATA, halafu unalalamika kwa nini serikali haiwaingilii kwa kuwaanzishia Kadhi. Waisilamu wawe wazi basi, wanapenda kuingiliwa au kutoingiliwa na serikali?

My take:
Kwa kuwa waisilamu wameshalalamika sana kwa suala la 'kuundiwa BAKWATA', naishauri serikali isijiingize kabisa kujaribu kuwasaidia tena, kwani watakuja kuilaumu tena na tena serikali kwa kuwaingilia. Waisilamu wajipange, waanzishe Mahakama ya Kadhi, waiendeshe wenyewe, wahukumiane wenyewe na hata hukumu zikiwa mbaya, walaumiane wenyewe
 
Waislamu lengo lao kuu ni kuifanya Serikali yenyewe kuwa ya Kiislamu, kwa hiyo wakifanikiwa hilo hawatakuwa "wanaingiliwa na Serikali" kwa kuwa itakuwa ni ya kwao!
 
Wandugu kinachosababisha watu watake hii mahakama iwe kwenye taratibu za ngazi za mahakama ni kufanya mambo ya waislamu ya kijamii yahukumiwe katika utaratibu uliopo kwenye quran tukufu.
Kuna watu wengi wanaunganisha familia (ndoa) kwa hiyari yao wenyewe katika taratibu za kiislamu, lakini unapofika wakati wa mashtaka wanakimbilia serikalini ambayo haina sheria hata moja ya kiislamu.
Kama mti akiua mathalani anaweza kufunguliwa kesi kwenye mahakama ya wilaya, atasomewa mashtaka lakini ataambiwa hatakiwi kujibu chochote mpaka hapo kesi itakapohamishiwa mahakama kuu.
Sasa kwanini isiwezekane mtu kufungua kesi ya mirathi au talaka mahakama ya wilaya akaambiwa kesi hiyo itahamishiwa mahakama ya kadhi? Je unaweza kuweka mfumo kama huu katika mahakama halafu uendeshaji wake usihusishe mapato yanayokusanywa katika taratibu za kiserikali?
Tafakari!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom