Ushauri wa bure kwa Tundu Lissu

Ushauri wa bure kwa Tundu Lissu

Sasa hivi jina la Tundu Lissu lina pepea kwenye mmmedia karibu zote kama mvua za masika.

Wengi tulisikitishwa na jaribio la kumaliza maisha yake, na waliotekeleza hilo bado wapo, hawajulikani.

TL amshukuru Mungu kwa kupona na kuweza kuelezea mkasa ule.

Tatizo la Lissu ni mdomo wake, hautulii!

Waswahili husema mdomo uliponza kichwa.

Waliotaka kumwua wapo, na kwa hali yoyote wameshika mpini, Lissu kashika makali.

TL namshauri awe mpole, mdomo utulie maana huko aliko Ulaya ni makazi ya muda tu, wanaomsaidiabila shaka watamchoka.

Na akirudi nyumbani atakutana na marafiki kwa mahasimu wale wale.

Lissu narudia, mdomo uliponza kichwa.
Kwani mnateseka?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubaya lazima usemwe ili dunia ielewe na iukomeshe , hii ndio maana Lissu anazidi kuchanja mbuga , hii ndio njia pekee ya halali ya yeye kuwa salama na kuheshimiwa , dunia lazima iambiwe uharamia wa Tanzania ambao miaka yote ulifichwa? .

Shukrani sana Mh Lissu kwa kuitoa matongotongo Dunia kuhusu Tanzania , kwa kuwataja wahusika wa uchafu kwa majina yao yote matatu
Vipi ile nishani ya Nobel bado Lissu hajaipokea hadi leo?
 
Back
Top Bottom