Ushauri wa bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako, Jiondoe kugombea NEC ya CCM!

Hivi EL huwa anapita mitaa hii?

Sasa kama hapiti basi ni kwa nini Pasco wa JF ametumia njia ndefu hivi kumfikishia ujumbe? Sio ange-PM au angewasiliana na Fred tu then msg ingemfikia Leigwanan......why lakini?
 
mkuu nadhani hata ikiwa kama unavyotaka "Policies and not personalities" si sahihi hata kidogo! nadhani personalities and Policies should be our anthem!(sijui nimeeleweka kwa kidhungu changu cha kuunga?)

Huwezi kuepuka personalities, ndiyo maana hata Marekani ni lazima usikie "Romney this" "Obama that"

Kwa hiyo unaposema "personalities and policies" siwezi kukukatalia.

Tatizo watu wamejikita katika personalities, wameachana kabisa na policies.

Ukiwauliza Lowassa anaaamini katika policies gani, hawawezi kukujibu. Ukiwauliza Lowassa na Membe policy wise wana tofauti gani? Hawawezi kukujibu.

Soma post ya Pasco tafuta policy issue hata moja inayomdistinguish Lowassa.

Ndo maana nasema tunazungumzia personalities zaidi kuliko policies.
 
Edward Lowassa kwa CCM na urais wa 2015 ni kama Zitto Kabwe na Chadema kwa urais wa 2015!, both are powerful, action oriented, mabingwa wa mass mobilization, wana vipaji vya hali ya juu vya "visionary leadership", wote wana capabilities za kutupatia the "best presidents" this nation had ever had, na both wana the same weakneses, vote ni "egotists", very assertive, selfish, with unicentric view ambao wanaona upande mmoja tuu wa shilingi,, their side which is the right side, hawaoni, hawasikii, wala hawaambiliki, wanalotaka wao ni lazima liwe!.

hapo tu ndio huwa pananifanya hawa jamaa nisifikirie kuwapa kura yangu
ikitokea hii combination kwenye uchaguzi 2015 EL VS ZZK .. ntapata wakati mgumu sana itabidi nimpe
prof.. lipumba akigombea..
 
Hivi EL huwa anapita mitaa hii?

Sasa kama hapiti basi ni kwa nini Pasco wa JF ametumia njia ndefu hivi kumfikishia ujumbe? Sio ange-PM au angewasiliana na Fred tu then msg ingemfikia Leigwanan......why lakini?
Mkuu RR, mimi ni mshabiki tuu wa EL sio mfuasi wake kusema nakaa naye hadi kuijua familia yake mpaka nimtumie PM au nimtafute mwanaye Fred. Pasco wa jf, hapa jf ndio nyumbani kwake na jf ndiyo sebuleni kwake, ndio chumbani kwake ndio kitandani kwake na jf ndio mdomo wake!. Kila kitu kinawekwa wazi hapa kwa sababu Pasco wa jf ni kwa ajili ya jf tuu, tukienda kwenye PM, SMS au kumpigia simu, itakuwa sio Pasco wa jf tena, huyo sasa atakuwa ni mtu mwingine halisi kama ulivyo wewe RR naamini hiyo RR ni kwa jf tuu tukianza kufuatiliana tutakuta kumbe ni mtu mwingine kabisa!.
P.
 
Nadhani Lowassa anafaa tu kuwa baba wa familia yake na si Urais wa nchi yetu. Nchi iliyojaa rasilimali nyingi hivi kumpa Lowassa Urais ni sawa na kumpa fisi bucha alinde.
 
Mkuu Pasco kuwa shabiki wa Lowasa hilo sio tatizo lakini wewe umesahau kirahisi kuwa huyu Lowasa alituingiza mkenge wa RICHMOND hadi leo tunnalipa mabilioni ya fedha mara capacity charge mara deni la RICHIMOND au na wewe uzalendo wa Tanzania huna ni wakuja tuu???
Mkuu Mtumishi Wetu. Richmond sio ya Lowassa bali ni ya wenyewe na wapo!. Ilikuja kwa jina la Richimond ikajigeuza Dowans na sasa ndio hii Simbion na tunanunua umeme kwa bei ile ile kilichobadilika ni jina tuu!. Kwa vile sasa EL sio sehemu ya uoza huu, kwa nini usiwaulize hao Tanesco kama serikali ilivunja mkataba na Dowans kutokana na madudu kibao, kwa nini imeingia mkataba mwingine na Simbioni wa madudu yale yale?. EL alikubali tuu kubeba zigo la watu kuwasetiri aibu!. Sasa wameisha setirika ndio hao sasa wanaleta ngebe!.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: SG8
Mkuu Mwalimu, Dr. Kitila Mkumbo, kama EL atapita NEC, then JK is nothing!, that will mean EL ndio CCM, na CCM ndio EL!. Serikali imeshatenga Bilioni 400 za kugawa kama ruzuku kwa wananchi wanaoishi below poverty line (less than one $ a day)!. by 2015, with daraja la Kigamboni, mabarabara juu na chini, na hiyo rushwa ya ruzuku kwa familia masikini, jee kuna jinsi nyingine yoyote ya kuizua CCM?. Baada ya kuwapatia Watanzania katiba mpya, nahisi sisi watatangaza huduma za afya na elimu mpaka kidato cha nne ni bure ili Chadema ikose cha kusema!.
Politics is a dirty game!.
P.
Mkuu Pasco,
Hapa pia natofautiana na wewe.... Billioni hizo hazitawafikia walengwa kama zile billioni 21 za JK. Yuko wapi wa kusimamia? Wassira? Pinda? Membe? Au Hawa Ghasia? hapa ndipo watakapoibua chuki kupita maelezo. Lakini pia naungana na Mwalimu Dk Kitila Mkumbo. Lowassa ni mzito sana ndani ya CCM na ana ushawishi mkubwa sana. Nimeongea na watu kadhaa wanaomuunga mkono.Jamaa ana wafuasi influential sana ndani ya Chama chake na hata serikalini. Hata mtandao wake watu wengi wanataka ku overlook..Kina Emmanuel Nchimbi, January Makamba, Ngeleja, Mahanga, Serukamba na wengine bado wamo. bado watu kama Ole sendeka na Shelukindo wasiotabirika. Kumbuka ndani ya CCM wapo watu wengi wanaosoma mwelekeo wa upepo. Tatizo la Lowassa ni nje ya CCM. Wananchi wa kawaida.. na kwangu mimi ni wale wenye uelewa wa chini/kati. Wanadhani Loawassa ni Richmond na Richmond ni Lowassa (Mimi siamini hivyo). Siku atakaporudia zile dakika 7 za NEC za kumwambia ukweli Mwenyekiti hukumu pekee atakayobaki nayo Lowassa ni kwanini alikubali kukinusuru chama na serikali yake kwa expense ya Wananchi (kujiuzulu) basi!!
 
Last edited by a moderator:
Pasco nimevua kofia nakupa LIKE sasa sitachangia tena ila nitakuwa nazisoma post zako kwa macho mawili nilikushauri tusubiri M/Mkuu picha Novemba 12 itajionesha lkn umeionesha na ww si mtabiri ila ndio reality
Ingawa muda bado kutabiri mgombea Urais lkn hata Membe alishakiri hadharani EL ana mihela!!
Mkuu umenitisha hasa ile Bilioni 400 point no 8 'Safety net' Bajeti ya Ruzuku naomba tumwagie hata link maana kweli hela huyu jamaa anayo
Ni kweli hakuna asiyetaka hela hao NEC ni walengwa na wote wanaweza kupokea na kura watampa EL km mgombea Urais lkn fika wanajua akisimamishwa na jiwe kwenye Ballot box la Wananchi HAPITI
 
Last edited by a moderator:
Pasco naona umegunduwa unafiki wa JK,ni vizuri kumshauri jamaa yako EL maana yule jamaa ni mnafiki haaminiki.Hata mimi nimeshangazwa kweli yani mke wake na mtoto wake wamemzidi licha ya yeye kumnusuru madaraka.

Sana sana alichoambulia ni kunyenyuliwa mkono juu kwenye kampeni,kusema hawajakutana barabarani,pamoja na ile kauli ya "Hii ni ajali ya kisiasa".Ushauri wako una ukweli,maana anaingizwa chaka.

JK hakutakiwa awe rais bana,huo ni ukweli.

mushi hamna mtu anayezaliwa kuwa rais

jk aliutaka urais, akavumilia kwa miaka kumi mpaka akaupata... hawa ccm wengine wa leo hawana huvumilivu.

kitu ambacho Jk anakifanya vizuri sana mpaka sasa hivi hajakosea tokea aingie madarakani ni "kuwachoma sindano vigogo wenzake wa ccm pale anapotaka"
ukiangalia alivyomdunga lowasa, sita na juzi tu kamfanya mkono aonekane sisimizi utashangaa

Jk is politically inteligent than EL
 
Last edited by a moderator:
UPDATE!,
Nimesoma taarifa hii kutoka Monduli
Edward Lowassa ameshinda ujumbe wa NEC wilaya ya Monduli!. Ushindi ulioupata mzee sasa umepitiliza. Walidhani utafuata nyayo za Sumaye ila kuna tofauti kubwa sana kati yako na yeye!

Kushinda kwa asilimia 99.9 si mchezo NEC hiyo sasa! Hongera Comrade......
 
Pasco:

i) Lowasa hawezi kushindwa uchaguzi wowote ndani ya CCM. He is currently the most powerful politician in CCM. Kumlinganisha na Sumaye ni kutokuzingatia context. Nguvu ya Sumaye ilikufa mara pale uwaziri mkuu wake ulipoisha. Kumbuka sifa pekee aliyekuwa naye Sumaye kama waziri mkuu ni kwamba alikaa miaka kumi katika nafasi hiyo na hivyo akatengeneza cronies wengi sana ndani ya CCM waliopata madaraka na ulaji kwa kupitia yeye. Lakini sasa miaka kumi baadaye hana kitu kwa sababu hao jamaa aliowaweka wameshasambaratishwa wote. Tofauti ya Lowasa ni kwamba bado anaendelea kuwa na watu ndani wanaomwamini kama taasisi na kusema kweli ndani ya CCM yeye ndiye mwenye akili zaidi za kisiasa, kifikra na kiutendaji. Hii pia inaeleze jinsi CCM ilivyo hoi kwa sababu hakupaswa kuwa na taswira hiyo. Kwa hiyo, Lowas madamu unahusisha kura, Lowasa atashinda uchaguzi wowote ndani ya CCM.

ii) Uchaguzi nje ya CCM-Lowasa ni mwepesi na ni mzito pia. Ni mwepesi kama atapambana na wanasiasa wenye sifa maalumu kama akina Dk Slaa. Kwa maoni yangu Dk Slaa ana sifa moja kubwa inayomtofautisha na wanasiasa wengine active kwa sasa, nayo ni ukweli kwamba yeye ni mkweli na mhalisia (genuine and honest). Hii ni sifa ambayo ni adimu sana kwa wanasiasa wa Tanzania. Ni mzito kama ukimgombeanisha Lowasa na mwanasiasa mwingine ambaye si aina ya Dk Slaa, ambaye itakuwa vigumu kupata sifa za ziada za kumshinda Lowasa.

Let's wait and see!
Mkuu Kitilla, matokea yametoka, Lowassa kashinda kwa 99.9 %!. You are dam right, I'm very wrong!.
Nakiri kukosea utabiri!, sasa tusubiri matokeo ya EL kuingia NEC!.

Pasco.
 
Wanabodi, hii nimeitoa kule Globu ya Jamii!.
MONDAY, OCTOBER 01, 2012
[h=1]MH LOWASSA ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA NAFASI YA UJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA WILAYA YA MONDULI[/h]



Mh Lowassa akizungumza na kuwashukuru wapiga kura wake waliompatia ushindi wa kishindo

Waziri mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,mh. Edward Lowassa akipongezwa mara baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu ya Wilaya ya Monduli uliofanyika leo katika ukumbi wa chuo cha ualimu Monduli,Mh Lowassa ameshinda kwa kishindo kwa kuwabwaga wapinzani wake kwa idadi ya kura 709,mpinzani mwingine ameta kura 44 na mshindi mwingine aliibuka na kura 7.


Waziri mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,mh. Edward Lowassa akipongezwa mara baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu ya Wilaya ya Monduli uliofanyika leo katika ukumbi wa chuo cha ualimu Monduli,Mh Lowassa ameshinda kwa kishindo kwa kuwabwaga wapinzani wake kwa idadi ya kura 709,mpinzani mwingine amepata kura 44 na mshindi mwingine aliibuka na kura 7.



MY TAKE!.
BAADA YA JK KUMPIGA PANGA MKONO, NILIAMINI SASA JK SIO DHAIFU TENA, HIVYO ANAYEFUATIA NI EDWARD LOWASSA ILI KUMSAFISHIA MEMBE NJIA NYEUPE YA 2015!.

NAKIRI, I WAS WRONG, SIO NILIMU UNDERESTMATE LOWASSA, BALI NILI MUO OVER ESTIMATE JK!.

KWA MATOKEO HAYO, KUBALINI, KATAENI, MSHINDI WA URAIS 2015 NI CCM!, NA RAIS WA 2015 NI EDWARD LOWASSA!.

NB. KUNA BILIONI 400 "SAFETY NET" KWA WAPIGA KURA WA 2015!. BAADA YA KUJENGEWA DARAJA LA KIGAMBONI, MABARABARA YA JUU NA CHINI!, HUDUMA ZA AFYA NA ELIMU BURE!, SASA FAMILIA MASIKINI ZITAGAWIWA RUZUKU YA KUONDOA UMASIKINI!, 2015 NANI ATATHUBUTU KUIVOTE OUT CCM?, KWA VIGEZO GANI?.

HONGERA LOWASSA!, HONGERA CCM!.

Pasco!.

NB: Naendelea kusisitiza Pasco wa jf, sio mwanachama, mfuasi, wala mshabiki wa chama chochote!. Sasa wale mnaoamini kuwa Pasco wa jf ni mshabiki wa CCM, endeleeni kuamini hivyo, if that will make you happy!.














 
Pasco, Mkuu wangu,
Hujue unapasua watu vichwa kwa jinsi unavyocheza na vichwa vya Pro-Chadema JF.
 
Last edited by a moderator:
Pasco, Mkuu wangu,
Hujue unapasua watu vichwa kwa jinsi unavyocheza na vichwa vya Pro-Chadema JF.
Mkuu RITZ, hakuna pasua kichwa yoyote, ninazo mwaga humu ni pure facts, huwezi kushindana na facts!.
Mfano ..
  1. Its a fact kuwa CCM as CCM imechokwa mpaka basi!
  2. Its a fact kuwa CCM imeshindwa kuondoa umasikini, ujinga na maradhi tangu tumepata uhuru zaidi ya miaka 50 iliyopita.
  3. Its a fact, Chadema imeonyesha tumaini jipya, hivyo kiuhakika kabisa, Watanzania kuelekea 2015, wamepanga kuipiga chini CCM jumla!.
  4. Its a fact, CCM imetambua jinsi ilivyo chokwa, hivyo ili kuondoa umasikini, itawajaza watu mapesa (hard cash), zimetengwa bilioni 400 kwa jina la "safety net", hivyo kufikia 2015, umasikini uliotopea utakuwa ni hadithi!.
  5. CCM watatangaza huduma za Afya na Elimu bure, hivyo kupelekea kukosekana kwa sababu za kutoichagua CCM!.
 
Pasco umeahidiwa kazi ya mwandishi wa rais ajae?
natumai hivo, yote kheri
sina imani sana kama Lowasa atakuwa Rais wakimchagua ndio watakuwa wamekizika chama
hata mtoto anajua huyu bwana sio msafi na kwa sasa watanzania wameamka hawataki tena kuibiwa kura
nadhani kama atashinda labda kwa asilimia 20 zingine ni za wizi na lazima nchi itaingia katika machafuko
watu kwa sasa wamechoka na CCM mm sina chama na sidhani kama CCM imeandikwa kutawala milele
kama ilivokufa KANU ndivo itakavokufa CCM
take my words pasco.
 
Mtaji wa Lowassa Monduli ni umasikini, ujinga na uhayawani wa wamasai. Mleteni kwenye urais ndo mtajua kuwa wamasai ni wa mwisho kwenye nyanja ya elimu.
 
Mkuu RITZ, hakuna pasua kichwa yoyote, ninazo mwaga humu ni pure facts, huwezi kushindana na facts!.
Mfano ..
  1. Its a fact kuwa CCM as CCM imechokwa mpaka basi!
  2. Its a fact kuwa CCM imeshindwa kuondoa umasikini, ujinga na maradhi tangu tumepata uhuru zaidi ya miaka 50 iliyopita.
  3. Its a fact, Chadema imeonyesha tumaini jipya, hivyo kiuhakika kabisa, Watanzania kuelekea 2015, wamepanga kuipiga chini CCM jumla!.
  4. Its a fact, CCM imetambua jinsi ilivyo chokwa, hivyo ili kuondoa umasikini, itawajaza watu mapesa (hard cash), zimetengwa bilioni 400 kwa jina la "safety net", hivyo kufikia 2015, umasikini uliotopea utakuwa ni hadithi!.
  5. CCM watatangaza huduma za Afya na Elimu bure, hivyo kupelekea kukosekana kwa sababu za kutoichagua CCM!.

Mkuu Pasco,
Tupo pamoja namaanisha nondo zako zinawapasua kichwa hawa Pro-Chadema.
 
Last edited by a moderator:
Pasco umeahidiwa kazi ya mwandishi wa rais ajae?
natumai hivo, yote kheri
sina imani sana kama Lowasa atakuwa Rais wakimchagua ndio watakuwa wamekizika chama
hata mtoto anajua huyu bwana sio msafi na kwa sasa watanzania wameamka hawataki tena kuibiwa kura
nadhani kama atashinda labda kwa asilimia 20 zingine ni za wizi na lazima nchi itaingia katika machafuko
watu kwa sasa wamechoka na CCM mm sina chama na sidhani kama CCM imeandikwa kutawala milele
kama ilivokufa KANU ndivo itakavokufa CCM
take my words pasco.
Mkuu Lokissa, naendelea na uandishi wa habari just for the love of it, nafanya wrap-up by 2015!, by then, I would have passed 45 years age bar!, not ideal kuendelea na kazi za kitumwa!. Niliacha kazi za public office, since 2002!, mwaka huu 2012, its 10 years on my own, I don't think its good idea 2015, kurejea tena utumwani, baada ya kuishi more than 13 years ya uhuru!.
P.
 
BAK,

Unajua masuala yafuatayo carry totally different meanings when attended individually:


  • A Fan – Mshabiki;
  • A Follower – Mfuasi;
  • A Supporter – Kumuunga mkono mtu;

Mimi nadhani Pasco angekuwa na majibu kwa swali lako iwapo angesema yeye ni Follower au Supporter kwani by being a follower or supporter, it involves a certain ideological belief, or school of thought or political orientation; Vinginevyo kwa suala la ushabiki, nadhani utakuwa unamwonea tu Pasco kwani sote tunajua chanzo cha ushabiki in any context ni nini – mara nyingi hutokana zaidi na FAME OR ACHIEVEMENTS/ACCOMPLISHMENTS za anayehusika, iwe ni timu ya michezo, muigizaji filamu, mwanamtindo, mwanasiasa n.k

Pasco wakati wote amekuwa akijieleza in that context i.e. anajenga hoja zake kwa vigezo vinavyolalia zaidi
FAME OR ACHIEVEMENTS/ACCOMPLISHMENTS, na ni haki yake kufanya hivyo, ili mradi anaeleweka namna hiyo na yeye analijua hilo. Vinginevyo kama nia ya Pasco ni kukukusanya watanzania kwa levels zaidi ya ushabiki, ni muhimu abadilishe his style of presentation na iegemee zaidi towards him being a ‘FOLLOWER’ OR ‘SUPPORTER’, otherwise kwa mtindo wa SHABIKI, atazidi kuacha watu na maswali mengi kuliko majibu, huku muda kuelekea 2015 ukizidi kuyoyoma;

Mkuu Mchambuzi, kati ya makundi haya matatu,

A Fan – Mshabiki;
A Follower – Mfuasi;
A Supporter – Kumuunga mkono mtu;
Beliver- Waumini!
​Hawa beliver, ni waumini wa viongozi fulani wa Chadema mpaka wana waabudu!. Hivyo kwa urais wa 2015, waumini hawa wanawasubiria hao kina fulani, like congeregation waiting for their preacher, longed to hear him pray!.
P.


 
Back
Top Bottom