Ushauri wa bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako, Jiondoe kugombea NEC ya CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako, Jiondoe kugombea NEC ya CCM!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Sep 30, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,618
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Naomba nianze kwa ku declare interest: Mimi Pasco wa JF ni mshabiki mkubwa wa Waziri Mkuu Mstaafu, na Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, na kumchagiza yeye ndiye awe mgombea wa urais wa 2015 kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM!.

  Huu ni ushauri wangu wa bure, kwa Mhe. Lowassa, baada ya jina lake kupitishwa na CC na NEC kuwa ni mgombea wa Ujumbe wa NEC kwa wilaya na Monduli, namshauri, ili kulinda heshima yake, na kuepuka aibu kama iliyompata Mzee Malecela kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Mtera, kwa heshma na taadhima, namshauri aondoe jina lake na kujiondoa kabisa katika kinyanyiro hicho, kwa sababu naamini jina lake limepitishwa ili baadaye CCM wampatie zawadi stahiki kwa utaratibu wa "I fear the Greeks, especially when they bring gifts"!.

  1. Kwa hadhi aliyonayo, tena kigogo haswa wa hali na mali, hakupaswa kugombania na yeyote, haswa kwa kuzingatia mtu kama vijivigogo "mke", na kajikigogo "mtoto" wamepita bila kupingwa katika wilaya zao, iweje jigogo la mbuyu, jabali la majabali, na mwamba wa Kaskaxi, kama Lowassa, apingwe?, yaani wana CCM gani hao wasio na adabu hata kidogo, wamediriki kupenyeza pua kumkabili!, hii sii bure, iko namna!.
  2. Naamini, kati ya hao waliochukua fomu kushindana nao, kuna inplant aliyeshauriwa ampinge na kitakacho fuata kwenye Mkutano Mkuu, ni kushindwa kwa aibu!. Ili kuepuka aibu hii, ni bora kujiondoa mapema!.
  3. Japo mimi sio mwana CCM, ila pia siamini kabisa kuwa kote kule ambapo kuna waliopita bila kupingwa, ni kweli hakukuwa na wana CCM wa kuwapinga, bali wana CCM walizuiliwa kuwa kitendo cha kumpinga mke wa fulani, au mtoto wa fulani, ni utovu wa nidhamu kwa mwenye mke, au baba wa mtoto, hivyo utaratibu huo ungeweza kutumika, kumlindia heshima Edward Lowassa!, kitendo cha kutotumika kwa utaratibu huo, ni dalili za awali kuwa hatimaye, CCM itamtosa Lowassa kama ambavyo, watamtosa Sumaye!.
  4. Baada ya kuivunja CC ya zamani na kuiunda upya, zile kauli za Nape, Chiligati na Mukama kuhusu kuvuana magamba na hatimaye kuzunguka nchi nzima, hazikuwa zao, zilikuwa ni kauli "zake" kwa kuzipitishia kubata baraka za vikao halali, walipoona wamegoma, ndipo akaamua waache kuhubiri kuvuana magamba, na sasa kupitia ujumbe wa NEC, hawatamvua tena gamba, bali sasa watamchuna mzima mzima, mbele ya kadanasi ya watu na kumuacha akajifie mbele kwa kifo cha aibu!.
  5. Kwa wale mnaozikumbuka tuhuma za Nape dhidi ya Lowassa kuhusu ufisadi wa Jengo la Umoja wa Vijana wa CCM, kama Lowassa atapita NEC, hakuna wa kumzuia, kugombea urais 2015, hivyo akipita, itambidi Nape, Chiligati na Mukama, wapigwe chini, au kumpiga chini Lowassa once and for all!.
  6. Baada ya JK kubezwa sana kuwa ni "dhaifu" hadi watu kama kina Mkono kuamua kuitishia CCM kwa jeuri ya pesa zao!, kitendo cha JK kumpiga chini Mkono, ni ku proove kuwa yeye sio "dhaifu", hivyo kummaliza EL bila kuwajeruhi kambi yake, kwa kuzingatia yeye ni kigogo na samaki mkubwa aliyenona, dawa yake ni kumtumbukiza kwenye karai na vijisamaki vilivyokonda, ili ajikaange mwenyewe kwa mafuta yake mwenyewe!.
  7. NEC ingeweza kabisa kumchinjia baharini Lowassa, kwa kulikata jina lake kabla hivyo kutompitisha, hilo, lingewaudhi wafuasi wake, na wangeweza kufanya lolote, hivyo namna bora ya kumuondoa, ni kwa kumpatia zawadi ya Kigiriki kwa kulipitisha jina lake kama zawadi ya utangulizi, halafu kinachofuatia ndicho hicho ninachokiita "I fear the Greeks, especially, when they bring gifts"!.
  8. Mimi nilijiaminisha kuwa CCM imechokwa mpaka basi, na 2015, itapigwa chini jumla, hivyo ili kujiokoa, nilijua CCM ndio mnamhitaji Lowassa more than anything else, lakini baada ya kusoma mahali ile bajeti ya Sh. Bilioni 400 kuwahongea Watanzania masikini kwa kuibatiza jina la ruzuku "safety net", then yoyote atakayesimamishwa kugombea CCM, atashinda, hivyo kwa sasa, CCM haimhitaji tena Lowassa, hivyo kumtosa mzima mzima, the sooner the better, ni bora zaidi ili kumfungulia njia Membe bila zengwe!.
  9. Japo mimi humu jukwaani natambulika kama ni "mtu wa Lowassa", sijawahi kukaa nae popote zaidi ya kukutana nae kihabari, sijawahi kuhudhuria mkutano wake wowote na waandishi wa habari, sijawahi kupokea hata senti tano yake ili kumpigia, debe humu, bali nilijitolea kwa sababu niliamini ni kupitia kwake, Tanzania ingepata ule ukombozi wa pili wa Mtanzania, ila kabla ya Uchaguzi Mdogo wa Arumeru, Mashariki, nilimshauri Lowassa ifuatavyo,Ushauri: Lowassa Asikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!. hakunisikia, kilichofuatia sote tunakijua!, hivyo na huu ni ushauri mwingine, asiposikia subirini muone kitakachofuatia!.
  10. Edward Lowassa kwa CCM na urais wa 2015 ni kama Zitto Kabwe na Chadema kwa urais wa 2015!, both are powerful, action oriented, mabingwa wa mass mobilization, wana vipaji vya hali ya juu vya "visionary leadership", wote wana capabilities za kutupatia the "best presidents" this nation had ever had, na both wana the same weakneses, vote ni "egotists", very assertive, selfish, with unicentric view ambao wanaona upande mmoja tuu wa shilingi,, their side which is the right side, hawaoni, hawasikii, wala hawaambiliki, wanalotaka wao ni lazima liwe!.

  Ushauri, ni ushauri tuu, mhusika anao uhuru wa kuufuata au kuupuuza, mimi kama mshauri, nimetimiza
  wajibu wangu!. Kipimo cha umuhimu wa ushauri huu, au ubora wa hoja hizi, utapimwa kwa matokeo ya
  ushauri huu.

  Wasalaam.

  Pasco.
  NB. Pasco wa jf, ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, ila ni mshauri wa mambo ya kisiasa na hulipwa
  mahela mengi kutoa ushauri huo kwa wageni!. ila kwa hapa jf, hutoa ushauri wangu bure kwa kujitolea, bila kulipwa
  hata senti tano na yoyote, popote!. Baadhi ya shauri zangu, huzitoa kwa malengo maalum, ila ushauri huu
  wa leo, lengo ni kumsitiri tuu na aibu huyu Waziri Wetu Mkuu Msataafu.

  UPDATE!.
  Mkuu Kitilla, matokea yametoka, Lowassa kashinda kwa 99.9 %!. You are dam right, I'm very wrong!.
  Nakiri kukosea utabiri!, sasa tusubiri matokeo ya EL kuingia NEC!.

  Pasco.

  UPDATE 2.
  Wanabodi, hii nimeitoa kule Globu ya Jamii!.
  MONDAY, OCTOBER 01, 2012
  [h=1]MH LOWASSA ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA NAFASI YA UJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA WILAYA YA MONDULI[/h]


  [​IMG]
  Mh Lowassa akizungumza na kuwashukuru wapiga kura wake waliompatia ushindi wa kishindo
  [​IMG]
  Waziri mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,mh. Edward Lowassa akipongezwa mara baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu ya Wilaya ya Monduli uliofanyika leo katika ukumbi wa chuo cha ualimu Monduli,Mh Lowassa ameshinda kwa kishindo kwa kuwabwaga wapinzani wake kwa idadi ya kura 709,mpinzani mwingine ameta kura 44 na mshindi mwingine aliibuka na kura 7.

  [​IMG]
  Waziri mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,mh. Edward Lowassa akipongezwa mara baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu ya Wilaya ya Monduli uliofanyika leo katika ukumbi wa chuo cha ualimu Monduli,Mh Lowassa ameshinda kwa kishindo kwa kuwabwaga wapinzani wake kwa idadi ya kura 709,mpinzani mwingine amepata kura 44 na mshindi mwingine aliibuka na kura 7.  MY TAKE!.
  BAADA YA JK KUMPIGA PANGA MKONO, NILIAMINI SASA JK SIO DHAIFU TENA, HIVYO ANAYEFUATIA NI EDWARD LOWASSA ILI KUMSAFISHIA MEMBE NJIA NYEUPE YA 2015!.

  NAKIRI, I WAS WRONG, SIO NILIMU UNDERESTMATE LOWASSA, BALI NILI MUO OVER ESTIMATE JK!.

  KWA MATOKEO HAYO, KUBALINI, KATAENI, MSHINDI WA URAIS 2015 NI CCM!, NA RAIS WA 2015 NI EDWARD LOWASSA!.

  NB. KUNA BILIONI 400 "SAFETY NET" KWA WAPIGA KURA WA 2015!. BAADA YA KUJENGEWA DARAJA LA KIGAMBONI, MABARABARA YA JUU NA CHINI!, HUDUMA ZA AFYA NA ELIMU BURE!, SASA FAMILIA MASIKINI ZITAGAWIWA RUZUKU YA KUONDOA UMASIKINI!, 2015 NANI ATATHUBUTU KUIVOTE OUT CCM?, KWA VIGEZO GANI?.

  HONGERA LOWASSA!, HONGERA CCM!.

  Pasco!.

  NB: Naendelea kusisitiza Pasco wa jf, sio mwanachama, mfuasi, wala mshabiki wa chama chochote!. Sasa wale mnaoamini kuwa Pasco wa jf ni mshabiki wa CCM, endeleeni kuamini hivyo, if that will make you happy!.   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,876
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  Mie naomba nikuulize huu ushabiki wako mkubwa kwa Lowassa unasababishwa na nini hasa kilichowahi kufanywa na Lowassa hadi umshabikie kiasi hiki!?

   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,944
  Trophy Points: 280
  Pasco bana nilikuona kwenye graduation ya mwanao.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Sasa mbona unajitetea kuwa hujala visenti vyake...huoni kwa wenye fani zao wanaelewa wewe ni wale wale?
  Lowassa ana dalili kubwa ya kuanguka monduli....subiri kishindo kikuuu
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Lowassa akijitoa si ndio ataonekana naye ni dhaifu? Nashauri agombee - Liwalo na liwe.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,618
  Trophy Points: 280
  Mkuu BAK, kwa vile humu jf tuko wengi, sio rahisi wote kunielewa, ila ushabiki wangu kwa ELuna sabau, na humu wako wachache wananielewa!. Naomba sasa tuendelee kuijadili hoja iliyo mezani, na sio mleta hoja!.
  P.
   
 7. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Psco ni jembe Muda mwingine, sumaye kishadondoka, kaangushwa na mpenzi wake wa siku nyingi
   
 8. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Pasco, ushauri huu amekutuma NAPE uulete ha JF? lowasa kwa sasa anaona 2015 yy ndiye rais, Lakini wewe wajua CCM wamechanganyikiwa kwa sasa, karata yao hawajui waichangeje, mwisho ndg yangu pasco jiunge na M4C, tunaijua nguvu yako kaka, karibu chadema tuikomboe inchi yetu
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  dah kwa kweli wewe uko 'in love na Lowassa '
   
 10. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pasco,

  Na hii tena?

  Sasa unamaanisha kwamba ulikuwa ukimshauri weee na muda wote wote huo tuchukulie ulikuwa ukilipwa kwa ushauri huo.

  Sasa mambo yamekuwa magumu mbona unatoa siri tena? Halafu unasema mpaka mambo ya vijizawadi.

  Halafu nikukumbushe EL anafahamika kwa uwezo wake tokea Arusha hadi pale AICC mpaka kufikia hapo alipo na ndio maana watu wanacheza "traditional ngoma dancing".

  Ikiwa EL anaweza kuleta ngoma za kimasai ambazo watu huruka tu bila kusepa kidogo na kuleta madoido basi asahau neno "presidency na state house"
   
 11. b

  bdo JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Mbona unamzingua Pasco?..my take kwa Pasco:Mtoto akililia wembe acha umkate
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,618
  Trophy Points: 280
  Mkuu Saint Ivuga, jukwaa hili pia kumbe huwa unatembelea?, nimekozoea kule kwako!.

  Du graduation ya yupi, jumla ninao 6, nimehudhuria graduation ya mmoja mdogo kamaliza chekechea, anakwenda kuanza la kwanza, nikahudhuria ya mwingine kamaliza la saba hizi shule zxetu za Kayumba, anasubiri kuchaguliwa shule ya kata aanze form one!, pia nimehudhuria ya mwingine kamaliza form 4 hizi shule zetu za kata, wengine wawili pia nao wako sekondari hizi hizi za kata!, nilitamani sana wanangu nao wasome hizi shule za academy, ila kipato chetu sisi waandishi hakiruhusu!.
   
 13. b

  bdo JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Bora Lowasa kuliko Membe
   
 14. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  BAK,

  Unajua masuala yafuatayo carry totally different meanings when attended individually:


  • A Fan – Mshabiki;
  • A Follower – Mfuasi;
  • A Supporter – Kumuunga mkono mtu;

  Mimi nadhani Pasco angekuwa na majibu kwa swali lako iwapo angesema yeye ni Follower au Supporter kwani by being a follower or supporter, it involves a certain ideological belief, or school of thought or political orientation; Vinginevyo kwa suala la ushabiki, nadhani utakuwa unamwonea tu Pasco kwani sote tunajua chanzo cha ushabiki in any context ni nini – mara nyingi hutokana zaidi na FAME OR ACHIEVEMENTS/ACCOMPLISHMENTS za anayehusika, iwe ni timu ya michezo, muigizaji filamu, mwanamtindo, mwanasiasa n.k

  Pasco wakati wote amekuwa akijieleza in that context i.e. anajenga hoja zake kwa vigezo vinavyolalia zaidi
  FAME OR ACHIEVEMENTS/ACCOMPLISHMENTS, na ni haki yake kufanya hivyo, ili mradi anaeleweka namna hiyo na yeye analijua hilo. Vinginevyo kama nia ya Pasco ni kukukusanya watanzania kwa levels zaidi ya ushabiki, ni muhimu abadilishe his style of presentation na iegemee zaidi towards him being a ‘FOLLOWER' OR ‘SUPPORTER', otherwise kwa mtindo wa SHABIKI, atazidi kuacha watu na maswali mengi kuliko majibu, huku muda kuelekea 2015 ukizidi kuyoyoma;
   
 15. M

  Moony JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Ai Pasco nigawieko hayo mahela
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,876
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  Mie siulewi ushabiki huu unatokana na nini hasa hivyo nakuomba unieleweshe. Hata kama watakaokuelewa watakuwa wachache lakini utakuwa umeziweka hadharani sababu zako kuu za wewe kumpigia debe la nguvu Lowassa.

   
 17. G

  GHANI JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 685
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  That real
   
 18. M

  Moony JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Lakini si unalipwa mahela mengi kwenye ushauri?.......peleka watoto academy bana
   
 19. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Pasco again......Huwa namuona hayuko serious anapozungumzia mada kama hizi, I strongly believe anafanya mzaha fulani wa kiuandishi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. b

  bdo JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Achana na Malecela, mavi ya kale hayo: Mbona haukumshauri Sumaye?au mavi ya kale pia,
   
Loading...