Ushauri wa bure kwa Mbunge Musukuma(CCM)

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Ingawa nipo safarini kuelekea Arusha katika Mkutano wa nusu mwaka wa TLS,nimewiwa kumshauri jambo Mbunge wa Geita Vijijini,Ndugu Joseph Kasheku 'Msukuma'. Ushauri wangu unafuatia kadhia iliyompata ya kukamatwa na kushtakiwa kwa kuhujumu miundombinu ya maji

Ndugu Msukuma amekuwa na juhudi za kumsema na 'kumtisha' Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Geita,kabla na baada ya kukamatwa kwake. Amekuwa akimzungumzia RPC wa Geita kana kwamba ni raia wa kawaida anayeweza kumsema kisiasa atakavyo. Pia,Msukuma,kwa uelewa wangu,analenga 'kumchongea' RPC wa Geita kwa wateule wake.

Nataka kumpa taarifa Msukuma,na kumshauri. Kwanza,polisi si raia. Polisi hawana chama. Polisi ni chombo cha dola;chombo cha Serikali na wananchi kwa ujumla. Polisi wanapaswa kuheshimiwa kwakuwa wanafanya kazi kubwa kwa ulinzi wetu na ulinzi wa mali zetu. Msukuma anapaswa kuwaheshimu polisi na kuwaweka mbali na mikwara yake ya kisiasa.

Serikali ni yetu sote. CCM si watanzania wote na hivyo Msukuma asitambie. Kwakuwa tayari jambo lake liko mahakamani,anapaswa kunyamaza kimya na kushughulika na jambo lake. Kumsema na kumtisha RPC hakutamsaidia. Anaowategemea wamsaidie kichama wako kimya kwakuwa wameona kuwa Msukuma hana hoja!
 
Ukitoka Arusha nenda Geita kamsaidie uwakilishi ama sivyo ataishia kule alikokua anawacheka kina Lema. JPM siyo kama wanamdhani. Mkutano mwema mtani
 
Uwe unaangaliwa watu wa kuwapa ushauri.
Mtu kama msukuma, ni wa kumpuuza tu
Nyerere alituambia binadamu wote ni sawa hivyo si kubagua watu ktk kutoa ushauri maana kijana Petro pamoja na kupewa mkopo kama kasomo wakati wa mikopo bado walipa kodi walichangia ilimu yake yaani pamoja na Msukuma
 
Serikali na polisi wenyewe wamewadekeza sana wanaCCM na kuona kwamba hakuna mtu au chombo chochote cha kumsumbua mwanaCCM. Yaani CCM na watu wake huona polisi ni kama tawi la CCM na ndio maana mwanaCCM anaweza kumuagiza RPC akamshughulikie Lema na kweli anaenda kufanya hivyo. Wangajitenga na kufanya kazi kwa misingi ya kipolisi msukuma hangekuwa na ujasiri wa kutoa kauli kama hizo. Mbona hawatoi kauli kama hizo kwa JWTZ? Ni kwa sababu JWTZ kwa sehemu kubwa imejitenga na siasa uchwara kama hizi tunazozishuhudia.
 
"wanaCCM msijibanze kwenye kwapa za polisi. jibuni hoja za wapinzani bila kutegemea polisi" (JK 2013/14)
 
Nadhani kunahitajika semina elekezi kwa viongozi waandamizi wa vyama vya siasa kuhusu uendeshaji wa serikali..Musukuma ni kijana na siasa serious kwa umri wake atakuwa amezianza miaka ya 2000 hivyo nilitegemea atakuwa anafanya kulingana na mabadiliko yaliyojitokeza baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi.

Yaani kifikra bado yupo enzi zile za chama kushika hatamu ya uongozi ambayo tuliachana na huo utaratibu mwaka 1992 ambapo shughuli za serikali zinabaki kuwa za serikali na za vyama zinabaki kuwa za vyama
 
Back
Top Bottom