Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,474
- 7,894
Mbunge wa Geita, Musukuma amesema alikuwa bingwa wa kutorosha dhahabu mpakani akibeba mpaka kilo 50 mwilini.
Musukuma amesema mwaka 1996 alikuwa na umbo dogo kimwili hivyo kuonekana kama mtoto, askari wakishusha watu kwenye basi ili wasachiwe, walikuwa hawasachi watoto hivyo alikuwa hakaguliwi kwakuwa alionekana kama mtoto japo alikuwa na mtoto mmoja tayari.
Kishimba
Musukuma amemtaja mbunge mwenzie, Kishimba kufungua ofisi ya kurudisha fedha kwani pia ilikuwa changamoto kuzifusha.
Kufilisika
Pia ameongea kufilisika mwaka 1998 baada ya kutapeliwa mpaka kuamua kutoroka kwani alikuwa anatafutwa na polisi ilhali yeye alikuwa anawaogopa sana. Alipotoroka alitelekeza familia na kuwa shoe shine Korongwe pamoja na kwamba alishakuwa mfanyabiashara mkubwa namba 3 Mwanza.
Kuibuka tena
Msukuma amesema kuna mfanyabiashara mpakistan alimsaidia wakati ana duka Mwanza, alileta ngano na TRA ikaishikilia na mpaka anafanikiwa kuitoa ilishaanza kuharibika. Ilipotoka akamtafuta msukuma ambae alifanya 'namna' ikauzwa nje. Msukuma amesema ile ngano alikopeshwa kwa miezi mitatu lakini alipouza tu alimlipa mhusika ndani ya siku 5.
Musukuma ameongea hayo leo July 6 wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power breakfast.