Mimi sio sawa na wale waislamu wanaondeleza sera na itikadi za kale. Ni mwislamu anayependa mabadiliko ya mfumo wa kale wa maisha ambao tunao mpaka sasa.
Geuza mfumo kutoka elimu ahera kwanza na kuwa elimu dunia kwanza ili tupate wasomi wa kupambana na huo unaosemekana mfumo kristo, mapambano ya kweli hayawezi kuletwa kutokana na kusoma hadithi za kale katika madrasa.
Tukitaka tuushinde mfumo kristo ni lazima wanetu wazingatie sana elimu dunia. Elimu isiyo rasmi unayoikazania wewe haina msaada wa ukombozi kwa waislamu kaka.
Mimi si mwislamu wa majungu, wala si mwislamu mgombea sadaka, wala si mwislamu wa kuzurura kutwa kucha misikitini na mabegi begani.
Mimi ni mwislamu ninayetaka kuwakomboa waislamu kutoka katika urithi wa utumwa wa fikra kutoka kwa waarabu wa kale.
Bless you sir!